Kweli tunapiga vita ugaidi au ni vita dhidi ya uislam?

Status
Not open for further replies.
Mkuu sisi hatumkatai Yesu na kwa taarifa yako muislamu yoyote anaye mpinga Yesu(USA) a.s huyo sio muislamu.

Tofauti inakuja kwenye kumtukuza(ghuluu) kwamba Yesu ni mungu/mwana wa mungu hapo ndio shida ipo.

Mkuu Mbona Hiyo sio shida!

Km unaamini yeye Yesu ndio atakae kuja hapo mwisho kwanini na hizo sifa zake usizikubali?

Bora tujadi ata haya mambo maana haya mambo ya ugaidi yanaumiza kichwa!

Naam! Unamuonaje Yesu Mkuu!?
 
Kama dini za waarabu hazikubaliani na ugaidi angalia matukio yakigaidi yote duniani yanafanywa na nani kama sio waarabu, pia ukiona kila siku dini yako ndio inapingwa kila kona ya dunia ujue inakasoro lazima, kingine tukio la westgate majuzi tu hapa magaidi walikua waislamu na ushahidi upo......angalia kinachoendelea syria leo, waarabu wanauana wao kwa wao wakiamini ukiua mtu unapata swawabu, Mungu gani anataka uue watu wasio na hatia alaf akupokee
mkuu huwaga unaisoma bibilia yako kweli ama umeiweka kama pambo?.
 
Kama dini za waarabu hazikubaliani na ugaidi angalia matukio yakigaidi yote duniani yanafanywa na nani kama sio waarabu, pia ukiona kila siku dini yako ndio inapingwa kila kona ya dunia ujue inakasoro lazima, kingine tukio la westgate majuzi tu hapa magaidi walikua waislamu na ushahidi upo......angalia kinachoendelea syria leo, waarabu wanauana wao kwa wao wakiamini ukiua mtu unapata swawabu, Mungu gani anataka uue watu wasio na hatia alaf akupokee

Mkuu mi nakujibu Jambo moja tu! Rudi tena ukaangalie chanzo Cha mgogoro Wa Syria ni nini!
 
Mwigulu muislamu? Nape ni muislamu? Sasa kama hapo tu umeweza kudanganya watu laivu nani unadhani atakuamini utakapo andika mambo tusio na uelewa nayo.

yanini kubishana toa data mkuu, Ni heri ukataja dini zao ili nijue kama wewe pia haudanganyi.
 
Wale jamaa walioingia westgate ulikuwa unawashabikia. Sasa unapohusianishwa na magaidi u just relax na uache dawa iingie
jana kule sudani ya kusini wamefukua kaburi la halaiki lenye maiti 75 watu wameuawa.kwanini kwa mawazo yako waliofanya mauaji haya hawajaitwa magaidi?.kumbuka huko wanapigana wakristo wao kwa wao.sasa unadhani nao wanaqualify kuitwa magaidi ama ukiuawa na mkiristo unakua umepata ubarikio.

Ama zile drone za kikristo zinaporipua watoto kule pakstani huo si ugaidi bali ni baraka.ugaidi ni mpaka ufanywe na mwislamu.
 
Nashindwa kuelewa sana,

Sijui tatizo ni nin,kwanin kila wasilam wanaposimama kuelezea madhila yanayofanywa na serikali watu wa iman zingine huja hapa kuwakashifu na kuuchagua upande na kuwapinga na kuwakejeli waislam??

Kwani nani kawaambia hii ni vita baina ya waislam na wale wasio kuwa waislam??tuacheni tunapoeleza yanayotuhusu tuyaelezeee

Ingekuwa ni madhila kati ya waislam na serikali hakika hamna mtu wa dini ingine angeingilia. Ninachokiona hapa ni lawama kuwa dini zingine ndo serikali kitu ambacho kwa kawaida tu na akili za kibinadam hakileti sense. Kwa nn isemwe kuna mfumo kristo na sio mfumo hindu? Kuweka kristo pale inasababisha watu wanaomwamin wamtetee na hapo ndo wewe unaona kuwa wanatetea serikal. Waislam piganien haki zenu toka kwa aliyenazo ambaye ni serikali wakristo wapotezeen watawaboaa tu.
 
Mkuu Mbona Hiyo sio shida!

Km unaamini yeye Yesu ndio atakae kuja hapo mwisho kwanini na hizo sifa zake usizikubali?

Bora tujadi ata haya mambo maana haya mambo ya ugaidi yanaumiza kichwa!

Naam! Unamuonaje Yesu Mkuu!?

Shida ipo kumpa mtu sifa sio yake ni kosa na ndio maana mwenyezimungu amesema mwenye kuamini mungu mwingine tofauti na yeye ni sawa sawa na nyumba ya buibui na nyumba ya buibui ni dhaifu kuliko nyumba zote duniani kwahiyo mkuu Ntuzu unapenda na wewe nikufananishe na nyumba ya buibui?
 
Miezi michache iliyopita vyombo vya habari vilisheheni taarifa ya magaidi waliokuwa katika vijiji vya Handeni.

Taarifa zilifika Tanga kuwa kulikuwa na magaidi wanaishi katika mahandaki na operesheni maalum ilikuwa ikifanyika kuwateketeza.

Propaganda ikaenezwa kuwa walikuwa hawaitambui serikali ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Habari zilivuja Tanga mjini na vitongiji vyake kuwa kuna vijiji vimeteketezwa.

Kwa hakika kuna watu waliletwa Hospitali ya Bombo wakiwa na majeraha ya risasi.

Kwa watu waliofika Hospitali ya Bombo kwa kweli waliwaona vijana waliokuwa wamefungwa pingu wakiwa katika vitanda vyao huku wakilindwa na askari.

Taarifa zikafika vilevile kuwa kuna watoto wadogo wamefikishwa Tanga baada ya kukutwa porini.

Watoto hawa walikuwa wamehifadhiwa katika moja ya shule za hapo mjini.

Katika hali kama hiyo vilevile zikafika taarifa tofauti kwa Waislam wa Tanga kuwa hao walioletwa Hosptali ya Bombo na watoto waliookotwa porini ni Waislam wa vijiji vya Madina, Dibungo na Lwande walioshambuliwa na askari pasi na sababu.

Juhudi za Umoja wa Taasisi za Kiislam Tanga (SHITA) chini ya Mayor Omari Guledi na Katibu wake Ahmed Mustafa kukutana na Mkuu wa Mkoa Chiku Galawa kupata ukweli zikagonga mwamba.

Hali ikawa tete baada ya Sheikh Rajab Ramadhani Chambuso mmoja katika masheikh vijana mjini Tanga kukamatwa na kuwekwa rumande kisha kuhamishwa Handeni ambako alifunguliwa kesi ya ''kushawishi mauaji.''

Ikavuma kuwa patakuwa na maandamano kushinikiza kuachiwa kwa Sheikh Chanmbuso.

Askari wa FFU walizingira misikiti kadhaa Ijumaa hiyo lakini hapakuwa na maadamano yoyote.

Alipopata dhamana na kuachiwa Sheikh Chambuso alikuja Tanga na habari za kutisha kuhusu dhulma iliyopita katika vijiji vya Madina, Dibungo na Lwande.

Habari hizi alielezwa na mahabusi wendake katika hivyo vijiji vilivyoshambuliwa.

Sheikh Chambuso katika hotba aliyotoa katika moja ya misikiti maarufu Tanga aliwafahamisha Waislam kuhusu misikiti iliyovujwa na kuchomwa moto, Qur'an zillizochoiwa moto na nyumba za Waislam zilizoteketezwa kwa kisingizo cha ugaidi.

Wananchi jioneeni wenyewe yote hayo katika hizi picha.

PS: Weka cursor kwenye picha click utapata na maelezo ya picha.
Tumesema hii mi vita dhidi ya uislam.sababu tumetoa sasa kama kuna mtu anaona hapana sio vita dhidi ya uislam badi aje na hoja kukanusha.
Wale wannaopenda malumbano ya kukashif uislam waende kwenye mada za aina hii
Hii mada ni muhimu tuijadili kama ilivo na ni muhimu kupata mawazo ya watu wote ili kuweka sawa suala hili. Kama ni kweli ugaidi ni kichaka cha kuwabamiza waislam then tuwambie wenye mamlaka hio sio kwa faida ya nchii hii.
Na kama hakuna uonevu pia waislam waondoe shaka. Na kama kuna watu ---------- nje au hata ndani ili kuwabughudhi waislam nao wasemwe wazi humu . Ninaamini kujadili hoja kistaatabu na kisomi ndio tunavojiinesha wa TZ tupo vipi tunapojadili mambo yanatugusa kama jamii. Hii jamii forum niwapongeze walio fikiria na kuusimamia mpaka kuanzishwa kwake. Ukweli kuna forym nyingi lakini hii ni ya kipekee na tuitumie vizuri kujadili hoja kistaarabu . Tukifanya hivyo itatusaidia kuondoa kila aina ya mabaya katika jamii yetu. Naamini hii forum imaweza hata kubadilisha maamuzi mabovu ya serrikali kama tutajadili issues with constructive ideas. Kama sisi watanzania waislam na wakristo tunaishi pamoja tuna cheza simba na yanga pamoja tupo jirani tupo makazini pamoja ambapo hakuna sehemu ya kazi ambayo kuna watu wa dini moja pekee yao basi yusikubali kugawanywa. Kama waislam wana malalamiko tuyajadili na kuyatafutia ufumbuzi.na pia hivo hivo kwa wakristo.tanzania ni yetu wote tusiruhusu ubinafsi ututuwale
Hii forum inafatiliwa na wanasiasa pamoja na hata Rais mwenyewe
Na rais mwenyewe nina hakika amekua hata akichukua baadhi ya hoja na mawazo ya watu humu jamii forum katika kuamua mambo yanayohusu watanzania. Nakumbuka kulikua na mada kuhusu jumuia ya afrika ya mashariki na nikasema kama nchi yanzania tunapaswa kwenda na kufata taratibu hakuna haja ya kukurupuka tu. Nikasema matatizo makubwa ya jumuia kama hizi ni mambo ya uchumi nikasema sisi tanzania tuna experience ya muungano wa kisiasa na kiuchumi na nikasema matatizo mengi ya muungano wetu mi masuala ya uchumi. Mkuu wa nchi aliyazungumza haya katika hotuba yake ya Bungeni alisema kama nilivo andika ndani ya jamii forum.
Hivo tujadili mada kistaarab na kwa mtindo wa yes hii ni vita dhidi ua uislam kwa sababu .... au hapana sio vita dhidi ya uislam kwa sababu .....
Turudi kwenye mada kuu tuisaidie nchi yetu
 
Ingekuwa ni madhila kati ya waislam na serikali hakika hamna mtu wa dini ingine angeingilia. Ninachokiona hapa ni lawama kuwa dini zingine ndo serikali kitu ambacho kwa kawaida tu na akili za kibinadam hakileti sense. Kwa nn isemwe kuna mfumo kristo na sio mfumo hindu? Kuweka kristo pale inasababisha watu wanaomwamin wamtetee na hapo ndo wewe unaona kuwa wanatetea serikal. Waislam piganien haki zenu toka kwa aliyenazo ambaye ni serikali wakristo wapotezeen watawaboaa tu.

controler hapa umenena, japo kuna jambo moja hujagusia, ukweli ni kuwa ushabiki hapa ambao kama inavyokuwa mpirani mchezaji wa timu yako anapocheza rafu na kulimwa kadi na refa, unabaki ukimtetea tu na kumlaumu refa kuwa anapendelea kwa lengo timu ishinde.
tatizo la ushabiki ni kukosa hoja za ku-link.
mimi sitagusia mapungufu haya mpaka bi chiku na mayor wa tanga watakapoonyesha msimamo wao kutofautiana na maamuzi ya massawe. its so obvious, hoja za wapinga kristo ni hafifu sana, kwani zimeelemea hali ya kutaka kubebwa na kiongozi anayenunuliwa kwa suti.
 
Shida ipo kumpa mtu sifa sio yake ni kosa na ndio maana mwenyezimungu amesema mwenye kuamini mungu mwingine tofauti na yeye ni sawa sawa na nyumba ya buibui na nyumba ya buibui ni dhaifu kuliko nyumba zote duniani kwahiyo mkuu Ntuzu unapenda na wewe nikufananishe na nyumba ya buibui?

Bilal bin Rabah unanifurahisha sn rafiki Yangu!

Shida iko Kwa Yesu tu!

Unajua hili Jambi si mahala pake na pia tutakwenda kinyume na mada ya Ms! Ila Nilipenda Tungeweza kujadili kidogo juu ya hili na nyie rafiki zangu! Ninaamini ipo siku tutajadili sn tu!

Alafu pia Leo ningependa niwe mdadisi ndani ya Quraan!

Nitakuuliza maswali Nawe pia ntakuomba unijibu vizuri!
 
usijali mkuu "be free"
 
Tumesema hii ni vita dhidi ya uislam.sababu zimetolewa sasa kama kuna mtu anaona hapana sio vita dhidi ya uislam badi aje na hoja kukanusha.
Wale wannaopenda malumbano ya kukashif uislam au ukristo waende kwenye mada za aina hio zipo humu ndani ya forum
Hii mada ni muhimu tuijadili kama ilivo na ni muhimu kupata mawazo ya watu wote ili kuweka sawa suala hili. Kama ni kweli ugaidi ni kichaka cha kuwabamiza waislam then tuwambie wenye mamlaka hio sio kwa faida ya nchii hii.
Na kama hakuna uonevu pia waislam waondoe shaka. Na kama kuna watu ---------- nje au hata ndani ili kuwabughudhi waislam nao wasemwe wazi humu . Ninaamini kujadili hoja kistaatabu na kisomi ndio tunavojiinesha wa TZ tupo vipi tunapojadili mambo yanayo tugusa kama jamii. Hii jamii forum niwapongeze walio fikiria na kuusimamia mpaka kuanzishwa kwakehakika Bravo..:thumbup: Ukweli kuna forym nyingi lakini hii ni ya kipekee na tuitumie vizuri kujadili hoja kistaarabu . Tukifanya hivyo itatusaidia kuondoa kila aina ya mabaya katika jamii yetu. Naamini hii forum imaweza hata kubadilisha maamuzi mabovu ya serrikali kama tutajadili issues with constructive ideas. Kama sisi watanzania waislam na wakristo tunaishi pamoja tuna cheza simba na yanga pamoja tupo jirani tupo makazini pamoja ambapo hakuna sehemu ya kazi ambayo kuna watu wa dini moja pekee yao basi yusikubali kugawanywa. Kama waislam wana malalamiko tuyajadili na kuyatafutia ufumbuzi.na pia hivo hivo kwa wakristo.tanzania ni yetu wote tusiruhusu ubinafsi ututuwale
Hii forum inafatiliwa na wanasiasa pamoja na hata Rais mwenyewe
Na rais mwenyewe nina hakika amekua hata akichukua baadhi ya hoja na mawazo ya watu humu jamii forum katika kuamua mambo yanayohusu watanzania. Nakumbuka kulikua na mada kuhusu jumuia ya afrika ya mashariki na nikasema kama nchi yanzania tunapaswa kwenda na kufata taratibu hakuna haja ya kukurupuka tu. Nikasema matatizo makubwa ya jumuia kama hizi ni mambo ya uchumi nikasema sisi tanzania tuna experience ya muungano wa kisiasa na kiuchumi na nikasema matatizo mengi ya muungano wetu mi masuala ya uchumi. Mkuu wa nchi aliyazungumza haya katika hotuba yake ya Bungeni alisema kama nilivo andika ndani ya jamii forum.
Hivo tujadili mada kistaarab na kwa mtindo wa yes hii ni vita dhidi ya uislam kwa sababu ....
au hapana sio vita dhidi ya uislam kwa sababu .....
Turudi kwenye mada kuu tuisaidie nchi yetu
 
Mkuu, ndani ya Quraan kuna Aya inayofundisha kupambana mpk kuhakikisha fitna inakwisha?
Au kuna Aya inayofundisha kutetea haki yako ata Kwa nguvu?
Naomba majibu yko Mkuu!

Hapo sijakuelewa vizuri unazungumzia JIHAD au kupambana kivipi na kama ni JIHAD ina masharti yake mpaka yatimie.

Usije ukaona vitendo vinafanya na vikundi vinavyojinasibisha na uislamu ukadhani ndio Quran imesema hivyo.

Unajua mtu anaweza akaitumia aya kuwaeleza waumini tofauti na maana halisi halafu waumini wakapata mhemko tofauti kabisa na maana sahihi kama aya zinazohusu JIHAD.
 
Ahsante Master Crabat turudi kwenye mada kuu
Please tujadili mada na sio dini ....naunga mkono tuache malumbano ya udini
 
Hapo sijakuelewa vizuri unazungumzia JIHAD au kupambana kivipi na kama ni JIHAD ina masharti yake mpaka yatimie.

Usije ukaona vitendo vinafanya na vikundi vinavyojinasibisha na uislamu ukadhani ndio Quran imesema hivyo.

Unajua mtu anaweza akaitumia aya kuwaeleza waumini tofauti na maana halisi halafu waumini wakapata mhemko tofauti kabisa na maana sahihi kama aya zinazohusu JIHAD.

Thx Mkuu!
Ok Kwa Mfano Jihadi, kuna Aya ambazo zinatoa mafundisho km nilivyouliza? Na pia umeniongezea kitu ambacho nilikua sikifahamu! Ni mashariti gani hayo Mkuu mpk yatimie juu ya Jihadi?

Usinione msumbufu Mkuu Kwa maswali yng! Iwapo km utakua si mchoyo Wa elimu Itafikia hatua mtu kupitia maoni yako akaweza kuutoa uislam dhidi ya tuhuma km Hizi!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom