P h a r a o h
JF-Expert Member
- Mar 25, 2024
- 785
- 1,413
Ushahidi unaonyesha kuwa alichangia kwa kiasi kikubwa katika nadharia ( theory ) za Einsten.
Lakini hakuwahi kupewa sifa yoyote.
Alikuwa mwanahisabati na mwanafizikia mahiri. Wawili hao walikutana katika Taasisi ya Polytechnic Zurich.
Tofauti na Einstein, yeye alilazimika kupambana na kupata ruhusa maalum ili kuhudhuria masomo.
Chuoni, alipata alama za juu zaidi kuliko Einstein. Kwenye applied physics, alipata alama ya juu kabisa ya 5, huku Einstein akipata alama ya 1 pekee.
Mnamo 13 Desemba 1900, walituma makala yao ya kwanza kuhusu Capillarity (kapilari), lakini ilisainiwa kwa jina la Einstein pekee, kwa kuwa kazi zao zisingechapishwa zikiwa na jina la mwanamke.
Nakala nyingi za mihadhara yake (lectures)zimeandikwa kwa mwandiko wa Mitza. na Einstein aliwahi kusikika akisema kwenye sherehe, "Namuhitaji mke wangu; hunisaidia kutatua matatizo yangu yote ya hisabati."
Asilimia 80 ya kazi maarufu za Einstein zilichapishwa wakati wa ndoa hii, kipindi kinachojulikana kama miaka yake ya maajabu.
Miaka hiyo ya maajabu ilimalizika ghafla baada ya talaka yao kutokana na usaliti na kuachwa kwake.
soma zaidi:MIT Press Bookstore