Turidi kwenye suali la msingi, jee wananchi waislam walio shambuliwa na kuuliwa na na polisi wa tanzania walikua magaidi ?
- ushahidi gani kwamba upo ?
- jee sio kweli kwamba uonevu wa wananchi wale kulazimishwa na kunyanganywa mazao yao na polisi/mgambo na halmashauri ndio zilisababisha vurugu Kilindi?
- jee vurugu zile za kukataa kulipa kodi kwenye mihogo ya masikini hawa si ndio ilio sababisha vurugu na hatimae mgambo mmoja na wananchi wengi kuumuizwa. na badae huyo mgambo akafariki?
- jee sio kweli kwamba kifo kile cha sokoni kwenye vurugu za wakulima wa mihogo walokataa kuonewa ndio ilio sababisha polisi waje na ffu wote wa Tanga kuja kulipiza kisasi ?
- jee hawa polisi walikua halali kupiga mji wote , kuchoma mota nyumba za watu, kuharibu mazao yao?
- jee baada ya kufanya unyama huu wa kuua hovyo kwa chuki za kidini kabisa ..mkuu wa polisi masawe akageuza kibao wananchi wale masikini kuwa wana pigana na magaidi ?
- akavamia madrasa zao waislam na kuwasingizia ugaidi ?
- jee polisi wale baada ya kuharibu na kuua , walifanya unyama ule kwa maelekezo ya nani ? ya Kikwete? Ya Said Mwema? au ni chuki ambazo askari wale wamepandikizwa juu ya waislam
imekua ni tabia ya polisi na serikali kufanya unyama na baadae kusingizia waislam ni magaidi wamefanya kule mbagala...
wamefanya zanzibar ...wamefanya kilindi...na wamefanya mtwara..haya ndio masuala ya kujibu kwa nini ? kwa faida gani ? kwa maelekezo ya nani ?
na jee kwa nini kusifanyike uchunguzi wa yale yalio tokea kilindi na mtwara? wanaficha nini ? wanaogopa nini ? na kwanini mbunge wa kilindi Shelukindo mkristo anashindwa kutoa kauli ambapo wapiga kura wake wapo porini kukimbia risasi za polisi ? kwa nini anashindwa kulisemea hili? kazi ya mbunge ni nini ? au kwa vile kijiji kile kina waislam na walopigwa ni pamoja na imam wa msikiti.
ya yesu hii sio mada yake....hapa kuna watu wamekufa....
Bopwe,
Ndugu yangu nalazimika kukupa hogera kwa haya ulosema.
Ngoja nikuongeze kitu.
Wakati hawa ndugu zetu wamesombwa na kufunguliwa mashtaka na kuwekwa
rumande Handeni ilitokea ibra ya ajabu.
Askari jela Waislam wakawa wanawatazama kwa karibu sana hawa mahabusu.
Walichogundua ni tofauti kubwa kati yao na mahabusu wengine wa kawaida.
Waislam mahabusu walikuwa wapole na wakimya kupita kiasi.
Siku moja wakati wanaswali huyu askari mmoja Muislam akawa anawaangalia
na akagundua kuwa katika safu wapo hata wale mahabusu jeuri.
Hili lilimshangaza na kwa kweli mahabusu ile ghafla ikabadilika hapakuwa na ugomvi
wala uvutaji bangi.
Lakini kilichomgusa aliwaona baadhi ya Waislam wapo kwenye sala na machozi
yanawatoka.
Baada ya sala akamwendea mmoja kumuuliza kipi kilikuwa kinamliza.
Yule mahabusu akamjibu, ''Imam alikuwa anasoma sura ambapo Allah amewasifu
Waislam na akawaeleza yale yatakayowakuta kutoka kwa makafiri. Mwisho
Allah akaahidi ushindi. Hiki ndicho kilichokuwa kikiniliza kuwa Allah kwa rehema
yake kanitia mimi katika kundi la wale walidhulumiwa kwa si kwa lolote ila kwa
kusema Mungu wangu ni mmoja ili aje anilipe hapa duniani na kesho akhera. Hiki
ndugu yangu ndicho kinachoniliza.''
Yule askari Muislam hakuchoka akataka kujua mengi kuhusu ugaidi Al Queda, Al
Shabab na wao wanavyohusika.
Yule Muislam akasema kuwa kama wangelikuwa wao wanahusika na ugaidi siku
nyingi wagelikuwa wameshakamatwa.
''Sikiza ndugu yangu. Hawa ndugu zetu kinachowakera ni huu Uislam wetu hakuna
kingine.''
Kwa muda yule askari alikaa kimya ameinamisha kichwa.
Aliponyanyua kichwa machozi yalikuwa yanamtoka.
Akasema,''Iko siku hizi bunduki tunazopewa tutakuja uana askari kwa akari.
Mimi siwezi kustahamili dhulma kama hii kwa ndugu zangu Waislam.''