Kwenu wasanii wa Tanzania: Uchaguzi ukiisha kila mmoja akale alipopeleka mboga

Kwenu wasanii wa Tanzania: Uchaguzi ukiisha kila mmoja akale alipopeleka mboga

Wale wa Bongo Muvi miaka michache iliyopita eti walimshawishi yule mwenzao BASHITE kwenda kufanya msako Kariakoo na kufunga vibanda vya wale wajasiriamali wanaouza Dvd za muvi za nje zikiwemo zile za Kikorea!

Yaani mimi na akili zangu niwaangalie Bongo Muvi ambao hawajitambui kwa lolote! Muvi zao ni za hovyo! Hazina mpangilio wowote ule zaidi tu ya kupiga makelele! Uigizaji mbovu na kiwango cha chini kabisa!

Wacha niendelee tu kuwaangalia jamaa zangu wa South Korea. No way out. Na hao wasanii wa Bongo fleva nitaendelea tu kuwadharau maana ninatambua yote hiyo ni njaa tu. Hakuna lingine.
 
Okey mimi kama Msanii nimeelewa ila acha kwanza kipindi hiki tupige hela kwanza, baadaye tutajuana huko juu kwa juu🤦😁🤪
 
Kwanza mambo ya bongo fleva bongo movie ndy ya nafanya Watoto wetu wadumae akili.

Sahivi nguvu nyingi imekuwa invested huko. Kila Aina mtu, Watoto akili zao ziko kibongo fleva fleva.

Kuhusu wasanii Kuingia kwenye kupigia kampeni CCM mm naona ni njaa zao!

Kwanza huwa najiuliza Hawa wasanii Wana impact gani kwa jamii Wana rudisha nn pia kwa jamii, zaidi ya madharau tu.

Ova
Utasikia wasanii wakisema eti sisi wasanii ni kioo cha jamii na tunaelimisha jamii.Ukijiuliza wanaelimisha nini wakati wao wenyewe hawana elimu.Wanapigana miti hovyo hovyo bila kujali maadili wanatumia shisha pombe,mirungi na hatimae wemgine hufa au kuumwa mfano feruzi ,ngwair nk
 
Kwenu wasanii wa Tanzania na Bongo Fleva. Sisi Watanzania wengine tusiopendezwa na mambo ya Chama cha Mapinduzi tumeona mwenendo wenu. Tumeona hakuna shida kwa mujibu wa katiba, mko sahihi.

Siasa zinapita. Sanaa yenu naamini mtapenda ibaki ikipendwa na sisi Watanzania wote.

Wazungu husema;

Scrach my back and I will scrach yours:

Msiige ya USA kina Jay Z; wenzetu wako mbali kidemokrasia sana. Hata aingie nani sanaa yake haitapigwa pini kama ataenda kinyume na INCUMBENT, yaani kiongozi alieko madarakani.

Tunawashukuru sana wanamuziki ambao mmeamua kuwa upande wa CCM, ni Uhuru wenu, ila uchaguzi ukiisha kila mtu akale alipopeleka mboga.

Asanteni.
Na kazi au nyimbo zao wakaziimbe Dodoma
 
Back
Top Bottom