Sun Zu
JF-Expert Member
- Mar 16, 2022
- 636
- 1,819
Nakumbuka alikuwa ni RPC wa Geita siyo Mwanza.RPC Mwanza aligomea kuibeba CCM Nyamagana enzi za Masha. Matokeo alirudishwa Dar kusimamia magwaride ya ffu.
Nafikiri hapa tatizo siyo la mtu mmoja mmoja kwenye hii taasisi, tatizo ni mfumo.
Tukisema ni mtu mmoja mmoja tunakosea. RPC huyu atakataa maelekezo ya CCM atatolewa atapelekwa huko madongo kuinama atawekwa mwingine pro-CCM.
IGP huyu atagomea maelekezo ya CCM atatolewa atateuliwa mwingine pro-CCM pro-uovu.
OCD huyu atasimamia sheria kanuni na taratibu ataonekana hafuati maelekezo ya CCM atatolewa atapelekwa hukoo madongo kuinama atawekwa mwingine Pro-CCM pro-uovu.
So cha kufanya ni kubadilisha mfumo mzima wa hili jeshi ili liweze kuwa huru lifanye kazi kwa weledi.
Pole sana mzee Sirro