Kwenu wanaJF: Saint Anne ninawashukuru mno

Kwenu wanaJF: Saint Anne ninawashukuru mno

Pole sana mkuu yote ni mitihani tu ya maisha yetu hapa duniani maana tunapita i know hali unayopitia mke wangu alimpoteza baba yake(yetu) nov mwaka jana mpaka leo bado hajarecover so nakuelewa
Akhsante..

Tofauti yangu na mkeo,yeye ana mume na watoto,mimi sina mume wala watoto,mimi bado ni mtoto.
 
Ashukuriwe na kuabudiwa,kazi yake haina makosa,naye atabaki kuwa Mungu,pole sana endelea kumuomba Mungu akutie ujasiri wa kusonga mbele....
 
Pole sana ila umeharibu kutajataja majina, kama shukrani ungetoa za jumla tu. Msiba sio sherehe kuanza kutajana majina.
Dukuduku langu ni hilo ila pole sana.
Akhsante.

Samahani kama nitakuwa nimekosea kutaja majina lakini nimetaja machache kwa niaba ya wengi waliokuwa nami.
Nafsi yangu kuna namna imeridhika kwa kutaja hayo majina.
 
Pole Sana Saint Anne kwa msiba huu mzito wa kuondokewa na baba naelewa Ni situation gani unaipitia ..hisia,majonzi nk Lakin nakuombea kwa Mungu wetu Alie hai akuvushe salama katika kipindi hiki kigum.
Ni kipindi unahitaji faraja na sisi tuko pamoja na wewe..!
Mungu alitoa na Sasa amechukua
Jina lake lihimidiwe.
Amen
Amen.
Ubarikiwe .
 
Back
Top Bottom