Kwenu Wanaume mnaozaa na michepuko

Kwenu Wanaume mnaozaa na michepuko

Nakadori

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
8,778
Reaction score
21,010
Waungwana na wasio waungwana nawasalimu.
Ninaandika haya nikiwa na masikitiko mengi sana...
Niko kwenye tukio moja la kifamilia ambapo imelazimu watoto wote wa mji husika kuwepo.
Ni tukio kubwa kiasi kwamba hata sisi tusio ndugu tumeshiriki.
Nimeumia kuona katoto ka nje ambako kwa makadirio kalizaliwa wakati baba mwenye mji akiwa tayari ndani ya ndoa kakiwa kwenye mazingira ya uchafu kuanzia mwili hadi mavazi. Mwili umesheheni mapunye ambayo inaonekana kabisa yamekuwa hapo kwa muda mrefu bila huduma. Nywele hazijanyolewa ni kama yule kiumbe wa Gods must be crazy.... nimeumia sana.

Baba na mama wa mji huu wana uwezo mkubwa sana na watoto wengine wapo vizuri kiafya na mengineyo.

Nikawaza ukute mama wa mtoto hajui mazingira haka katoto kanayoishi kwakuwa tu baba mtoto amelazimisha aishi na mwanae kwa sababu za kibinafsi...na sasa mtoto anaishi maisha ya kunyanyapaliwa.

Lakini pia nimeumia kuona mwanamke I mean huyu mama wa kambo kuruhusu huyu mtoto kusafiri umbali mrefu na hali ya uchafu ule huku watoto wake wakiwa smart. Kwa nini ambague ? Hajui kwamba hata yeye anaweza kufa wanae wakalelewa na mama wa kambo? Hata kama amesalitiwa lakini huyu mtoto hana kosa lolote.

Wanaume kabla hamjazaa na michepuko yenu jipimeni na muwe na uhakika kama ki akili mko wazima kiasi cha kuweza kusimama na hawa watoto. Lakini pia punguzeni ubinafsi na kuwatoa hawa watoto kwa mama zao kwa kukwepa gharama za mara kwa mara atakazotaka mama mtoto. Hii ni gharama ambayo lazima muilipe kwa kupambana na matokeo ya starehe zenu.
Mje na matusi mapya

Picha haihusiani na uzi wangu
images (28).jpeg
 
Kuna Binti mmja nilikuwa namjua aliishi maisha magumu saana kumbe baba yake ni mtu mkuu Sana,ishu ilikuwa Kwa mama tuu,baadaye alirudi Kwa babaye anakula kuku Kwa mrija
 
Back
Top Bottom