Kwenda kwa mumeo na vitu vyote au kwenda na begi?

mwaka jana tulimfanyia KP wifi yangu. mchumba hakuwa na hela sana, huku kwetu kulikuwa na uafadhali. tukiwa tunajadili cha kumpa binti kwa kp na sendoff nikashauri wakwe kuwa huu sio wakati wa kujionyesha, hebu tumpe binti muda wa kwenda kukaa na mwenzie wajue wanataka nini.
Orodha waliyotupa karibu yooote ilikuwa vitu vya jikoni, huyo kaka alikuwa kapanga tu vyumba 2, na walikuwa na vitanda vyao 2 etc, wakaona vinawatosha kwa kuanzia maisha. wakaomba kama kutakuwa na hela ya ziada, kuliko kuwanunulia vitu ambavyo kwa sasa vitakaa tu bora tuwape hizo hela ziwasaidie.
badala ya kwenda china kufunga kontena la vitu ambavyo hawana hata nyumba ya kuviweka, tuliwapa zawadi ya 25M. Imewasaidia kuongezea, nasasa karibia watahamia nyumbani kwao na hayo masofa watanunua wakiwa na pa kuyaweka
like like...waambie bwana..mambo mengine sio kabisa
 
Huyo ni binti au sugar mummy?

Hilo ndo tatizo la kuolewa aged. Hata ndoa za hivyo hazidumu...sitaki kutaja majina ntapewa za uso.

Raha ya ndoa either muanza hamna kitu (muanze pamoja) au mume awe nazo. Mwanamke ata kikimchanganyia iwe ndani ya ndoa si kabla.
kweli kabisa sijui vitv na viredio vya huyo mume vitatupwa wapi maskini
 
mwaka jana tulimfanyia KP wifi yangu. mchumba hakuwa na hela sana, huku kwetu kulikuwa na uafadhali. tukiwa tunajadili cha kumpa binti kwa kp na sendoff nikashauri wakwe kuwa huu sio wakati wa kujionyesha, hebu tumpe binti muda wa kwenda kukaa na mwenzie wajue wanataka nini.
Orodha waliyotupa karibu yooote ilikuwa vitu vya jikoni, huyo kaka alikuwa kapanga tu vyumba 2, na walikuwa na vitanda vyao 2 etc, wakaona vinawatosha kwa kuanzia maisha. wakaomba kama kutakuwa na hela ya ziada, kuliko kuwanunulia vitu ambavyo kwa sasa vitakaa tu bora tuwape hizo hela ziwasaidie.
badala ya kwenda china kufunga kontena la vitu ambavyo hawana hata nyumba ya kuviweka, tuliwapa zawadi ya 25M. Imewasaidia kuongezea, nasasa karibia watahamia nyumbani kwao na hayo masofa watanunua wakiwa na pa kuyaweka

Mlifanya sahihi sana
 
Na msisahau
haya maharusi wenye sauti sio wale wahusika
kunakamati,mjomba,,mama aliechangia harusi za wenzie
na kadhalika na mashindano na kurushana roho

jiulize umealikwa harusi ya Smile na Mr ROCKY mfano
halafu ndani ya harusi kuna kumtunza mama yake smile kwa mabulungutu ya pesa
as if watu tumekuja kuona 'show za kutunzana pesa'

sasa kuna influence nyiingi mno
mimi nina aunty ambae keshachangia harusi zaidi ya 100
unaweza pata picha harusi ya mwanae atakavyolipiza mbwembwe na jinsi mwanae atakavyokosa sauti
hata kama mwanae atataka harusi ndoogo tu isiyo na mbwembwe..
Nakuambia, shida tupu. lakini hii yote ya kutokuwa na say na harusi yako inatokana na kuchangia hizi harusi. unafikiri kama nchi za wenzetu ambako hakuna kuchangia harusi nani atakulazimisha ufanye kufuru?
 
Mimi nina dada yangu mtoto wa shangazi...aliolewa mkubwa though sina hakika na umri kamili...ila tulishajua hawezi tena kuolewa.

Sasa huyu dada alikuwa ni milionea mdogo; ana nyumba kadhaa mpaka ma guest house. Afu mtu eti kaingia King.

Kwani walidumu? Huyo jamaa si kuwa alikuwa masikini sana ila alikuwa kwanza mdogo ki umri; pili ana ka umarioo ela zake zote kwenye pombe anajua wife anazo...na nadhani alikuwa hajatulia vile vile...kwa ufupi kila mtu alikuwa anamuona amefuata maslahi. Walitengana baada ya sijuhi miaka kumi ...ya uvumilivu uliotukuka kwa upande wa sister...lakini alibwanga manyanga...ameambulia watoto.

Tatizo laweza kuwa pande yeyote kwa mke kuleta dharau au mume kuwa mume maslahi from day one...a.k.a. tapeli alofuata ela na si penzi. Kwa sababu most of these rich girls ni wakubwa ki umri..ukitoa hao wa utajiri wa baba.

Kukujibu kama wanaoolewa aged ndoa zinadumu au hazidumu...jibu langu mimi kama NK ni kuwa uwezekano wa kudumu ni mdogo kama mume ni mdogo ila ni mkubwa akiolewa na mzee mwenzie...mostly mjane wa kiume au dovorcee.

Usilete mifano ya US sijuhi Mariah Kelly sijuhi nini naongelea utamaduni wa kiafrika ambao age is still everything.

Sugar mami inaanzia ngapi???

Je ni wote wanaoolewa aged ndoa zao hazidumu???

Na raha ya ndoa, imelala kwenye nani kachangia nini katika mali??
 
Not always mzazi atakupa kilicho haramu
Hakuna wazazi wenye pesa halali za kuwapa watoto wao??

Reginald Mengi je?? Asimpe mtoto wake wa kike nyumba kisa mmewe atajisikia vibaya??
Kikubwa ni kuwafunza watoto kuamini katika kazi.

Thread ime evolve
Hapa tunazungumzia zaidi role ya kumfanyia kila kitu
ndo maana nikasema unaweza kumpa pesa afanye mwenyewe
mfano kama ni furniture basi mpe pesa atafuute wee mwenyewe kuliko umnunulie
tena zenye taste ya kwako umleteee
get it?
The Boss naomba unifahamishe ama uniweke vizuri, kwani kuna tofauti gani kati ya mama akininunulia nyumba au akanipa hela ninunue nyumba???!!! Maana kama ni swala la taste basi hata wakati wa kwenda kununua anaweza kunichukua nikachague ninayoitaka mimi.
Nisichoelewa hapa ni kwamba Smile anasema wakipewa hela wakanunue hata kama ni vitanda vyao haina shida lakini wasipewe vitanda(kwa kuwa mwanaume atakua analalia kitanda kilichonunuliwa na mama mkwe)lakini si bado hela iliyotumika kununulia kitanda hata kama wameenda mume na mke si katoa mama mkwe???!!!!!!!!!! Nahitaji kufafanuliwa hapa.
 
Last edited by a moderator:
Badili tabia nimekupenda real constructive comment wish mgekuwa wengi kwenye community.
 
The Boss naomba unifahamishe ama uniweke vizuri, kwani kuna tofauti gani kati ya mama akininunulia nyumba au akanipa hela ninunue nyumba???!!! Maana kama ni swala la taste basi hata wakati wa kwenda kununua anaweza kunichukua nikachague ninayoitaka mimi.
Nisichoelewa hapa ni kwamba Smile anasema wakipewa hela wakanunue hata kama ni vitanda vyao haina shida lakini wasipewe vitanda(kwa kuwa mwanaume atakua analalia kitanda kilichonunuliwa na mama mkwe)lakini si bado hela iliyotumika kununulia kitanda hata kama wameenda mume na mke si katoa mama mkwe???!!!!!!!!!! Nahitaji kufafanuliwa hapa.

Nilichosema ni kuwa
kama watu wamefunga ndoa
mnaweza kuwaambia shikeni hii milioni kumi au 15
mtaanzia maisha mtajua wenyewe vipaumbele vyenu
sio eti wazazi mkae muanze orodhesha sijui vitanda,sijui mashuka..
sijui kiwanja......hiko ndo napinga
tazama alichoongea Fixed point hapo juu alipokuwa mwanakamati wa harusi
 
Umenijibu kwa ufasaha kabisa
Na hiyo ndio ilikuwa point yangu kuwa kuachana kwa sababu tu ya pesa si lazima
Kama kuna sababu zingine ilikuwa halali yake huyo dada kubwaga manyanga.

Hiyo ya kudate mwanamme mdogo kuliko mie, hiyo ni marfuku kama mbwa kupanda darini.
Hao akina Maria Carey wakae nao wao, huku kwetu NO.
Kwanza napenda akija nimpokee, nimwamkie na goti, ntaamkia vipi kitoto lol

Mimi nina dada yangu mtoto wa shangazi...aliolewa mkubwa though sina hakika na umri kamili...ila tulishajua hawezi tena kuolewa.

Sasa huyu dada alikuwa ni milionea mdogo; ana nyumba kadhaa mpaka ma guest house. Afu mtu eti kaingia King.

Kwani walidumu? Huyo jamaa si kuwa alikuwa masikini sana ila alikuwa kwanza mdogo ki umri; pili ana ka umarioo ela zake zote kwenye pombe anajua wife anazo...na nadhani alikuwa hajatulia vile vile...kwa ufupi kila mtu alikuwa anamuona amefuata maslahi. Walitengana baada ya sijuhi miaka kumi ...ya uvumilivu uliotukuka kwa upande wa sister...lakini alibwanga manyanga...ameambulia watoto.

Tatizo laweza kuwa pande yeyote kwa mke kuleta dharau au mume kuwa mume maslahi from day one...a.k.a. tapeli alofuata ela na si penzi. Kwa sababu most of these rich girls ni wakubwa ki umri..ukitoa hao wa utajiri wa baba.

Kukujibu kama wanaoolewa aged ndoa zinadumu au hazidumu...jibu langu mimi kama NK ni kuwa uwezekano wa kudumu ni mdogo kama mume ni mdogo ila ni mkubwa akiolewa na mzee mwenzie...mostly mjane wa kiume au dovorcee.

Usilete mifano ya US sijuhi Mariah Kelly sijuhi nini naongelea utamaduni wa kiafrika ambao age is still everything.
 
Na msisahau
haya maharusi wenye sauti sio wale wahusika
kunakamati,mjomba,,mama aliechangia harusi za wenzie
na kadhalika na mashindano na kurushana roho

jiulize umealikwa harusi ya Smile na Mr ROCKY mfano
halafu ndani ya harusi kuna kumtunza mama yake smile kwa mabulungutu ya pesa
as if watu tumekuja kuona 'show za kutunzana pesa'

sasa kuna influence nyiingi mno
mimi nina aunty ambae keshachangia harusi zaidi ya 100
unaweza pata picha harusi ya mwanae atakavyolipiza mbwembwe na jinsi mwanae atakavyokosa sauti
hata kama mwanae atataka harusi ndoogo tu isiyo na mbwembwe..

Halafu The Boss tutagombana, mambo gani hayo kumtaja laaziz wangu na kimwana Smile wakati mkewe nipo????!!!uacheeee.
:focus: Binafsi huwa sielewi hilo swala la kumtunza mama limeanzia wapi??anatunzwa kwaajili ya nini???kumlea binti mpaka kuolewa au???!!! Ni jukumu lake kumlea mwanae sasa anatunzwa ili iweje???!!!jamani kuna mambo siku hizi inabidi kuyaangalia tu na kuyaacha kama yalivyo. Mbona baba huwa hatunzwi?au huyo mtoto kalelewa na mama pekee?! Ngachoka kbsaaaa chaa!
 
Last edited by a moderator:
Asante The Boss.....
tulipofikia ni kubaya nilishahuhudia mama ameenda kumtukana mume wa mtoto wake na kumfukuza kisa tu support kubwa ya kifedha mpaka nyumba wanayoishi binti alipewa na wazazi.

Ni bora wazazi kuwasaidia watoto pesa tu
lakini vitu vingine wafanye wenyewe
Mzazi unamnunulia mpaka mtoto kiwanja
Mzazi ukifa mtoto wala hajui ofisi za ardhi zilipo
wala hajui kuna kodi za viwanja kumbee

Kufanya wenyewe kunawafanya wa discover themselves pia
vitu kama tastes na ulazima au umuhimu wa kununua hiki au kile

Na msisahau tunaishi kwa connections...sasa mtoto lazima atengeneze connections zake pia
sio kila kitu arudi kwa baba au mama...apewe ki memo...
Mnasomeshas watotto Ulaya
Barua za kuomba kazi mnawaandikia
Interview pia mnawapa vimemo
Kazi kama ina tatizo mtoto anarudi ku ripoti kwa wazazi na sio kupigana huko huko oficin
Viwanja muwanunulie
Magari muwapatie

Halafu mnashangaa kwa nini wanakunywa sumu sababu ya boyfriend'girlfriend????
 
Umeona eeh. Haya mambo watu hawaoni kuwa ni tatizo mpaka pale ndoa inapoanza migogoro...ndio utajua kama gari ni lako au walikupa wakwe. Lol.

Si kuna mtu alitimuliwa na mfuko wa rambo maana nyumba ya wife.

Afu wanawake wengi hatunaga huruma hasa mume akianza ukichehche...ni ngumu kuvumilia ushenzi wakati mtu yuko kama mkimbizi hana kitu.

Asante The Boss.....
tulipofikia ni kubaya nilishahuhudia mama ameenda kumtukana mume wa mtoto wake na kumfukuza kisa tu support kubwa ya kifedha mpaka nyumba wanayoishi binti alipewa na wazazi.
 
Umenijibu kwa ufasaha kabisa
Na hiyo ndio ilikuwa point yangu kuwa kuachana kwa sababu tu ya pesa si lazima
Kama kuna sababu zingine ilikuwa halali yake huyo dada kubwaga manyanga.

Hiyo ya kudate mwanamme mdogo kuliko mie, hiyo ni marfuku kama mbwa kupanda darini.
Hao akina Maria Carey wakae nao wao, huku kwetu NO.
Kwanza napenda akija nimpokee, nimwamkie na goti, ntaamkia vipi kitoto lol

Hahahaaaaaa Kongosho nafwaaaaa........goti lina utamu wake ati haloooooo
 
Last edited by a moderator:
Kwa jinsi maisha ya sasa yalivyo magumu, kama unamwoa mwanamke atakayekuja na vitu vyote hivyo ni jambo la kushukuru sana.
 
Umeona eeh. Haya mambo watu hawaoni kuwa ni tatizo mpaka pale ndoa inapoanza migogoro...ndio utajua kama gari ni lako au walikupa wakwe. Lol.

Si kuna mtu alitimuliwa na mfuko wa rambo maana nyumba ya wife.

Afu wanawake wengi hatunaga huruma hasa mume akianza ukichehche...ni ngumu kuvumilia ushenzi wakati mtu yuko kama mkimbizi hana kitu.
watu wanaongea tu...wanawake tulivo ni ngumu sana mimi nitaenda na chupi tu kwa kweli
 
Kwa jinsi maisha ya sasa yalivyo magumu, kama unamwoa mwanamke atakayekuja na vitu vyote hivyo ni jambo la kushukuru sana.
na vijana wa siku hizi mlivo iresponsible mnapenda kweli siku ukikutana na malboro ya voboksa vyako viwili getini usije kulia hapa
 
Nilichosema ni kuwa
kama watu wamefunga ndoa
mnaweza kuwaambia shikeni hii milioni kumi au 15
mtaanzia maisha mtajua wenyewe vipaumbele vyenu
sio eti wazazi mkae muanze orodhesha sijui vitanda,sijui mashuka..
sijui kiwanja......hiko ndo napinga
tazama alichoongea Fixed point hapo juu alipokuwa mwanakamati wa harusi

Gotcha u bro! Umeongea vizuri sana imeniingia maana hata wakinunulia nguo zao za ndani nyie hamtajua kama mkwe wetu leo kavaa ile pichu....lol
Na kama hivyo ndivyo haina haja ya kuwakabidhi hizo hela mbele ya umati wa watu si wapeane nyumbani tu kwamba wanetu sisi kama wazazi tumeonelea tuwape hizi pesa zitawasaidia kuanzia maisha,uamuzi ni wao kununua Kuger ama kuzinywea chibuku shauri yao!
 
Zawadi nzuri ni ile unayopewa nyumbani mkiwa ndugu tu
au watu wa karibu
sio zawadi inaletwa na matarumbeta na mc mishipa imemtoka....
hiyo sio zawadi
hiyo ni 'show off'
 
watu wanaongea tu...wanawake tulivo ni ngumu sana mimi nitaenda na chupi tu kwa kweli

Hahahaaaaaaaa Smile akhsante sana kwa huu msredi nimecheka leo aaahhhh hapana
 
Last edited by a moderator:
Wale wale kwa nini hufikiri kutafuta pamoja unafikiria kushukuru.... unafikiri kwa kujaziwa nyumba ndio ugumu wa maisha utakuwa umeisha jamani ndoa ni zaidi ya makochi masufuria na mazagazaga yote.

Back
Top Bottom