kibiasharazaidi
Member
- Mar 15, 2013
- 17
- 7
kuna mshkaji miaka ya zamani kidogo alipewa dozi ya malaria akawa hapati nafuu, kumbe alikuwa na typhoid, baada ya wiki moja akatokea jamaa ambaye alishawahi kuugua typhoid akamshauri akapime typhoid kwa daktari mwingine, akakutwa na typhoid na ilibaki kidogo ifikie stage mbaya. jamaa akatumia dozi ya typhoid akapona kabisa.Nilichogundua ni kwamba kwenye hospitali nyingi za mikoa, kushuka chini asilimia kubwa ya wagonjwa wakifika tu kwa madaktari wanapatiwa dawa za malaria hata kabla ya vipimo, na hata vipimo visipoonyesha uwepo wa wadudu hao, bado utapatiwa dawa. Hivi nyie madaktari wetu kwani ugonjwa ni malaria tu mnaoujua? hamna magonjwa mengine mnayoweza kutibu?
A negative blood smear for malaria parasites does not rule out malaria.Ndio maana madaktari wameenda shule.Ukitaka kuelewa zaidi na wewe nenda darasani ukafundishwe kama hao madaktari.
Tatizo siku hizi kila mtu anajifanya anajua kutibu, hatufuati ushauri wa wataalamu hawa.Wewe unaijua life cycle ya malaria parasites?kuna kipindi hivi vijidudu vinakuwa kwenye ini na havipatikani kwenye peripheral blood smear, daktari anaelewa anachofanya dalili za malaria zinaweza kumsaidia kuanzisha tiba hata kama majibu ya damu hayaonyeshi vidudu.Msiingilie kazi za wataalamu.
its tricky!
matibabu ya mgonjwa yanategemea historia, upimaji wa mwili na majibu ya maabara.
majibu ya maabara yana mchango mdogo katika kuamua matibabu ya mgonjwa.
kwa mazingira ya kwetu (ambapo wagonjwa wengi hawana family dr) dr. hana uwezo wa kumfuatilia mgonjwa kwa ukaribu anaweza kutibu hata kama malaria haijaonekana. kama mgonjwa anakuwa na family dr, akizidiwa anaweza kumpigia family dr wake akampatia matibabu.
sijaenda shule ya udaktari lakini nimeenda shule zingine na najua kutumia common sense na pia nasoma sana hata vitabu vyenu, kama sio malaria kali, hakuna haja ya kutoa dawa mpaka ithibitishwe kwa kuwa mnatengeneza usugu wa madawa
its tricky!
matibabu ya mgonjwa yanategemea historia, upimaji wa mwili na majibu ya maabara.
majibu ya maabara yana mchango mdogo katika kuamua matibabu ya mgonjwa.
kwa mazingira ya kwetu (ambapo wagonjwa wengi hawana family dr) dr. hana uwezo wa kumfuatilia mgonjwa kwa ukaribu anaweza kutibu hata kama malaria haijaonekana. kama mgonjwa anakuwa na family dr, akizidiwa anaweza kumpigia family dr wake akampatia matibabu.
dalili zamalaria mara nyingi ni sawa na za magonjwa mengine kama typhoid, kwa hiyo dr unataka kusema kwamba ukifikiria tu ugonjwa basi uutibu? kama ni hivyo sina haja ya kuja kwako kwa sababu dalili za malaria nazijua na ntanunua dawa dukani

Mkuu ulichosema ni kweli kabisa,ila kifanyike kwenye malaria kali tu! ninachohoji hapa ni sisi tunaoenda hospitali kwa vidalili vya kichwa kuuma, kizunguzungu, maumivu ya viungo n.kMkuu unayo haki ya kuhoji hivyo lakini linapokuja suala la tiba,weledi na kipaji,wito na kujitoa ni vitu muhimu sana!wakati mwingine ni muhimu kwenda nje ya miongozo rasmi iwapo unadhani ni muhimu kuokoa maisha ya mgonjwa!Sijui iwapo umewahi kujiuliza pia accuracy ya vipimo vya malaria maabara?kwani inatokea sana mtu anacheki asubuhi anakuta hana malaria parasites halafu hapewi dawa za malaria ingawa ana kila dalili!sasa unakuta analazimika kurudi hospitalini usiku wa manane akiwa kazidiwa sana na ukicheki tena malaria unakuta inaonekana!Wataalam wa maabara watwambie ukweli ni kwa nini hutokea hii?Hii inakuwa mbaya kwa mtoto.Nimewahi kuona mtoto kazidiwa sana na walivyocheki malaria hawakuona hivyo alipewa antibiotic tu na painkillers!lakini homa haikwisha na walikuwepo madaktari wenye imani kuwa usipoona majibu ya kuwa na malaria basi is muhimu kutoa dawa za malalia!Yule mtoto hatimaye alianza kupata degedege na alifariki wakijaribu kumpa dawa za kuzuia degedege!Ninavyojua ujuzi wa kugundua tatizo kwa 75% inapaswa kufanywa na daktari na 25% iliyobaki ni support ya vipimo ili ku confirm alichokuwa anafikiria daktari.Sasa naona siku hizi hata wananchi wa kawaida wanaamini vipimo vya maabara ni zaidi ya uwezo wa daktari kugundua tatizo.Hiyo inaweza kuwa Ndio kwa baadhi ya magonjwa ila sio malaria kwani malaria ni deadly disease!Ukichelewa kuitibu inaweza kugharimu muda,raslimali na hata maisha ya mgonjwa.Acha wenye taaluma yao watumie ujuzi wao kutoa huduma kutokana na mazingira yetu!
Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
UNAJUA POSITIVE PREDICTIVE VALUE NA NEGATIVE PREDICTIVE VALUE YA KIPIMO CHA MALARIA (BS) NA WIDAL TEST?
unajua prevalence ya typhoid hapa Dar?
UNAJUA TAFSIRI YA KIPIMO CHA TYPHOID (WIDAL TEST) KUWA POSITIVE MAANA YAKE NI NINI?
JE UNAJUA NI MUDA GANI UNAPITA MTU ALIYEKUWA POSITIVE KUWA NEGATIVE?
tatizo la watanzania kila kitu wanajua wao.ngoja siku mtoto wako awe na homa ulete kujua kwako; ndio utajua majuto ni mjukuu.
Mgonjwa mwenye homa kama vipimo vimeonyesha sio malaria basi anatakiwa kupimwa vitu vingine vinavyoweza kusababisha homa.
Wakati vipimo vinaendelea anaweza kupewa dawa ya kutuliza homa na dalili nyingine za ugonjwa wake.
Kama daktari hana vipimo anatibia "emperically" kwa kutoa dawa ya ugonjwa anaodhani una uwezekano mkubwa kumuathiri mgonjwa.
Tafiti zinaonyesha kiwango cha malaria ni kidogo sana Tanzania. Homa nyingi Tanzania husababishwa na magonjwa ya bacteria na virus. Tatizo ni kwamba wapo madaktari ambao hawasomi taarifa mpya na wanaendelea utaratibu wa zamani wa kutoa dawa ya malaria kwa wagonjwa wenye homa. Utaratibu huu hutumika sehemu zenye maambukizo mengi, ambayo Tanzania sasa hivi sehemu nyingi haziko hivyo, ingawa kuna wilaya kama Karagwe ambako maambukizi ni mengi.
Dar es Salaam maambukizi ya malaria ni machache sana. Kwahiyo kutoa dawa za malaria kwa kila homa tusiyojua sababu yake Dar es Salaam si sahihi whereas kwa Karagwe inaweza kuwa sahihi.
Sounds professional! ahsante
UNAJUA POSITIVE PREDICTIVE VALUE NA NEGATIVE PREDICTIVE VALUE YA KIPIMO CHA MALARIA (BS) NA WIDAL TEST?
unajua prevalence ya typhoid hapa Dar?
UNAJUA TAFSIRI YA KIPIMO CHA TYPHOID (WIDAL TEST) KUWA POSITIVE MAANA YAKE NI NINI?
JE UNAJUA NI MUDA GANI UNAPITA MTU ALIYEKUWA POSITIVE KUWA NEGATIVE?
tatizo la watanzania kila kitu wanajua wao.
ngoja siku mtoto wako awe na homa ulete kujua kwako; ndio utajua majuto ni mjukuu.
Nadhani Mpigania Uhuru ameweka wazi hapa.mie nilifikiri unatafuta maoni ya kitaalamu kumbe uko kwenye ligi!endelea kujinywea dawa kwa kusoma vitabu mbalimbali.ipo siku utahitaji maelekezo ya kitaalamu, kwa kuwa haujui pharmacodynamics na pharmacokinetics ya hizo dawa unazomeza.