Kweli Ndoa yataka Moyo.....

Kweli Ndoa yataka Moyo.....

Ndugu zanguni yamenikuta na naomba ushauri wenu,Mimi ninaishi na mume wangu yapata miaka miwili sasa,nina mpenda sana Mume wangu na ninaamini kuwa naye ananipenda pia.Ila kuna tatizo linanisumbua sana juu yake ambalo linanipa wasiwasi kiasi kwamba nashindwa kuelewa hatma ya mahusiano yetu ya ndoa kwa maana ya kwamba nahofia yasije yakaingia shubiri na ile imani nlionayo juu yake ikateteleka.Ni hivi kabla ya kunioa mimi aliwahi kuwa na mahusiano na wanawake wengine ila mwanamke wa mwisho ambaye aliachana nae amekua akiendelea kuwasiliana na mume wangu na kila ninapohoji juu ya hilo Mume wangu hunijibu kuwa hauna kitu kinachoendelea baina yetu ni rafiki yangu tu wakawaida na hana shida yoyote na sisi kwanza huwa anapiga simu na kutuma meseji za kutujulia hali,anyways nimejitahidi sana kuwa na mtizamo chanya na kuuambia moyo wangu uamini hivyo.Ila siku zinavyokwenda nikaona mazoea yanakua sio mazuri kwa maana wakati mwingine humpigia simu ana hutuma meseji humueleza mume wangu kuwa amemmiss sana na anataka kuonana nae na vitu kama hivyo.Nlimwambia mume wangu mawasiliano na huyo mpenzi wako wa zamani hayanibariki hata kidogo naomba uwe na mipaka na ikibidi uache kwa maana yananiumiza mimi zaidi,aliniahidi kufanya hivyo na kweli kwa kipindi fulani kazi ilipungua ila sasa leo ametuma tweets kuhusu mume wangu kwenye mtandao wa twitter kitu ambacho kimeniuma maana anaeleza jinsi anavyofurahia tendo la ndoa na mume wangu na baada ya kuliona hilo nkampigia mume waqngu kumweleza akaniambia atampigia simu kumsema juu ya hilo na kumuonya.Badala yake kilichotokea yule mwanamke alituma tweets za kunitukana na kunidhalilisha mimi kitu ambacho kinaniuma sana kwa maana mume wangu anasema yule mwanamke ni rafiki mzuri tu na hana shida hata kidogo.Nisaidieni ushauri ndugu zangu je niendelee kuvumilia hayo yote yanayojitokeza na kuamini maneno ya mume wangu kuwa huyo mwanamke hana shida na sisi ama nifanyenye?Naomba ushauri wenu katika hili.....

mdada ndoa hujengwa na wawili. Kaeni pamoja mjadili kinyume na hapo ndoa inaweza kuwa chungu. Kwani huyo mdada c rafiki mwema bali nji m2 mbaya kwenu na hasa kwako
 
Ukitaka kuishi kwa raha na furaha acha kufatilia mambo yake ya nje ya mumeo, ili mradi tu awe anatimiza mambo yako ya muhimu, yaani... chakula cha mchana na kile chakula muhimu cha usiku na mengineyo ambapo tukitaka kuyaorodhesha yote hapa wino utaisha bila kuyamaliza.
 
shost kusoma hujui hata picha nayo huoni,hapo unaibiwa,jamaa bado ana mahusiano na huyo dada,kama vp vizia cm yake utajua ukweli,au anzisha timbwili la kupinga kuwasiliana kwao,wanakuchora hao aisee,ila poleeeee!
 
FP, umesema yote, hicho huwa ni kipindi cha majaribu, wengi wetu tumekipitia, be strong, watu tulifika hatua ya kulaliwa nje na humuulizi kalalia pande zipi na asubuhi anakuta umemwandalia kila kitu ye ni kuoga/kubadili hapo hujui kama atarudi au atalala huko huko, tumekipita pia, sasa hivi tunalisongesha kwa sana tu, na majaribu kama haya kwa wengi wetu tukiyavuka yanatupa ujasiri wa ajabu.
 
Yeah nakuunga mkono mkuu ulichosema ni kweli 100% ingawa inahitaji moyo wa pekee na ujasiri wa hali ya juu kusolve ishu kama hiyo kwa njia hiyo.
nataka kubaki maana nampenda sana mume wangu kutoka moyoni[/QUOT

Sasa sikia,unachotakiwa kukifanya ni kigumu lakini ni dawa kubwa sana. Puuza vitimbi,maruerue na makorokocho ya mume wako kwa huyo mwanamke mwingine. Achana na kufuatilia mawasiliano ya mume wako na huyo mwanamke mwingine.

Ni hivi,binaadamu ameumbwa kama kiumbe mpenda sifa.Unapomfuatilia na kumhojihoji mumeo ndipo yeye anapoongeza manjonjo ya mawasiliano na huyo mwingine ili akuumize zaidi. Unamfanya ajidai kuwa 'kwake umefika' na hauna jinsi. Anavimba bichwa. Anakudharau. Anakupuuza.

Mpuuze naye aone anachokifanya ni upuuzi. Lakini,siku moja moja chachamaa na utishie hata kumlazimisha kupima afya. Atafyata mkia. Ndoa yako itakuwa salama.

Fanya hivyo uone
 
Hongera sana kwa kuishinda mitihani migumu kiasi hicho,ila pia pole sana kwa kupitia kipindi kigumu sana kama hicho.
FP, umesema yote, hicho huwa ni kipindi cha majaribu, wengi wetu tumekipitia, be strong, watu tulifika hatua ya kulaliwa nje na humuulizi kalalia pande zipi na asubuhi anakuta umemwandalia kila kitu ye ni kuoga/kubadili hapo hujui kama atarudi au atalala huko huko, tumekipita pia, sasa hivi tunalisongesha kwa sana tu, na majaribu kama haya kwa wengi wetu tukiyavuka yanatupa ujasiri wa ajabu.
 
hakuna urafiki wa mwanaume na mwanamke ambaye alikuwa X wake,lazima wanado.Mmeo lazima akufiche.Na inawezekana yule demu anapewa kichwa na mme wako,kwa nini akutukane?ila vumilia ndo ndoa hiyo.
Hujaulizwa
 
Back
Top Bottom