Kwenda chuo kuna faida ambazo form 6 hawezi kuja kuzipata, Nasisitiza kama uwezo upo nendeni chuoni, form 6 nenda ikishindikana kwenda chuo

Uzi wa kipumbavu utakaofurahiwa na wanaopenda shortcut. Aliyemaliza form six anapata admission kokote duniani endapo kafaulu vizuri. Huu upuuzi wa kupenda shortcut hauwezi kutupeleka popote. Watoto wenye akili hupita form 6 then chuo. Na sio lazima watu wasome ili waajiriwe serikalini. Wengine watajiajiri. Mtu anayeibeza form 6 ni mtu mvivu aliyekata tamaa ya maisha.
 
Acha kujidanganya. Mwanafunzi wa diploma mara nyingi hakuwa na matokeo mazuri kama walioenda form 6. Hata wakikutana chuo yule wa form 6 atamburuza wa diploma. Sijawahi kuona best student chuo aliyetokea diploma.
 
Huu ujinga watanzania wanaojazana ni kama miaka ile ya 2014 walipojazana ujinga kuhusu kilimo cha matikiti na wote wakaenda kulima matikiti. Shortcut is always a wrong cut.
 
Imekaa njema
wanaobeza wengi ni form 6 walio vyuoni kwa sasa ama ni fresh graduates, na mimi nilikuwa kama wao, ilikuwa inaniuma kukiri kwamba waliosoma form 4>>chuo wana advantage kuliko sisi tuliopiga six, nilikuwa najipa moyo kwamba njia wanazopita ni kuunga unga, n.k.

Muda ulivyosonga na kichwa kutulia nikapata picha safi kwamba kujua kitu ni uongo na ukakiamini ni ujinga, nikaweka ujinga pembeni na kukiri kwamba form 4>>chuo ni mtiririko mzuri zaidi kitaaluma, nimeandika hii post iwe faida kwa wadogo zetu na wazazi / walezi wao, hata mimi nawashauri sana ndugu zangu waende chuoni, watoto pia ningependa waanze kusomea taaluma zao mapema wakimaliz form 4.
 
Wewe una stress za maisha. Take it easy kwasababu kila mtu ana changamoto zake. Wewe unataka watu wapite njia yako ya shortcut wakati wengi wanawaza zaidi ya hapo. Kimsingi unataka watu wapate hizo diploma then ajira sehemu ambayo nyingi huwa ni za kukusaidia tu usife. Acha vijana wapite six ili waende kwenye malengo makubwa zaidi na sio kuishia kuwa fundi mchundo.
 
Acha kujidanganya. Mwanafunzi wa diploma mara nyingi hakuwa na matokeo mazuri kama walioenda form 6. Hata wakikutana chuo yule wa form 6 atamburuza wa diploma. Sijawahi kuona best student chuo aliyetokea diploma.
Umeongea ukweli ambao hawatataka kuusikia. Form6 ni ishara ya mwanafunzi anayejiweza kielimu.
 
hayo yote umeongea lkn Bahat inasimama pale pale nina mifano mingi hai , so ajira ni Bahat tu siku iz no matter what
 
Meuelewe aliyekwambia form six inamfanya kijana kuwa maturity kitaluma na kiakili na ndio maana baadhi ya taaluma hapa Tz hauwezi kupata degree yake kama hajasoma form five na six, sababu wanajua wanaitaji content siyo vyeti mfano degree ya uwalimu kwa bongo huwezi kuwa na degree ya uwalimu ujasoma form five na six hilo unalijua

Hata wale wanafunzi wanachukuliwa kutoka kidato cha nne kwenda kusomea diploma ya uwalimu siunajua uko chuoni pamoja na kusoma kozi ya uwalimu ila wanachagua combination na wanaanza kupiga topic za form five na six na paper ya form six ya necta wanafanya kabisa

Kingine mnatakiwa mjue siyo eti mtu aliyesoma certificate kisha diploma ni mzuri zaidi ya yule anayeanza first year degree fresh from from six hapana, kumbuka certificate na diploma unaanza somea taaluma uyu wa form six alipotoka alikuwa asomei taluma alikuwa anachukua msingi wa taaaluma kwaiyo akija darasani wewe wa certificate na diploma utamsumbua mwaka wa kwanza tu baada ya hapo humwambii kitu sababu yupo mature enough kuelewa vitu na anajua anachokifanya

Kingine nyie mnaoenda certificate sijui diploma mnaanza bado na akili za kitoto mnawaza bata na mademu na mabwana so wengi wenu huwa si wazuri mengi mnayojifunza hamzingatii

Ushauri wangu kwa vijana kama una sifa za kwenda form five na six nenda usikimbilie jitesa maana maisha ya chuo bwana kama fedha huna nikujitesa tu na kumbuka elimu ya certificate na diploma dunia ya sasa imebaki na deal kwenye mifugo, kilimo, afya na ufundi, na IT basi uko kwengine unapoteza muda wako tu nani anaitaji mhasibu wenye certificate ili iweje so ukianza certificate basi tambua unauwezo wa kwenda diploma to degree yanin sasa usome miaka sita wakati unaweza kusoma miaka mitano,

Maika miwili form five na six miaka mitatu chuo kikuu uku unakula boom lako safi
 
Uzi ufungwe. Umemaliza kila kitu. Pia mtu mwenye ndoto kubwa za siku moja kusoma vyuo vikubwa vya nje na hata kufanya kazi huko hawezi kuacha kupita form six. Kijana aliyemaliza form six anaweza kujiunga chuo kikuu USA ila kijana wa diploma ni ngumu kueleweka.
 
Acha kuongea maneno matupu

MATURITY ? form 6 bado inam treat mwanafunzi kama mtoto wa form 1, anatandikwa viboko kama mtoto watoto wa form 1, anapewa adhabu kisa hajavaa tai kama form 1, haruhusiwi hata kumiliki laptop wala simu kama form 1, hio maturity iko wapi ?

KITAALUMA ? Form 6 Inamjenga vipi kitaaluma mwanafunzi wakati hatambuliki kwa taaluma yoyote akihitimu ?

Hao ni kama wameenda kusomea form 5 na 6, ndio maana nimeandika kwenye post wale wanaotaka kuwa waalimu ni vema wapitie form 5 na 6

Kingine nyie mnaoenda certificate sijui diploma mnaanza bado na akili za kitoto mnawaza bata na mademu na mabwana so wengi wenu huwa si wazuri mengi mnayojifunza hamzingatii
Ndio ugeni wa uhuru wa chuoni huo, form 4>>chuo na form 6>>chuo huwa wanafanana kwenye ugeni wa chuo, lakini form 4>>chuo ana advantage anautolea ushamba akiwa certificate, wenzake wa form 6 wanautolea wakiwa degree.
Hujui unachoongea, Hao wahasibu kenrye vyeo vya assistant accountants wanahitaji wenye diploma, kazi kibao za assistant kwa taaluma nyingi zinahitaji diploma,

Hili ni tangazo la ajira TANROADS cheo cha assistant accountant wanahitaji mwenye diploma au vertifivate


Maika miwili form five na six miaka mitatu chuo kikuu uku unakula boom lako safi
Hata diploma wanapata mikopo, nina ndugu zangu wapo vyuoni wamepitia dip, wazazi wao hawahangaiki
 
Kwanini umeifungia akili yako yote kwenye kuajiriwa tena hata sio nchi za nje yaani hapahapa Tanzania? Yaani wewe unawaza maisha mazuri yapatikana kwenye kuajiriwa kwa kutumia hizo diploma. Inaonekana huna exposure kabisa.
 
Kwanini umeifungia akili yako yote kwenye kuajiriwa tena hata sio nchi za nje yaani hapahapa Tanzania? Yaani wewe unawaza maisha mazuri yapatikana kwenye kuajiriwa kwa kutumia hizo diploma. Inaonekana huna exposure kabisa.
Ni kwasababu uhalisia wa hali ya mfumo wa elimu ya nchi yetu inaandaa zaidi wanafunzi kuajiriwa na hilo wala halina kupepesa macho, System ya elimu inabidi ibadilishwe ili kujengea vijana mindset ya kutamani kujiajiri zaidi na mazingira wezeshi yawepo mfano mikopo kwajili ya mitaji yenye riba ndogo kwa wahitimu, Kuandaa utaratibu wa kuwapleka wahiitimu wapate uzoefu kwa waliojiajiri, misamaha ya kodi kwa wahitimu wanaojiajiri kwa miaka miwili ya mwanzo, n.k.
 
Form six ni mihimu kujenga maturity na reasoning capacity ya mtoto, sio kila mtu anasoma kuajiriwa, vyuo vibaki kwa watoto kutako kaya masikini
Umejibu vizuri, kutana na mtu alifeli sa saba alafu nenda kwa mmoja alifeli form four na zero..hao ni watu wawili tofauti, kwenye mitizamo mingi..shule ina vingi zaidi ya ajira
 
Umejibu vizuri, kutana na mtu alifeli sa saba alafu nenda kwa mmoja alifeli form four na zero..hao ni watu wawili tofauti, kwenye mitizamo mingi..shule ina vingi zaidi ya ajira
Ni wanafunzi wengi tu wenye division 1 wanachaguliwa kwenda kusoma vyuoni, sijajua unatumia kigezo kipi, waweza kuangalia selection zilizotoka juzi, wanafunzi ni wengi tu wliofaulu vizuri wamechaguliwa vyuoni.

Mfano hawa ni wahitimu wa form 4 Ilboru Secondary wamechaguliwa vyuoni, wana division 1 zao safi tu.

 
Acha kueneza stress kwa vijana.
 
Hili ndio tatizo lenu wanafunzi ujuaji juaji mwingi at the end mnashia kubet
 
Hili ndio tatizo lenu wanafunzi ujuaji juaji mwingi at the end mnashia kubet
hoja yako ni hewa, Jibu kama msomi ambaye ni matured mwenye reasoning capacity

Mimi nimeweka hoja kwa facts, na wewe jibu facts iwe ni kwa kukosoa, ku approve, nyongeza, n.k
 
Kuna baadhi ya hoja zako nakuunga mkono ila naku-challenge kwakushindwa kwako kueleza negatives/mapungufu ya kupitia form 4- chuo cha kati.
Changamoto mojawapo ya kupita form 4-chuo ni kwamba anabanwa kwenye nafasi za kwenda kusoma shahada(degree) kwakuwa wanapewa nafasi chache na pia wanataka GPA ya kuanzia 3.0 au zaidi, kitu ambacho kinafanya diploma holders wengi hasa wa afya na engineering washindwe kusoma degree.
Zipo pia changamoto zingine ulipaswa kutuambia kuliko kuegemea upande mmoja wa positives/faida tu.
 
Kubanwa kwenda chuo inategemeana na chuo unachoomba, vyuo vinavyogombaniwa kama Udsm, Mzumbe, DIT, Muhimbili, n.k. ni ngumu sana kupenya hata kwa wahitimu wa form 6 ambao ni wengi zaidi ya mara 10 kuzidi wahitimu wa diploma, Tena siku hizi division 1 na 2 zilivyo nyingi form 6 ishakuwa kawaida kusikia wanakosa nafasi inabidi wasome vyuo private, lakini bado hata Diploma wapo wengi tu wanaodahiliwa degree, advantage ni kwamba ukisomea diploma chuo flani inakuwa rahisi zaidi kudahiliwa degree ila ukitaka kubadili chuo hasa vinavyogombaniwa ni shida,

GPA ya 3.0 ndio mchujo wa kusonga mbele, Wanaoshindwa kuifikisha wapo ila sio kiasi cha kushangaza, ikizidi sana kwa wastani ni almost wanafunzi wawili katika kila wanafunzi kumi (20 %). kwenye darasa la watu mia, 80 wanapita, wapo wataoishia diploma kushindwa kusonga mbele kama ilivyo kwa form 4, form 6, n.k.

Changamoto zipo kila sehemu, ni suala la kuziweka kwenye mzani kupima if its worth it.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…