Kweli nimekutana na tapeli wa mapenzi

Kweli nimekutana na tapeli wa mapenzi

Demu unayekutana naye gesti asitahiri kuwa mke wako.Huyo muweke kama akiba wa kuokoa jahazi wakati mambo si mambo.Gest .? tena uchochoroni.?Na we demu unayeperekwa gest.?
gest za uchochoroni nazo zinaraha yake sio kila siku movenpick
 
Achana nae atakupotezea muda! Akikupigia simu.....ipokee alafu iache hewani, usiongee lolote! Msg usijibu pia. Huyo ni pepo hajielewi!
Msichana,niliepanga kufunga nae ndoa na tena anafahamika hadi kwetu,amenifanyia mambo ya ajabu.

Ilinichukua miezi minne tangu nionane nae mara ya mwisho.Tukiwa gest nikakuta kuna namba mbili moja kasevu LOVE na nyingine SWEET.Namba hizi zote ni za mwanamme mmoja anatumia mitandao miwili tofauti.

Nilipomuliza alikiri,na kuomba msamaha mimi nikakubali.

Cha ajabu siku nyingi baadae akanipigia simu kidume wake akanichimba mkwala,na pia alimfosi demu wangu aongee mbele yangu kua hanitaki,kweli alifanya hivyo.Nami nikwamwambia sawa.Hatimaye akanambia nisimpigie simu.Lakini nashangaa yeye ndo amekua wa kwanza kunipigia,kunitumia meseji na kuniomba hela na wakati mwingine anajifanya ananisalimia.Je!Nimjulishe mtu wake?
 
Mkuu Chipanje, huu uzi wa leo na huyu msichana unayemsema vina uhusiano wowote na ule uzi wa jana?! Ebu nijibu kabla sijakuona wewe ndo tapeli unayehangaisha watu humu kwa visa vya uongo.
 
Si bure kutakua kuna kidafu hapa, huwezi kuwa bado haujui la kufanya
 
Demu unayekutana naye gesti asitahiri kuwa mke wako.Huyo muweke kama akiba wa kuokoa jahazi wakati mambo si mambo.Gest .? tena uchochoroni.?Na we demu unayeperekwa gest.?

wazee wa zaman mna matatizo kwel,we hujui hilo ndo eneo pekee la kufanyia uzinifu ambao hata wewe huwa unaufanya bila shaka...wanao wanafanya na sisi vijana wenzao...uzinifu ni uzinifu tu hata kama ukiufanyia kanisani
 
sichoki kurudia hii: 'advice is what we ask for when we know exactly what to do bt dont wanna do it'. .[/QUOT

Hapo ndio yote ..mshukuru Mungu kwa kukuonyesha mapema wengi hawapati bahati hiyo wanafunga ndoa huko ndani ndio wanakutana nacho ......Mke mwema mtu hupewa na bwana...so huyo hafai kuwa mkeo na hata huyo jamaa atakuwa anapiga tuu mda ukifika atamtema mazima
 
Mkuu Chipanje, huu uzi wa leo na huyu msichana unayemsema vina uhusiano wowote na ule uzi wa jana?! Ebu nijibu kabla sijakuona wewe ndo tapeli unayehangaisha watu humu kwa visa vya uongo.

Yah kaka,ni kisa cha kweli kabisa.Naomba niseme kwa kumuogopa Mungu,uzi bado unamuhusu yule yule wa jana.
 
sichoki kurudia hii: 'advice is what we ask for when we know exactly what to do bt dont wanna do it'. .[/QUOT

Hapo ndio yote ..mshukuru Mungu kwa kukuonyesha mapema wengi hawapati bahati hiyo wanafunga ndoa huko ndani ndio wanakutana nacho ......Mke mwema mtu hupewa na bwana...so huyo hafai kuwa mkeo na hata huyo jamaa atakuwa anapiga tuu mda ukifika atamtema mazima

Kaka,nimeukubali ushauri wako.We ni great thinker!
 
Msichana,niliepanga kufunga nae ndoa na tena anafahamika hadi kwetu,amenifanyia mambo ya ajabu.

Ilinichukua miezi minne tangu nionane nae mara ya mwisho.Tukiwa gest nikakuta kuna namba mbili moja kasevu LOVE na nyingine SWEET.Namba hizi zote ni za mwanamme mmoja anatumia mitandao miwili tofauti.

Nilipomuliza alikiri,na kuomba msamaha mimi nikakubali.

Cha ajabu siku nyingi baadae akanipigia simu kidume wake akanichimba mkwala,na pia alimfosi demu wangu aongee mbele yangu kua hanitaki,kweli alifanya hivyo.Nami nikwamwambia sawa.Hatimaye akanambia nisimpigie simu.Lakini nashangaa yeye ndo amekua wa kwanza kunipigia,kunitumia meseji na kuniomba hela na wakati mwingine anajifanya ananisalimia.Je!Nimjulishe mtu wake?

Wanaume wengine mnakuwa kama mmebemendwa, ushauri gani unataka hapo? Huyo si mwanamke ni jambazi la mapenzi, (Bullshit). Tafuta mwingine haraka au undelee nae ili uwe mume *****! lol
 
Pole sana,ila usiwe mwepesi wa kwenda na mtu gesti wakati hujamfahamu vizuri.
 
....teh teh teh. Mwite, mwambie ampigie simu bwanake na amkane mbele yako.
Kisha uachane nae ni kimeo.
Inaonekana kuna mtu anamshikia mawazo yake.
Ila kama wampenda na unahisi waweza kumbadili tabia, endelea nae....
 
Ahhh mambo mengine haihitaji utumie hata nguvu kujiuliza 1+1=2
Haihitaji utumie akili ya kuzaliwa kujua kuwa huna nafasi ya kubadilisha mambo
Songa mbele achana na huyo mtu na wala usitake mawasiliano naye maana anaonekana anahitaji kukuchuna na sio kuwa anataka lolote kwako
Tayari ana mtu wake ya nini anatafuta mawasiliano na wewe wakati kashakutema
 
Nadhani anaeneleza yale mabo yenu ya siku hizi vijana wa dot com,kwamba mnaweza kupigana chini mkabaki marafiki......labda na yeye anakuchukulia hivyo.....rafiki!.....tuma pesa kijana si ndio life style zenu jamani........enzi zetu huo ukurasa ulishafungwa bwana,unamwambia kabisa akikuona unakuja abadilishe njia au atafute kichochoro ajifiche mpaka upite!

Msichana,niliepanga kufunga nae ndoa na tena anafahamika hadi kwetu,amenifanyia mambo ya ajabu.

Ilinichukua miezi minne tangu nionane nae mara ya mwisho.Tukiwa gest nikakuta kuna namba mbili moja kasevu LOVE na nyingine SWEET.Namba hizi zote ni za mwanamme mmoja anatumia mitandao miwili tofauti.

Nilipomuliza alikiri,na kuomba msamaha mimi nikakubali.

Cha ajabu siku nyingi baadae akanipigia simu kidume wake akanichimba mkwala,na pia alimfosi demu wangu aongee mbele yangu kua hanitaki,kweli alifanya hivyo.Nami nikwamwambia sawa.Hatimaye akanambia nisimpigie simu.Lakini nashangaa yeye ndo amekua wa kwanza kunipigia,kunitumia meseji na kuniomba hela na wakati mwingine anajifanya ananisalimia.Je!Nimjulishe mtu wake?
 
Kwani umemuoa? Mwanamke unaeweza kutembea nae wewe nje ya ndoa anaweza akatembea na mwanamme yoyote yule, huna hati miliki.

Halafu nawapa nasaha vijana, mwanamke wa maana haswa, si yule ambae anahitaji matumizi yake ya kila siku kutoka kwako. Mwanamke anaehitaji kutoka kwako huyo yupo katika biashara na mfanya biashara huwa na wateja wengi na tofauti.

Astahili yenu yawapate na mtaendelea kupatikana hivyo hivyo kwa uzinzi wenu.

Nawashangaa sana kuona kuwa kuwa na mwanamke au mwanamke kuwa na mwanamme (boy friend/girl friend) mnaona kuwa ni sifa au uhodari. Sifa ya mwanamme au mwanamke ni kuwa na mume/mke wa ndoa.

Hivi haya maadili huwa mnafundishwa wapi? Taifa omba omba huanzia kwa hawa wazinzi wa kike na wa kiume. Zinaa huongeza ufukara, si wa mali tu, bali hata wa mawazo. Jiulize, hivi mwanamke anaeweza kukuvulia nguo kabla hujamuoa anaweza kukushauri nini cha maana? Wakati wana falsafa wanasema kuwa "kuna mwanamke mwenye nguvu nyuma ya kila mwanamme mwenye mafanikio". Sasa mwanamke nguvu za nini? Nguvu za mawazo na si misuli. Anaeweza kukuvulia chupi nje ya ndoa hana nguvu za mawazo au ni mfanya biashara ya kuuza mwili wake. Hivi mkivuliwa nguo mnajiona mahodari na mmepata? Mnanchekesha! Wenzenu huwa wanaona "lione jinga hili limepatikana".
 
badilisha number,usimpe huyo msichana number yako mpya,kuwa mwanaume na wewe mwambie live humtaki..?!
 
Da Mkuu na hili tena unataka ushauri kha,nakumbuka kalikawe alishawahi kusema "panapofuka moshi ujue mbele kuna moto" mkuu sitaki uje kukutana na moto hapo mbele kwakua ushamjua huyo msichana cha msingi ni kufungasha virago na kuondoka vijana wa kileo wanasema unaamsha
 
Hivi kaka unajua jinsi yakusoma alama za nyakati?
Hayo ni mambo yakik kulipizalipiza visasi,wewe ukina kol yake ispokee akiandika msg delete kabla yakusoma, akizidi mwambie utamchukulia hatua za kisheria.Hawezi kukufanyia ushenzi ule alafu anajikosha she got some nerves.
Mwanaume lazima uwe jasiri tena si katika kupambana na mwanamke bali maisha bro
 
Back
Top Bottom