Kweli sasa naamini CHADEMA wana maslahi fulani wanayoyapata wakivichokoza vyombo vya dola vikachokozeka

Bhisumbinyama

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2019
Posts
797
Reaction score
581
Ndugu wanajamvi!

Nakusalimuni nyote!

Tangu mama Samia ashike madaraka baadavya kifo cha bwana yule mama wa watu amechukua mrengo wa kiungwana huku akionesha dhamira ya kweli kutoka moyoni mwake kuliunganisha taifa lililokuwa limesambaratishwa na hayati bwana yulee.

Mambo yamekuwa yakienda vema kiasi kwamba mama akawa anaombwa na CHADEMA ahudhurie shughuli zao ambapo alihudhuria shughuli ya wanawake wa CHADEMA na wakamshangilia vema.

Ameendesha nchi kwa haki mpaka Mbowe kaondolewa mashtaka bandia na Lissu kapewa haki zako alizodhulumiwa na utawala wa hayati bwana yule.

Sasa sijui baada ya kula maharage ya wapi, wakaanza kumuandama na kumumbagua kwa uzanzibar wake huku wakikodi wanasheria wa kumtukana kama akina Nshalla na chapombe Mwabukusi bila hata hashima kabisa.

Wakaona haitoshi wakakodi baadhi ya watu wa makanisa kama akina Kitima na Mwamakula kuungana nao kumshambulia Rais lengo likiwa washitakiwe kisha mabwana zao wa nje ya nchi wawatetee! Kwa kweli CHADEMA ni genge ovu sana siyo chama cha siasa. HAKIFAI.
 
ONDOKA DPWORLD Samia arudi kwao makunduchi hadi Sasa kazi yake ipi
 
😂😂 ati demokrasia!! Who told you...? ruling people democratic for 100 percentage is like to welcome your neighbor kids to play with your eyes!!

Watakutofoa tu..! Watu waongoze 50 demokrasia hizo nyengine changanya na zako!. Ukiwachekea watakucheka!.
 
Wewe unaweza kujibu hoja eti kwa kuwa Rais ni mzanzibar hapaswa kushughulikia uwekezaji Tanzania bara na kama anataka aanze na Zanzibar! Sasa hapa kuna hoja gani ukabila na ubaguzi mtupu!! Lol!
Unaruka ruka maneno
 
Nadhani tuwapuuze tu CHADEMA kwasababu ndo kazi yao inayowaweka mjini. Wasipopinga watakuwa sio wapinzani tena.

Tuwaache wafanye kazi yao ya checks & balance ila nao wasivuke mipaka. Kuanza kuleta hoja ya uzanzibari na utanganyika ni upumbavu usioelezeka kwa Mbowe na chama chake.

Wananchi wanawaandalia adhabu kwenye sanduku la kura kama ilivyo kawaida na desturi kwenye uchaguzi mkuu.
 
Eti jibuni kwa hoja 🥸chadema wanahoja gani zaid ya ubaguzi msijifanye mnaonewa kwa upumbavu wa wanasiasa. Rais Samia yuko vizur kwenye utawala ukiangalia swala la bandari vizur utagundua upotoshaji mkubwa mno

Mbeleni mkija jua itakua aibu kwenu pale bandar itapokua imekamlika na maisha yakawa nafuu

Hakuna asiejua unafki wa nchi hii hatuna jema hata kidogo

Huo uzalendo mnaojificha nao ni unafiki mkubwa
 
Ndugu wanajamvi!

Nakusalimuni nyote!

Tangu mama Samia ashike madaraka baadavya kifo cha bwana yule mama wa watu amechukua mrengo wa kiungwana huku akionesha dhamira ya kweli kutoka moyoni mwake kuliunganisha taifa lililokuwa limesambaratishwa na hayati bwana yulee.

Mambo yamekuwa yakienda vema kiasi kwamba mama akawa anaombwa na CHADEMA ahudhurie shughuli zao ambapo alihudhuria shughuli ya wanawake wa CHADEMA na wakamshangilia vema.

Ameendesha nchi kwa haki mpaka Mbowe kaondolewa mashtaka bandia na Lissu kapewa haki zako alizodhulumiwa na utawala wa hayati bwana yule.

Sasa sijui baada ya kula maharage ya wapi, wakaanza kumuandama na kumumbagua kwa uzanzibar wake huku wakikodi wanasheria wa kumtukana kama akina Nshalla na chapombe Mwabukusi bila hata hashima kabisa.

Wakaona haitoshi wakakodi baadhi ya watu wa makanisa kama akina Kitima na Mwamakula kuungana nao kumshambulia Rais lengo likiwa washitakiwe kisha mabwana zao wa nje ya nchi wawatetee! Kwa kweli CHADEMA ni genge ovu sana siyo chama cha siasa. HAKIFAI.
Nikusahihishe@Bhisumbinyama
1. Mbowe hakufunguliwa mashitaka bandia na bwana yule ila bi huyu mwezi Julai 2021 ambapo bwana yule alikuwa hayupo duaniani
2. TAL hakushambuliwa kwa risasi na bwana yule ila ni hao wanaolazimisha watanzania wamwite bi huyu mama

Funguka ufahamu wako msimsingizie JPM ambaye hayupo kujitetea na kauli zenu za kukosa nguvu kihoja.
 
Sawa bwana Luhanga mpina nimekuelewa.
 
Back
Top Bottom