Mkuu unayo haki ya kuhoji hivyo lakini linapokuja suala la tiba,weledi na kipaji,wito na kujitoa ni vitu muhimu sana!wakati mwingine ni muhimu kwenda nje ya miongozo rasmi iwapo unadhani ni muhimu kuokoa maisha ya mgonjwa!Sijui iwapo umewahi kujiuliza pia accuracy ya vipimo vya malaria maabara?kwani inatokea sana mtu anacheki asubuhi anakuta hana malaria parasites halafu hapewi dawa za malaria ingawa ana kila dalili!sasa unakuta analazimika kurudi hospitalini usiku wa manane akiwa kazidiwa sana na ukicheki tena malaria unakuta inaonekana!Wataalam wa maabara watwambie ukweli ni kwa nini hutokea hii?Hii inakuwa mbaya kwa mtoto.Nimewahi kuona mtoto kazidiwa sana na walivyocheki malaria hawakuona hivyo alipewa antibiotic tu na painkillers!lakini homa haikwisha na walikuwepo madaktari wenye imani kuwa usipoona majibu ya kuwa na malaria basi is muhimu kutoa dawa za malalia!Yule mtoto hatimaye alianza kupata degedege na alifariki wakijaribu kumpa dawa za kuzuia degedege!Ninavyojua ujuzi wa kugundua tatizo kwa 75% inapaswa kufanywa na daktari na 25% iliyobaki ni support ya vipimo ili ku confirm alichokuwa anafikiria daktari.Sasa naona siku hizi hata wananchi wa kawaida wanaamini vipimo vya maabara ni zaidi ya uwezo wa daktari kugundua tatizo.Hiyo inaweza kuwa Ndio kwa baadhi ya magonjwa ila sio malaria kwani malaria ni deadly disease!Ukichelewa kuitibu inaweza kugharimu muda,raslimali na hata maisha ya mgonjwa.Acha wenye taaluma yao watumie ujuzi wao kutoa huduma kutokana na mazingira yetu!
Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums