- Thread starter
- #121
Nakubaliana na hoja yako ninachotaka mimi sio kushindana na huyo ex wake kwenye manjonjo ama la,nataka heshima yangu irudi na ule upendo ulionidrag hapa uendelee kugrow....sitakata tamaa ntapambana tu ila naamini machozi yangu hayataenda bure kuna siku Mungu atanilipia tu.Mume wangu ntaongea nae kwa adabu na upole na kirafiki juu ya hili jambo na kama kuna kitu anaona siko swa ntamuomba anieleze wazi ili nijirekebishe na ntamuomba tuweke mikakati ya pamoja katika kuinusuru ndoa yetu ikiwa ni pamoja na kukata mawasiliano na huyo ex maadamu hayana faida kwetu zaidi ya kuharibu tu...Nakubali kuna ex wanaweza kuwa rafiki kwa maana ni wastaarabu na wanajua nyajibu zao ila wengine wako katika kuharibu tu furaha za wenzao na si vinginevyo,nitampa ushauri mzuri ambao naamini utakua na matokeo chanya baina yetu wawili