Usijaribu kuingia na hiyo mentality na huo uhakika wa mil 8 utaumia na kuchukia watu.....
Uzuri kuna rafiki angu alilima tikiti nikiwa nae bega kwa bega.....ni hiyohiyo heka 1 tena alilima kwa kumwagilia Dodoma pale.....
Kwanza aliset shamba vizuri sana na kufunga mipira ile ya maji vizuri (mipira ile inafanya drop irrigation kama sijakosea), akazungushia uzio vizuri sana na kuhakikisha supply ya maji ni ya kutosha tena yanatoka bombani na anamatank yake makubwa 10 na muda wote yanejaa maji......
mbegu zikapandwa vizuri, baada ya kupanda mbegu, ikaja shida ya kunguru kufukua mbegu, tukatafuta ile mikanda ya zamani tukatoa ile kama ramani ya ndani sauti yake inafukuza wanyama au ndege ikifunga......
limeisha hilo mbegu zikaanza kutoa majani vizuri kabisa....panzi wakaja wakawa wanajificha chini ya majani wanakula focal point za muhimu za majani.....tukaanza ona majani yanasinyaa, hapo tuliishapiga dawa ya kwanza ila tukapiga dawa nyingine kidogo ikasaidia.....
Mbegu zikaota matikiti yakaanza ota vizuri tu, shida ikaja matikiti mengi yakadumaa hivi, hadi yanakomaa yakawa madogo sana..... Wiki 2 kabla ya kuvuna, wakaibuka wezi wanaiba hadi 4 kwa siku, tukatoa uangalizi yakavunwa yakiwa machache sana hayazidi 500 .....
Mwisho wateja wakawa hamna, ikabidi watu wakopeshwe na majirani wakopeshwe vizuri zaidi .....wadeni wasiozidi 50 ndio walilipia......biashara ikawa imeleta hasara
Huyo jamaa amesema (ukaamua kuuza) hamna mtu anaamua kuuza bei fulani bali dalali ndio anakuamulia bei, maana masokoni bila madalali mzigo wako utakuharibikia.....
Hivyo hiyo hesabu haina uhalisia kabisa nimeshuhudia.