Kwenye Mahakama za Haki, Serikali dhalimu haziwezi kutoboa

Kwenye Mahakama za Haki, Serikali dhalimu haziwezi kutoboa

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Tumezisikia kesi zikiihusisha serikali ya Tanzania.Tumeyasikia madege yakishikiliwa. Hivi serikali yetu inasimamia haki wapi?

1. Angalia hili la kuwafutia watoto wadogo matokeo ya mitihani. Wapi hukumu za jumuiya zinakubalika? Kwa nini hawakuwakamata wahalifu na kuwashughulikia kikamilifu hao?

2. Agiza kitu nje uone mlolongo wa makodi na tozo zenye lengo la kutaifisha tu ulichoagiza. Kutalazimishwa storage charges za ajabu ajabu humo, lengo likiwa upokonywe kiharamia tu hicho ulichoagiza.

3. Anza biashara yoyote. Kodi watakayotaka ni payable in advance na bila kujali utapata faida au la.

4. Ni kwenye lipi serikali ya Tanzania iko kwenye facilitation?Wao ni kwenye kuwakamua watu tu. Serikali hii ni chanzo cha umaskini wa wengi na umaskini uliopo.

5. Angalia ada za shule na vyuo kuona uhalali wa viwango vilivyopo. Nani ana regulate au hata kuwatetea walaji kwenye ya namna hii dhidi ya serikali?

6. Angalia polisi na mahusiano yao na watu. Mizania inawanyeshea vidole kwenye unyang'anyi kutokea kwenye maisha ya watuhumiwa hadi wa mali dhidi ya raia.

7. Angalia sekta za serikali na rushwa. Wapi Pako salama? Ni immigration, NIDA, polisi, TRA, Tanroads au Tanesco?

8. Angalia sheria iliyojiwekea serikali kwa manufaa yake. Mfano, likikamatwa gari na wahamiaji haramu au mali ya magendo au waliyojiainishia wao, serikali watalitaifisha hata kama mwenye nalo hahusiki na kadhia nzima inayogombewa.

9. Magari faini ya dereva inafungamanishwa na mwenye gari hata kama hahusiki na linaloitwa kosa. Lengo likiwa kumlenga zaidi mwenye gari Ili kumpoka chochote kinchowezekana.

10. Gonga mnyama pori. Linganisha na mnyama pori kuathiri watu.

11. Angalia sheria na kanuni za mamlaka zozote za serikali kuwaelekea watu. Mwendo ni mahusiano yasiyokuwa na usawa. Ni ma EFD, ving'amuzi, nk?

12. Nk nk.

Sheria nyingi zimewekwa na serikali kwa manufaa yake pekee dhidi ya watu bila hata ya chembe ya aibu, yote kwa maslahi yake.

Enyi wanasheria ya nini kuyaacha yanayoendelea kana kwamba ni halali? Kulikoni nyie kuendelea kutoa ushirikiano kwao kunako hali kama hizi?

Kulikoni kutokuonyesha jitihada za kutosha za kupatikana mustakabali mwingine ikibidi hata kuwasusia haramu zao?

Tuzitegemee mahakama za nje pekee hadi lini kwenye kusikia neno haki dhidi ya madhwalimu hawa?
 
Uko sawa isipokuwa kwenye suala la kufutiwa matokeo ya mtihani.
Soma vizuri sheria za baraza la mitihani(NECTA) utaelewa jinsi ambavyo baraza lilivyo FAIR na TRANSPARENT.
 
Uko sawa isipokuwa kwenye suala la kufutiwa matokeo ya mtihani.
Soma vizuri sheria za baraza la mitihani(NECTA) utaelewa jinsi ambavyo baraza lilivyo FAIR na TRANSPARENT.

Yote niliyoandika ni sahihi kwa mujibu wa sheria zao walizoziweka kulinda maslahi yao. Rejea kwenye mada kujiridhisha.

Waliozowea haramu vya kuchinja na wao, wapi na wapi?
 
Matokeo ya haya ni ndege zetu ndio zinapata tabu, kila zikienda nje kwa matengenezo hazirudi, mzungu anazifunga pingu.
 
Matokeo ya haya ni ndege zetu ndio zinapata tabu, kila zikienda nje kwa matengenezo hazirudi, mzungu anazifunga pingu.

Kama nchi tunastahili total system overhaul.
 
Tanzania hakuna sheria Wala mahakama Kuna wahuni tu wanao nufaika na mfumo huu kandamizi kwa wananchi.

"Wajinga nao huwa wazee"
 
Tanzania hakuna sheria Wala mahakama Kuna wahuni tu wanao nufaika na mfumo huu kandamizi kwa wananchi.

"Wajinga nao huwa wazee"

Kesi hii ya CAG Assad, jiwe angekuwapo na majaji hao hao hukumu ingekuwa nyuzi 180 tofauti.
 
Tarehe Saba Nane
Ni siku ya Ukombozi.
Mahakama itoe haki, rudisheni mkataba huu Dubai.
 
Back
Top Bottom