Pinda na yeye aache kupindisha mambo. Amekuwa serikalini akilipwa mshahara kwa zaidi ya miaka thelathini.Mshahara wake kwa kujinyima tu anasa angeweza kuwajengea wazazi wake nyumba nzuri tu na ambayo ni sawa na hadhi ya mshahara wake. Kuna waalimu tena wa shule za msingi wana nyumba bora na wanalima na kufuga kwa njia ya kisasa. Sitegemei kuona waziri asiye badilisha hali ya wazazi wake pamoja na jamaa zake kwa kuwahamasisha kubadili mtindo wa maisha eti tu kwa kuogopa kuonekana jajiri. Kama umeumbwa kutokukubali mabadiliko hata ukiwa rais, bado hutobadilika. Si tegemei mimi niteuliwe kuwa waziri mkuu, nikiwa na wazazi wangu wote nishindwe kuwanunulia nguo nzuri tena za kuvutia eti kwa kuogopa mimi kuonekana tajiri.