Kwenye mapendekezo 21 ya ripoti ya Kamati ya Professor Osoro, yapi yana ukweli, yapi si ya kweli? Tumeshatekeleza mangapi? Makinikia ilikuwa usanii?

chagu wa malunde , kama huna majibu, subiri wenziyo waje kama wanayo. Maana naona wanasoma tu na kupita kimya kimya wanakuachia mzigo mzito na wewe unaanza ile “fallacy” yenu ya “ad hominem”
 
chagu wa malunde , kama huna majibu, subiri wenziyo waje kama wanayo. Maana naona wanasoma tu na kupita kimya kimya wanakuachia mzigo mzito na wewe unaanza ile “fallacy” yenu ya “ad hominem”
Hakuna mzigo mzito hapo. Kwanza kabisa mimi nilikuja kuweka sawa kuwa walicho sema akina Kawe Alumni na wenzake kuwa Lissu ni msaliti ni kweli,sababu alikuwa anawatetea Accacia waendelee kutunyonya. Na alisema uongo kuwa tukibadili mikatana tutaburuzwa MIGA.
Wewe ukaanza kuleta habari za kishika uchumba. Nikakupa jibu,alafu ukaleta link ambazo sio msaada kwako maana zile zinazungumzia yale madai ya kodi iliyokwepwa toka 1998.
Kwa ufupi mimi nasisitiza Lissu ni msaliti. Maana hakutaka tuwe na kitu kama Twiga minerals Ltd.
 
Hakuna smelter ya makinikia imejengwa.
Makinikia yanasafirishwa kama kawaida kinyume na sheria ya madini ya 2017...
Tulisema humu ile sheria ilitungwa kwa makasiriko na haitekelezeki
Here we are today.
Ila kuna watu wanakwambia tupo vzr.
 
Huu utaratibu mpya wa members kuanzisha threads with just sweeping statements with no reference no proof, inaendelea kushika kasi humu jf, ukiweza kuthibitisha uongo ni upi na propoganda ni zipi, utakuwa umeisaidia sana jf.
P
Humu watu wanaandika hisia tu kama hadithi za kijiweni.
Badala ya kuweka hiyo ripoti na kuanza kuchambua kipengele hadi kipengele.

Akumbuke kuna mambo yapo kwenye ripoti hayakuwekwa hadharani, na majadiliano yalivyo kuwa yanajadiliwa na kubishaniwa au kukubali ndani ya majadiiano mengi yamekuwa siri hivyo hapa tunajadili mambo jujuu tu.
 
Nenda kwenye post ya kwanza! Mbona ripoti ipo hapa? Unadhani tunajadili kitu gani hapa?

Eti juu juu, ndo muje na conclusion makengeza kabisa?
 
Wewe ni Kawe Alumni?

Huwezi hata kutuelezea lolote kuhusu kishika uchumba, eti ukanipa jibu! Jibu gani? Mbona ni simple tu?

Wapi hakutaka tuwe na Twiga minerals? Uongo tu! Weka ushahidi hapa.

Nimeshakuleza ni kwanini hawakuenda MIGA! Kwanini bado makinikia yanaondoka? Kuna mabadiliko kwenye malipo yake tofauti na awali? Ndiyo maana tunauliza kuhusu mapendekezo yaliyofanyiwa kazi.

Ninahisi wewe ni mwanasiasa ambaye ni mpiga debe tu na hauna details za maana zaidi ya porojo tu! Kwasababu vyote kuanzia makinikia hadi issue ya kodi tokea mwaka 1998-2017, na “gold concentrate”, ama makinikia, ripoti ikidai ni trillion 188 na kwenye kodi Ilikuwa ni 103 trillion kwa mujibu wa ripoti ya Professor Osoro.
Yote ni masuala ambayo yamo kwenye ripoti ya Osoro, wewe unasema nazungumzia vitu vya tofauti. Utofauti huo uko wapi? Unaweza kuwaonyesha wasomaji wa JF huo utofauti ulipo?
 
Kuhusu ripoti ya Osoro kutoa hiyo ripoti juu ya kuibiwa kodi tril 103 na tril 188 kutoka kwenye uuzwaji wa Copper concetrate hiyo ni ishu nyingine.
Na kuhusu wewe kukomaa kuwa mapendekezo ya tume Osoro hayajafanyiwa kazi ni ishu nyingine.
Mimi nipo kwenye ishu uliyoraise juu ya kipara kipya na wenzake kudai kuwa Lissu ni msaliti.
Nasema hivi ni msaliti sababu alitaka kuaminisha umma kuwa hii sio voidable contract. Na alisema kama mkitaka kubadili mkataba na Barrick mtashitakiwa MIGA. Na alisisitiza haiwezekani na madini haya ni mali ya Accacia. Mtu kama huyu sio msaliti? Maana anajua wazi taifa lake linaibiwa ila anawatetea wanaloliibia taifa lake!
Hakuna porojo wala kupiga debe za kisiasa hapa. Wewe unaesema mapendekezo ya tume ya Osoro hayajafanyiwa kazi. Fanya analysis ya pendekezo moja baada ya moja namna ambavyo halijafanyiwa kazi utufahamishe kama una fact.
 
Jibu kuhusu kishika uchumba sijakupa? Sijakuambia kuwa mazungumzo kati ya Accacia na serikali yalikwama na Barrick wakaingilia kati na kusema watatoa bil 700 ili mazungumzo yaendelee? Na Barrick wakainunua Accacia na kuiondoa kama mbia!
Unachotaka kutuambia zile tril 103 za kodi ndio zimegeuzwa kishika uchumba? Au ulianzisha mada bila kufanya tafiti?
 
Kama huu uzi ndio unaishtaki CCM kwa wananchi umeula wa chuya!
 
Unafahamu maana ya kuwa “void”?

Unafahamu neno “clauses” kwenye mikataba?

Tatizo si mumuificha? Kwanini?

Kuhusu kipara kipya, hata yeye mwenyewe si unaona amekuja, akasoma na kutimka bila hoja?
 
Kwahiyo madai kwamba Acacia ilikuwa kampuni ambayo haijasajiliwa, na hivyo kukwepa kodi mlizozitaja za trillion 103. Wakati mnaanza hayo madai, ndo Barrick wakainunuwa, na kulipa hicho kishika uchumba cha 700 billions.

Sasa unabisha kitu gani? Toa maelezo unielimishe.
 
Magamba hawapendi haya mswa;li magumu ukiwatinga sn wanakuteka unapotea.........Mfano waulize zilipo trillion 1.5 uone wanavokukanzaga utasikia polepole alifundisha....mbwa kabisa hawa jamaaa wanaharibu nchi

Professorial Rubish!!!!!
 
"It is professorial rubbish". Said TL.
 
"It is professorial rubbish". Said TL.
Ndo maana hakuna anayekuja hapa na hoja. Wote wametimka! Wanasoma na kusepa! Inaonyesha ni buku saba kweli! 😀 no substance! Blah blah tu!
 
Nimeweka ripoti hapa kwenye post ya kwanza link ipo! Lakini watu wanakuja hapa na kuzunguruka zunguruka tuu!🤦🏾‍♂️
 
Huna hoja kwa ujumla. Ulileta mada kwa hisia tu.
Ripoti nimeweka hapo juu, wewe unazungumzia vitu ambavyo havimo kwenye ripoti.

Pili, kwenye post yangu #2, nimeweka link ambayo Barrick wanaelezea yaliyotokea, pamoja na wataalam wa kwenye soko la dunia wakizungumzia kuhusu hisa na mwelekeo wa kampuni. Pia wameongelea kuhusu mazungumzo ya kampuni na serikali, pamoja na makubaliano yaliyofikiwa. Nenda kasome kwanza ndo uje hapa ukiwa na hoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…