Kwenu wanawake, njia pekee ya kugundua mwanaume anakupenda ni pale akili yake inapofanya maamuzi baada ya kupiga mshindo (post nut clarity)

Kwenu wanawake, njia pekee ya kugundua mwanaume anakupenda ni pale akili yake inapofanya maamuzi baada ya kupiga mshindo (post nut clarity)

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Si kila mwanaume anaekwambia anakupenda anamaanisha. Haijalishi kwamba kakufanyia kitu gani iwe kukupa muda wake, kukusaidia, kukupa furaha, kukujali, kukupa pesa, n.k, kuna wanaume ambao huyafanya haya wakiwa bado hawapo timamu.

Kwa mwanaume ambae kamfata mwanamke kwa lengo la starehe huyu anajitambua tayari lakini sasa kuna wanaume ambao wanamfata mwanamke wakiwa na hisia za kimapenzi ila uhalisia ni kwamba akili zao zinafanya maamuzi kwa kiasi kidogo kuuelewa uhalisia wa hisia walizonazo.

Post nut clarity ni muda baada ya mwanaume kufika mshindo, hapa ndipo akili inakuwa imekaa sawa sasa fully functional, hapa ni kama vile furaha ya pombe imeisha na mtu kajirudi katika hali halisi, akili inaanza kutathmini na kupembua hadhi, tabia, uzuri, mapenzi na vitu vingine juu ya huyo mwanamke kama vinaendana na hali ya mwanaume pindi akili imejirudi, na ndio hapa wanaume wengi hujikuta wakijilaumu kwa walichofanya kwasababu mwanamke sio type yake.

Kwako mwanamke kama ukitaka kutambua mwanaume alikuwa katika akili yake sawa na kila alichofanya alimaanisha kwako basi msubiri apige mshindo au mishindo yake ya kumrudisha barabara kuu kichwani. Ukiona bado ana interest na wewe tena kwa dhati bila kujilazimisha basi jua huyo alikupenda kweli, ila ukiona mapenzi yameanza kuwa ya kulazimisha, mawasiliano yamepungua, anakutafuta tu siku za kusex, n.k basi jua huyo alikuwa na wenge tu.
 
Back
Top Bottom