Kwenu wataalamu, ni upi uzuri wa gari hii aina ya Probox?

Kwenu wataalamu, ni upi uzuri wa gari hii aina ya Probox?

kazi NA sala

Wewe ni mkurya? Maana hizo gari na wakurya. Ni sawa na mchagga na pesa.

Huna haja ya kuuliza mara mbili kuhusiana na hilo gari.

Kwa kifupi, Probox ni Peugeot 504 of our time.

Hiyo utatumia hadi uiache, ukishindwa hiyo basi jua hakuna gari utaweza kuimudu tena.
Sio Mkurya Mkuu.

Nashukuru kwa maelezo yako muhimu sana,itoshe kusema nimepata ushawishi wa kutosha
 
Vipi Mkuu,zina mfanano?
Toyota Probox na Toyota succeed kimuonekana zinafanana kila kitu.
Ni few technical specification (mambo ya kiufundi) ndio zinatofautiano.

Zote ni gari nzuri kwa misoto ya mjini na rough road, japokuwa Toyota succeed inaonekana ni vumilivu zaidi kwa mishe mishe za rough road.

All in all, bei zake ni sawa (milioni 12-14 inaagiza toka Japan), japokuwa Toyota succeed inaweza kuwa adimu kidogo.
 
Shukran boss kwa maelezo mazuri sana.
 
Herushingo
Screenshot_20210217-081756_Gallery.jpg
 
Gari za namna hii (Probox/Succeed) ndio zimekuwa mbadala wa zile gari za zamani wazee wa kichaga walizokuwa wanazipenda (Toyota stout, Peugeot, Land Rover aka mando!). Yaani zilikuwa ndio gari zao za mitoko (kanisani, mjini, sherehe nk), gari zao za shambani (atabebea pumba, mashudu, majani, maziwa, mayai, mahindi) na ndio gari hizo hizo za mishe mishe (kuvushia mizigo yao mipakani, kuanzia bia, mafuta ya kula, bidhaa za dukani), nyingi zilikuwa hazina four wheel lakini zinakamua kuliko gari za four wheel za kisasa.
 
Watu wanamwaga sifa lukuki,ukija nunua siku utashangazwa itakapokuzingua ikiwa ni miezi 2 tuko uinunue
 
Back
Top Bottom