Kwenu wataalamu, ni upi uzuri wa gari hii aina ya Probox?

Sio Mkurya Mkuu.

Nashukuru kwa maelezo yako muhimu sana,itoshe kusema nimepata ushawishi wa kutosha
 
Vipi Mkuu,zina mfanano?
Toyota Probox na Toyota succeed kimuonekana zinafanana kila kitu.
Ni few technical specification (mambo ya kiufundi) ndio zinatofautiano.

Zote ni gari nzuri kwa misoto ya mjini na rough road, japokuwa Toyota succeed inaonekana ni vumilivu zaidi kwa mishe mishe za rough road.

All in all, bei zake ni sawa (milioni 12-14 inaagiza toka Japan), japokuwa Toyota succeed inaweza kuwa adimu kidogo.
 
Shukran boss kwa maelezo mazuri sana.
 
Gari za namna hii (Probox/Succeed) ndio zimekuwa mbadala wa zile gari za zamani wazee wa kichaga walizokuwa wanazipenda (Toyota stout, Peugeot, Land Rover aka mando!). Yaani zilikuwa ndio gari zao za mitoko (kanisani, mjini, sherehe nk), gari zao za shambani (atabebea pumba, mashudu, majani, maziwa, mayai, mahindi) na ndio gari hizo hizo za mishe mishe (kuvushia mizigo yao mipakani, kuanzia bia, mafuta ya kula, bidhaa za dukani), nyingi zilikuwa hazina four wheel lakini zinakamua kuliko gari za four wheel za kisasa.
 
Watu wanamwaga sifa lukuki,ukija nunua siku utashangazwa itakapokuzingua ikiwa ni miezi 2 tuko uinunue
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…