Kweli Vyama vya Upinzani wamelamba asali

Chakwale

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2015
Posts
1,080
Reaction score
1,585
Nilikuwa siamini Ile kauli ya Vyama vya Upinzani kulambishwa Asali Ili wakae Kimya, lakini kwa namna mambo yanavyoenda naamini kabisa kuwa Wamelamba.

Haiwezekani Umeme ukatike hovyo hovyo bila sababu za msingi,yaani wanakata kata tu wanavyojisikia.Mwanzoni walikuwa wanasema Maji yamepungua kwenye mabwawa lakini Mwenyezi Mungu anawaumbua Mvua inanyesha hadi mafuriko lakini Bado umeme ni tatizo.

Sasa hivi Wafanyabiashara wa vyombo vya Usafiri wameamua kupandisha bei ya nauli watakavyo,watu wako Kimya tu Ili hali bei ya mafuta kwenye Soko la dunia bado Iko pale pale.

Sasa najiuliza Hivi Vyama vya Upinzani KAZI yao hasa ni IPI? Kama kwenye mambo nyeti kama haya yanayogusa maisha ya mtanzania wa chini kabisa hadi wa juu wako Kimya bila kuwasemea chochote wao Wana umuhimu Gani kwenye hii Nchi?

Ni bora Upinzani ufutwe tu usiwepo tujue Moja kuwa tunapambana n'a mkoloni Mmoja CCM tujue tutamalizana nae VP kuliko kuwapa Ruzuku za bure ilihali hawana wafanyacho.

Yaan Walambe Asali,halafu tena wapewe Ruzuku wanatafuna hukuhuku bila sababu yeyote île Uwajibikaji wao una madhaifu makubwa.

Baada ya Ongezeko hili la Nauli tutarajie mfumuko mkubwa wa bei kwenye Bidhaa mbalimbali Pia kwenye Vyakula mbalimbali sababu ya hili Ongezeko la Nauli.

Yaani pamoja n'a kwamba Maisha magumu lakini Bado Mwananchi wa kawaida anatafutia Njia za kuendelea kumnyonga badala ya kumsadia kujinasua Ktk ukali wa Maisha unaomkabili.Viongozi wetu wameamua kuwa wanyonyaji kama mdudu kupe kwa raia wanao waongoza bila kujali udhaifu wa afya Zao.

Enewei Acha niishie hapa.
 
Nilikuwa siamini Ile kauli ya Vyama vya Upinzani kulambishwa Asali Ili wakae Kimya,lakini kwa namna mambo yanavyoenda naamini kabisa kuwa Wamelamba...
Tanzania hakuna wapinzani wa kweli kilichopo ni biashara ya kisiasa, unapiga kelele ukirushiwa paja unatulia zako.
 
We boya wewe yanapoguswa maisha yao kwa risasi, kutekwa na jela hua unawasaidia nn??
Kama Mawazo Yao yamefika kikomo na hawana Msaada tena,ndio maana nikasema bora wasiwepo wabaki CCM pekee tujue hakuna wapinzani kuliko kujifariji wapo Ili hali ni wafu
 
Wapinzani wataongelea mambo yenye maslahi yao tu. Tume huru ya uchaguzi na katiba mpya nk. Hawako kwa ajili ya kuongelea maslahi ya wananchi au ya nchi.
 
Uwepo wao wewe unakuuma nn??
Badala ya kuwabana uliyowapa madaraka unahangaika na uliowakataa kama si kurukwa na akili ni nn??
 
Kwani saizi tunafanya kazi gani ? Au nani kasema maisha yetu na kula yetu inategemea uwepo wa upinzani huu dhaifu uliojaa wasaka tonge na wenye uchu wa madaraka?
Kwakweli naungana na WW kwenye hili,Wapinzani wamekuwa DHAIFU SANA kiasi Cha kuwa na shaka ya Kulambishwa Asali Ili wakae Kimya.

Ukimya wao ni kama CCM inafanya KAZI nzuri sana na inatekeleza Na kutatua changamoto za maisha ya watanzania kwa asilimia mia moja.Kumbe ni kinyume chake.

Watanzania wamechoka,wananyonywa kiasi kwamba hâta kupiga kelele hawawezi tena.Lakini Hawa wapinzani tuliowapa dhamana ya kutusaidia kutupigia kelele wameamua kuungana na Wanyonyaji wetu Ili kutuua Zaidi.
 
Wapinzani wataongelea mambo yenye maslahi yao tu. Tume huru ya uchaguzi na katiba mpya nk. Hawako kwa ajili ya kuongelea maslahi ya wananchi au ya nchi.
Maslahi yao hao wapinzani yako kwa WanaNchi,kufikiri kutetea maslahi yao pekee bila wanaNchi huo ni ufinyu wa Fikra.
Kutetea Maslahi Yao pekee bila kuwasemea wanaNchi kupoteza nguvu Zao bure tu..mana nguvu Yao na maslahi yao vyote viko kwa WanaNchi.So kujitenga na wanaNchi ni kujitenga wao wenyewe.
 
Nilikuwa siamini Ile kauli ya Vyama vya Upinzani kulambishwa Asali Ili wakae Kimya, lakini kwa namna mambo yanavyoenda naamini kabisa kuwa Wamelamba.

Haiwezekani Umeme ukatike hovyo hovyo bila sababu za msingi,yaani wanakata kata tu wanavyojisikia.Mwanzoni walikuwa wanasema Maji yamepungua kwenye mabwawa lakini Mwenyezi Mungu anawaumbua Mvua inanyesha hadi mafuriko lakini Bado umeme ni tatizo.

Sasa hivi Wafanyabiashara wa vyombo vya Usafiri wameamua kupandisha bei ya nauli watakavyo,watu wako Kimya tu Ili hali bei ya mafuta kwenye Soko la dunia bado Iko pale pale.

Sasa najiuliza Hivi Vyama vya Upinzani KAZI yao hasa ni IPI? Kama kwenye mambo nyeti kama haya yanayogusa maisha ya mtanzania wa chini kabisa hadi wa juu wako Kimya bila kuwasemea chochote wao Wana umuhimu Gani kwenye hii Nchi?

Ni bora Upinzani ufutwe tu usiwepo tujue Moja kuwa tunapambana n'a mkoloni Mmoja CCM tujue tutamalizana nae VP kuliko kuwapa Ruzuku za bure ilihali hawana wafanyacho.

Yaan Walambe Asali,halafu tena wapewe Ruzuku wanatafuna hukuhuku bila sababu yeyote île Uwajibikaji wao una madhaifu makubwa.

Baada ya Ongezeko hili la Nauli tutarajie mfumuko mkubwa wa bei kwenye Bidhaa mbalimbali Pia kwenye Vyakula mbalimbali sababu ya hili Ongezeko la Nauli.

Yaani pamoja n'a kwamba Maisha magumu lakini Bado Mwananchi wa kawaida anatafutia Njia za kuendelea kumnyonga badala ya kumsadia kujinasua Ktk ukali wa Maisha unaomkabili.Viongozi wetu wameamua kuwa wanyonyaji kama mdudu kupe kwa raia wanao waongoza bila kujali udhaifu wa afya Zao.

Enewei Acha niishie hapa.
😂😂 anza wewe kwanza kuwa front line
 
Shida ni kuwa wananchi wa taifa hili ni wapumbavu.Vyama vya upinzani wakisema mnadai wanafanya siasa za matukio.Wakikaa kimya wamalamba asali yaani hatujui tunataka nini.
 
Back
Top Bottom