Kwenu wanaJF: Saint Anne ninawashukuru mno

Pole sana St.Anne.Mungu ni mwema aendelee kukutia nguvu kipindi hiki unachopitia.Mshukuru Mungu baba amewafikisha hapo walau mnajitambua.Mmeuonja upendo wake.Wengine wazazi wanafariki watoto wakiwa wadogo imagine unakuja kuoneshwa picha tu.Yote kwa yote amani ya Mungu itawale moyoni mwako.
 
Pole sana Saint Anne Mungu akutie nguvu

Ruhusu nafsi yako iamini kwamba Baba haupo nae tena, iruhusu pia nafsi yako iamini kwamba maisha lazima yaendelee baada ya msiba, iruhusu pia nafsi yako iamini kwamba Sote tupo njia moja, baba ametutangulia na tutafuata, ukiweza kujinasua kwenye hayo basi hiyo depression itaondoka automatically, jipe muda najua sio rahisi lakini this too shall pass

Naamini wewe ni Mkristo, sisi wakristo tunaamini kuishi ni kristo na Kufa ni faida, hili neno hata kwenye Biblia linaandikwa, endelea kumuombea baba na kuyaenzi mema aliyokuachia ili aendelee kupumzika kwa amani

Mshukuru Mungu na usonge mbele, Mungu akuponye majeraha na maumivu yote uliyoyapitia kwa kumpoteza baba, you still have 10000 reasons to live.
 
MUNGU aendelee kukutia nguvu Sis na familia nzima, May his Gentle Soul keep resting in Eternal peace
 
Pole sana saint Anne

Baba amepumzika, Mungu akupe moyo wa kukubali na amani

Nimesoma hii post nikaona una mengi mazuri yanayokuumiza kwa kumkosa, ila una mengi zaidi ya kumshukuru Mungu kwaajili ya uhai wake kwani amekua baba bora sana

Ametenda mema, ametenda yaliyompasa, amemaliza kazi na ameenda kupumzika kwa Mungu wetu

Lala salama baba saint Anne 🙏
 
Dada ukiendelea hivyo utajitesa na mwisho utamkufuru Mwenyezi MUNGU shida uliyo nayo ni ya akili kukubali baba hayupo tena chakufanya endelea mbele yawezekana una deni hukutimiza ila you still have time,mweke baba katika sala Fanya yote mazuri aliyokufundisha ndio njia sahihi yakuendelea kuishi nae katika maisha mazuri yake yapo endelea kuyaenzi utamwona baba yupo kila wakati,biblia unasema kila jambo na wakati wake kuna wakati wakulia na wakucheka.....ruhusu akili yako kukubali kazi ya MUNGU kama una jambo unaweza kwenda katika mahali alipopumzika na ukanena nae kwa imani na ukapata suluhu,mwache baba apumzike kwa amani usijifunge na manung'uniko,amani iwe juu yako na familia nzima
 
Kwakweli hiki ni kipindi kigumu sana kwako, tuliopitia huko tunaweza elewa ni namna gani unahisi my dear, nikupe pole kwa mara nyingine

Lakini pamoja na yote tunakuombea Mungu akushike mkono uvuke salama katika pito hili gumu kwako

Na zaidi ya yote muda ni uponyaji mwingine Mungu aliyoweka kwajili ya kutufuta machozi na kutusaidia kusonga mbele

Hivyo my dear kua imara huku ukimtegemea Mungu nae atakuimarisha zaidi na zaidi. Baba ameumaliza mwendo kazi kwetu tuliobakia tujipange tujue nasi tutaumalizaje huu mwendo kila mmoja kwa wakati wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…