Binafsi naona sio biashara, mfano ukimiliki viti pamoja na vitu vingine vya harusini ili uwe unavikodisha, inabidi mfumo wako wa maisha ubadilike kisha uwe mtu wa kukesha kwenye kumbi za sherehe maana bila hivyo hawakodi vyombo vyako.
Pia kuna hawa wamama wa kamati, hawa ndiyo wabaya sana maana wao ndio wanapanga bajeti na wana watu wao maalumu kwa ajili ya kuwakodisha vyombo hivyo kwa beo mseleleko.
Wanajua kabisa kuwa kukodisha vyombo fulani bei ni kadhaa ila wamama wachache kati ya wale waliopo ktk hicho kikundi cha bajeti wanakuja na bei yao, labda kukodi muziki 150,000 sasa wao wanakuja na nusu yake au robo tatu.
Mwamba unapiga hesabu unaona hailipi ila kwa kuwa mpo wengi wenye muziki inabidi ukubali ivo ivo kupiga muziki kwa bei ya HASARA.
Hayo ni machache kati ya mengi ambayo utakutana nayo huko.