Kwenye historia hakuna mabadiliko yaliyoletwa kwa kulalamika

Kwenye historia hakuna mabadiliko yaliyoletwa kwa kulalamika

MURUSI

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2013
Posts
4,537
Reaction score
8,824
Hii nchi inaweza kuwa inaongoza kuwa na raia wanao lalamika na hakuna hatua wanayo chukua. Napitia sana vitabu mbalimbali vya kimageuzi duniani, sijaona nchi ambayo baada ya malalamiko ya muda mrefu kuna mageuzi yalifanyika. Kwa kifupi malalamiko ni kele za chura, haziwezi zuia ng'ombe kunywa maji kamwe.

Kwa sasa karibia raia wanasahau gharama ya bando, wamehamia kulalamika makato ya benki ambako nako baada ya wiki watapoa na litakuja swala jingine tena. Nchi imejaa wajinga na walalamishi tupu, huwezi kutofautisha wanaume na wanawake, wote wako sawa.

Endeleeni kulalamika, hii ni furaha kwa watawala. Wanapo kaa vikoa vyao huwa kabla ya jambo wanaulizana je, wanachi watafanyaje? Jibu wanaambiwa, wale watalalamika sana baadae watanyamaza. Hakuna jambo zuri kama watawala kujua wanaongoza watu wa aina gani. Nchi zingine huwa hazitabiriki sababu muda wowote raia wanalianzisha, Iia bongo inajulikana, tutalalamika baadaye kimya.

Republic ya walalmishi bila action.
 
Hehe wanakwambia ipo siku watu watachoka kulalamika, hio siku wanaingoja kila siku.......jamhuri ya watu wa Keyboard warriors
 
Hehe wanakwambia ipo siku watu watachoka kulalamika, hio siku wanaingoja kila siku.......jamhuri ya watu wa Keyboard warriors
Wapi hawa Raia, hawa? Hio ni kuhakikishia haitakaaa itokeee kamwe, haitakaaa itokeee
 
Back
Top Bottom