Tatizo kuna watu wanaongelea ukweli halafu wengine wanakasirika na kuanza kujibishana kama watoto
Wengi hawajui wanataka nini kama Taifa
Asubuhi ya leo nilikuwa nasikiliza speech ya Joe Biden kwa kweli imegusa maslahi ya nchi tu
Kaongelea maendeleo ya nchi yake tu na vitu wanaongoza kwa mambo mengi
Simpingi Lissu kudai haki yake ila hayo ni private na yeye ni mwanasheria anajua pa kupita
Tunataka mtumambie Sera zenu tu
Biden anasema Mito yao inasafirisha mizigo yenye thamani ya $2B kwa siku yes kwa siku
Na ndio Mito yao Rivers sasa sisi mito yetu hata jeshi halipiti, wakulima hawapitishi mazao yao hata mboga mboga hazisafirishwi kwa njia ya mito
Umwagiliaji ndio tumeanza kuamka
Tumejifungia kwenye Bubble hatutaki watu wa nje kila leo matajiri wakubwa wanatukanwa wakati sisi tumebaki kumuita tajiri wetu Mengi ambae ni marehemu bado tunajisifia tu
Hotuba ya Biden itawafundisha mengi mkiisikia hata kama mtapinga
800,000 Hispanics wameajiriwa kwenye viwanda kwa roho Safi
Na sisi kama hatutaki wakuja wawekeze basi leteni mbinu za kimkakati ili na sisi tuuze bidhaa nje na pia tusiagize vingi kutoka nje badala yake tupambane na kutengeneza ndani ya nchi
Kama wao [emoji631] walivyofanya kwenye Chip za magari na simu
Mwanzo walikuwa wanaagiza kutoka China, Malaysia, Taiwan na South Korea na kufanya bidhaa kuwa juu ila sasa wanatengeneza ndani ya nchi
Kama hatuwezi kitu tujiite vilema tu tusaidiwe kila kitu
Na tuache kusingizia wengine
Vijana wanashangaa kwanini wana umasikini halafu unakuta highly educated