Kwenu Wanawake, upo tayari kuwa na mwanaume uliyemzidi umri?

Kwenu Wanawake, upo tayari kuwa na mwanaume uliyemzidi umri?

mshamba_hachekwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2023
Posts
20,704
Reaction score
66,337
Maisha yangu yote, toka naanza kujitambua mpaka sasa, nimekua nikivutiwa sana na wanawake walionizidi umri. Sijui ni kwanini au ni kivipi nimekua na hii tabia.

Nilichokua nakifanya ni kupuuzia na kukandamiza hisia zangu, ikitokea nimempenda binti aliyenizidi umri, basi nafanya kumpotezea ama kumkwepa kadri niwezavyo.

Niliwahi kumpata binti mmoja kwa kumdanganya umri, ila ilinitokea puani vibaya mno.

Lakini hivi karibuni nimeanza kuona kama najitesa sana kwa kuzuia hisia zangu. Nataka sasa nijaribu bahati yangu.

Swali kwenu wadada, je unaweza kua na mwanaume uliyemzidi umri, tuseme kuanzia mwaka 1 hadi miaka 10?

Unalichukuliaje swala hili? haiwezekani kabisa au ni ushamba wangu tu?

Nahitaji mawazo yenu dada zangu na shangazi zangu.

NB: wanaume pia mnaruhusiwa kuchangia kama una cha muhimu au ushauri.

To yeye
Leejay49
Demi
Aaliyyah
Kelsea
Lenie
Depal
Lovie Lady
Darlin
Ms eyes
Dahan
cocastic
Cute Wife
Bushmamy
Joanah
Joannah
Dejane
Palina
Kapeace
Cienna
Tinsley
Bantu Lady
 
Yaani mimi niwe na kavulana ka 30s Yr? Ohh nope. Labda nikaajiri kachekeshaji kangu
To be honest, siwezi date na mtu hata ambaye tunalingana umri,, napenda my man awe amezidi walau kuanzia miaka 5 hivi hadi 10..tofauti na hapo better niendlee kua single 😌😌
hata kama ni mdogo anaweza akawa anajitambua, ana tabia za kiutu uzima

hapo vipi....
 
Back
Top Bottom