Kwenu viongozi wa Simba SC

Kwenu viongozi wa Simba SC

NAJYUZ

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2021
Posts
1,981
Reaction score
3,475
Siku zote ambazo simba imekua ikipoteza mechi au ikifanya vibaya baadhi ya mashabiki na viongozi 'huwaga' wanatoa madai ya kujuhumiwa.

Walianza kumsimamisha Said Tully kwa madai hayo hayo ya hujuma then wakamrudisha tena kundini, pia wakarudi kwa haji manara kwa madai ya kua anatumiwa na GSM kuihujumu simba.

Madai ya mashabiki na baadhi ya viongozi yalienda mbali mpaka wakamtuhumu Patrick Rweyemamu baada ya kufungwa na jwaneng galaxy kua aliuza ramani.

Jana ndio ilikua kituko baada ya hamasishaji la mabingwa wa nchi ndugu mwijaku kusema kwamba yanga anacheza mechi za simba,na akienda mbali mpaka kudai kua coastal union hawana uwezo wa kulala kwenye hotel nzuri kama walizofikia pindi alipokuja kucheza na simba.

Kitu nachojiuliza ni kwamba viongozi wa simba walituaminisha kua simba ni next level na kama timu ni next level basi wao wako more advanced na wanaamini katika science ya mpira.

Sasa kama unaamini katika science ya mpira, kwanini unakuja mbele ya public na kumshutumu mtu au taasisi ilihali yeye hachezi uwanjani na wala hayupo katika benchi la ufundi, hivi kweli penalty aliyokosa John Bocco na biashara au goli la jana la wazi alilokosa Kibu Denis utasemaje kua Yanga anakuhujumu?

Timu ikifungwa viongozi na mashabiki wanatakiwa waamini kua ni mambo ya ufundi ndio yalienda vibaya na sio kadhalika.

Football is an art.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yule babra siku izi amepoa sana tofauti na kipindi cha nyuma alikuwa front kwenye kila tukio sijui matokeo yamemchanganya au ndo zile nyepesi nyepesi bosi mkubwa anaanza kujiweka pembeni mdogo mdogo maana nasikia ata bonus alizokuwa anatoa kipindi bado ni mwenyekiti wa bodi atoi tena!
 
Yule babra siku izi amepoa sana tofauti na kipindi cha nyuma alikuwa front kwenye kila tukio sijui matokeo yamemchanganya au ndo zile nyepesi nyepesi bosi mkubwa anaanza kujiweka pembeni mdogo mdogo maana nasikia ata bonus alizokuwa anatoa kipindi bado ni mwenyekiti wa bodi atoi tena!
[emoji23][emoji23][emoji23] Na Hanspope hayupo sijui itakuaje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom