Kwenu vidume mnaojifanya hampendi umbea ila hamkauki celebrities forum

Kwenu vidume mnaojifanya hampendi umbea ila hamkauki celebrities forum

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
70,916
Reaction score
141,437
Huwa nawashangaa hadi nimechoka kuwashangaa, nawashwa washwa kuwauliza...UNAPOINGIA CELEBRITIES FORUM UNAJUA NI NINI UNAKUJA KUSOMA? au huwa hamuelewi maana yake?kuna mtu huwa anawatag mje kusoma umbea wa hili jukwaa???

Mi huwa nawashangaa mno na kuwaona malofa msiojielewa, Hance Mtanashati akileta ubuyu hapa mnakuja kama nzi kwenye mavvvv "mwanaume hupendezi kuwa mbea" kawaambia anataka kupendeza? "mara mna wasiwasi na jinsia yake" mnataka muijue jinsia yake ili iweje nyie jinsia zenu nani kawauliza, sasa hampendi umbea jukwaa la story za umbea mmefata nini, mmeambiwa huku kunauzwa vifaa vya bodaboda? alieweka majukwaa tofauti tofauti alikua na akili alijua interests hazifanani kama hampendi umbea nendeni huko jf garage mkaangalie aina za magari na spana zake, nendeni intelligence forum huko mkiingia huku wote ni wambea mwandishi, wasomaji wachangiaji wote wambea. Majukwaa zaidi ya 30 yooote umeyaacha umekuja celebrities forum na unasema hupendi umbea, kenge!!!!

Hance Mtanashati binafsi nakukubali sana, nakukubali kwa ubuyu ila pia una roho ya kipekee pamoja na kuandamwa na hawa vidudu watu haujali maneno yao unaleta tu ubuyu na wala hauna hasira hata chembe warumi ye hadi hasira huwa zinampanda ila we upo cool, nakupenda bureeee. Usiache kutuchangamsha na ubuyu ikibidi tumia umbea kama fursa si unawacheki kina soudy na kwisa umbea unawaweka mjini, afu vitumbili vinakuja huku kudiss tu kifalafala shwain.
 
IMG_20181106_181613.jpg
 
Mm huwa napenda sana kuheshimu mawazo yanayo telewa na mwanamke siku zote huwa yanajenga....... Haya mawazo aliyo kuja nayo asubuhii yote hii kabla hata hajapata kifungua kinywa na kuanzisha mada kama hii asubuhi yote hii ni kitendo cha ujasiri tena ujasiri ulio tukuka, wakipatikana wataalamu na wasomi wanaweza kuyageuza haya mawazo ya huyu mdada na kuyafanya kuwa kiwanda cha kusindika tumbaku na tukawa tumeongeza ajira........ Na huyu dada akawa Bilioner within a minute, tukawa tumeongeza billioner mwingine Tanzania
 
Umekariri kwakua hujanywa chai unajua kila mtu hajanywa? Na asubuhi hii kabla hujanywa chai nawe ushakuja kusoma umbea tayari huku niliko ndo nmemaliza kupata dinner mie....bilionea mbea una kiwanda!?
 
Evenly salt namkubali Sana kupita maelezo..yeye na miss chagga walinifanya niipende Sana jf.afu ukitegemea bila shaka atakuwa umri sawa na mama zangu wadogo.kila unalosema hukoseagi
 
Unajua kipndi cha kwanza etii..! Sasa mwalimu wa hivi kuna haja ya kwenda shule kweli kwa wanetu???

Bila shaka ni mwalimu wa kiswahili huyu..!
 
Crush kashasema...huwa hakosei

Mamii twendezetu tukaandae lesson plan sasa tuwaache wakipanda na comments[emoji23] [emoji23]
 
Huwezi kuwa cool kila muda... Kuna vitu mtu lazima afanye ikiwa na kupitia humu kumaliza stress zake, na haimaanishi yeye ni fala au lofa kisa ni mwanaume. Dunia huwezi ibadili ila unaweza kujitengenezea ulimwengu wako wa kuishi....

Sio kila siku habari za viwanda tu ili kuonekana na watu uko serious na vitu unavyofanya. Hata anko Magu anaangalia shilawadu..
 
Ukizingatia wabongo tunaupenda na kuuweza sana umbea....huko kwingine siasa michezo tupo tupo tu vichwa chini miguu juu
 
Kazi yangu masaa kumi na mbili nipo kwenye kompyuta,nikipata break napita kwenye threads zozote zile kuondoa stress,afu muache kudharau watu wa sengerema.
 
Back
Top Bottom