Kwenu wanaJF: Saint Anne ninawashukuru mno

Kwenu wanaJF: Saint Anne ninawashukuru mno

Hakuna njia ya mkato katika kuomboleza. Kwa sasa ukijisikia kulia lia. Tena lia kabisa bila woga. Na huwa tunasema kuwa muda ni tabibu mwema. Naam! Jipe muda. Endelea kusali. Omba faraja na mwongozo wa Roho Mtakatifu.

Kwa sasa ni giza lakini kwa jinsi muda utakavyokuwa unapita, pole pole kutaanza kupambazuka na Mungu wako unayemwabudu hatakuacha. Japo pengo la mzee halitazibika kamwe lakini tabasamu litarejea tena katika uso wako, moyo huo unaouma utaanza kupona na maisha yataendelea. Dumisha mema yote aliyokufundisha baba yako; na kupitia kwako mzee huyo ataendelea kuishi.

Pole sana. Mungu Atakuinua tena [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
Amen
 
Time is a best healer,

Vitu vinapotukuta huwa tunaona kama tumeisha au dunia imeishia hapo ila muda hutufundisha kuishi na kumbukumbu zote pasipo kutuumiza kama mwanzoni..

Mungu akawe chanzo cha nguvu, faraja na uponyaji wako katika kipindi hiki kigumu saint Anne
Amen
 
Pole sana Saint Anne! Inauma sana kumpoteza mzazi ila ni mapito ya hapa duniani cha muhimu ni kujikaza najua ni ngumu ila haina jinsi mzazi anauma sana. Waliosema msiba usikie kwa wengine ila usiwe kwako hawakuwa mbali kabisa na uhalisia yani it hits so hard ila tuko pamoja na wewe kama moja ya wanafamilia wa jf i pass my condolences for the loss!
Amen
Akhsante bro.
 
Pole ndugu, ila nikupe moyo tu usiwaze Sana kuhusu maisha bila ya baba, aliefanya wewe uwepo atajua utaendelea vipi, aliefanya baba yako kuwepo na wewe kutokea kwake na aliefanya baba yako asiwepo muda huu ndie huyo huyo atahakikisha haukwami.

Mimi nimeishi bila baba na mama tokea nikiwa chini ya mwezi mmoja na niliweza kuvuka na Leo nimesimama vipi ishindikane kwako? Tena wewe unaeamini?

Ombi langu Ni baba yako ajaliwe kukutana na Mungu wetu alietuumba bila ya Shari.
Amen.
Ni kipindi kibaya kuwahi kupitia maishani
 
Kifo ndio mwisho wa kila kiumbe chenye uhai,mtu husikitika na kuumia kwa kuondokewa na mtu wake but one day we will all die,

Weka imani yako kwa muumba hope utarudi katika hali yako ya kawaida,uzuri sisi binadamu Mungu alituumba kusahau.
Amen
Akhsante
 
Back
Top Bottom