Special cases mtu aende form 6
Bado ni mdogo sana kiumri
Hakuna uwezo wa kumlipia ada
Kutaka kuwa mwalimu,
Background yangu, Nilimaliza form 6 miaka ya 2009 nikapiga division 2 ya 10, baada ya kufaulu ikabidi nianze kufatilia chuo, Ni kipindi ambacho wanafunzi wengi sana wanachanganyikiwa wasomee kipi, mimi binafsin nilichagua kusomea nachokipenda lakini nilipofika chuoni uhalisia ulikuwa tofauti sana na nilivyodhani, niligundua nimekurupuka kuchagua kozi, Nachoshukuru nyumbani vijihela vipo, ilibidi nibadili chuo kusoma kozi nyingine upya.
Kwenda chuo kuna faida zifuatazo
UWANJA MPANA WA KUPATA AJIRA - form 4>>chuo wana uwanja wa ajira mkubwa, wao wanaweza kuomba kazi za certificate, diploma na degree lakini wale wa form 6>>chuo wanaomba kazi za degree na huwa wanakuwa wengi sana kwenye maombi sababu form 6 ni wengi sana na pia wale wa form 4>>chuo wanajumuika, mfano unakuta nafasi 10 kazi ya diploma zinatangazwa wanaomba 500, lakini kwenye kazi za degree ni kawaida kukuta nafasi 10 wanaoomba watu elf 10. Hivyo form 4>>chuo anaweza kukosa ajira ya degree pamoja na mwenzake wa form 6>>chuo lakini labda akabahatika kupata kazi ya diploma au certificate ambayo form 6>>chuo hawezi kuipata, Ni kweli kazi za diploma zina mishahara midogo waweza kuta degree analipwa take home laki 8, diploma laki 5, lakini ni heri upate kitu kuliko kukosa kabisa.
KUPATA KAZI KABLA YA DEGREE - Inaweza kutokea mzazi kafariki ama kuna matatizo mengine ya kiuchumi yametokea mtu akashindwa kwenda degree, Ni kwamba form 6 bila degree hana taaluma hawezi kuajiriwa lakini mwenzake aliyeanza chuo baada ya form 4 anaweza kuajiriwa, Vyuoni kuna vijana wanasoma degree hawategemei mkopo wala wazazi wao, tayari wameajiriwa kwa diploma wanajisomesha kwa mishahara yao, wao wanaongeza elimu kupanda madaraja.
ADVANTAGE YA CV - Kitu kingine ni kwamba form 4>>chuo wana cv inayovutia kiuzoefu kuzidi form 6>>chuo, ni kwamba form 4>>chuo wamesomea taaluma kwa muda mrefu zaidi darasani kuzi form 6>>chuo, wana vyeti vya kitaaluma vingi (certificate + diploma + degree) kuzidi form 6>>chuo mwenye degree pekee, na cv inaonyesha wamefanya kazi kwa vitendo maofisini (field work) mara nyingi zaidi kuliko form 6>>chuo.
URAHISI WA KUBADILI KOZI - Mtu kamaliza form 4 ana ndoto za kusomea kitu anachopenda mfano marketing, anaingia chuoni certificate mwaka moja anakuja kugudndua ni kozi anayoipenda lakini haina soko kwenye ajira, Diploma ya miaka miwili anabadili kozi kusomea labda accounting hasa ukizingatia masomo mengi walishasoma pamoja darasa moja akiwa certificate hivyo sio mgeni sana, Degree anaweza kubadilisha kozi kusomea nyingine mfano Accounting and IT ili kuongeza zaidi uwanja wa ajira za IT, Sasa tukija kwa hawa form 6>>chuo unakuta mtu anapenda kusomea insurance, anafika chuoni anakuja kugundua kitu anachokipenda kupata ajira zake ni ngumu, kubadili gia angani sio rahisi, yanabaki kuwa majuto.
KUYAZOEA MAISHA YA CHUO MAPEMA - form 4>>chuo na form 6>>chuo wote kwa pamoja wakiwa mwaka wa kwanza chuoni huwa wanapata changamoto ya uhuru wa maisha ya chuoni, style ya kusoma chuoni, kuandaa assignments, presentations, n.k. hii huwa inachangia wengi kufanya vibaya kwenye masomo mwaka wa kwanza. form 4>>chuo na form 6>>chuo wakiingia degee si ajabu kukuta Form 6 > chuo wapo wanaofaulu sana lakini muda huo huo wanaofeli zaidi na hata kudisco (kufukuzwa chuonu) ni hao hao wa Form 4.
KUYAZOEA MASOMO KWA KUYARUDIA - Na ndio sababu kubwa baadhi ya kozi za degree za miaka minne form 4>>chuo wataambiwa wasome miaka mitatu lakini form 6>>chuo watasoma minne, Ni kwamba chuoni huwa kuna kurudia rudia masomo kwenye ngazi tofauti sababu wanasomea taaluma sio vidato, kwa upande wa form 6>>chuo unakuta kasoma mambo mengi akiwa sekondari ambayo akifika chuoni hatayakuta sababu ni nje ya taaluma, atavikuta vitu vingi zaidi vipya vilivyojikita kwenye taaluma. Mfano unamkuta form 6 kasoma topics kibao za hesabu lakini wakifika chuoni wanarudia topics tatu tu na kukuta topics mpya nyingi zaidi, Muda huo form 4>>chuo kwao vitu vingi ni marudio walishavisoma sababu ni muhimu kuvijua katika taaluma, Lakini hii haimaanishi kwamba form 4>>chuo ndio wana uhakika wa kufaulu zaidi, LA HASHA !! kuna form 6 wanawakimbiza vizuri kabisa form 4>>chuo waliobweteka ama wasio na bidii.
UHURU WA KIUTU UZIMA - miaka 18+ tayari ni mtu mzima kisheria, Inashangaza kuona watu hawa wapo form 6 wana age 18+ wanatandikwa viboko, wanapangiwa mavazi, hawaruhusiwi simu, hawaruhusiwi kufuga ndevu, kusuka, n.k. ni kama watoto wadogo !! Chuoni ni tofauti uankuwa treated kama mtu mzima kisheria, hutakuja shikiwa bakora. Kuna wazazi husema wasipeleke watoto chuoni baada ya form 4 kwa kuogopa uhuru, Ukweli ni kwamba wakimaliza form 6 wataenda chuo na uhuru wataukuta, Ni suala la kuweza kuwajengea misingi watoto wajue namna ya kuishi hata wakiwa huru, hawa wanaobanwa sana ni kwaida sana wakifikaga chuoni lazima uhuru uwachanganye iwe ni form 4 ama form 6.
kwa ufupi
- form 4>>chuo kasomea miaka mingi zaidi taaluma kuzidi form 6>>chuo
- form 4>>chuo kafanya mazoezi ya kazi kwa vitendo mara nyingi zaidi kuzidi form 6>>chuo
- form 4>>chuo ana vyeti vingi vya taaluma (certificate+diploma+degree)
- form 4>>chuo badhi ya vyuo akiingia degree anasomea miaka mitatu tu, yule wa form 6>>chuo ni mgeni sana inabidi asomee miaka minne
- form 4>>chuo anatambulika kitaaluma akihitimu diploma, cheti cha form 6 hakitambuliki kwa taaluma yoyote
- ikitokea mzazi kaishiwa pesa, hakuna mkopo wa chuo, n.k. kwenda kusoma degree, form 4>>chuo anaweza kuajiriwa bila degree, form 6 hawezi kuajiriwa hata kama ana division 1.