Nilifiwa na ndugu yangu dar, msiba ukaletwa mkoani kwetu kuzikwa kijijini. Pale kijijini hatuna nyumba ila shamba tu ambako huwa tunazika wanafamilia. Jirani na eneo letu kuna vijumba vya slope vimechakaa japo majirani wanaishi ndani ya vijumba hivyo. Wasindikiza msiba toka dar na kwingine walianza kukandia eti inakuwaje marehemu alijenga jumba la kifahari dar lakini nyumbani kwao asijenge hata kibanda cha kufikia? Wasindikiza wafiwa walianza kuhusisha vijumba vile kuwa ndio nyumbani kwa marehemu ikabidi tuwaambie hapa tulihama kitambo sana enzi tukiwa wadogo na tuna mpango wa kujenga nyumba ya maana hapa ili tuwe na pa kufikia tukitoka mikoani kunako mishe zetu. Wasindikiza wafiwa wana tabia ya kuchunguza nyumbani kwao na marehemu kuna nini cha maana walinganishe na huko dar alivyonavyo