Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kabla hatujaenda mbele zaidi, maana nataka nikujibu fresh tu, lakini kwanza naona kuna pahala tunatakiwa tuwekane sawa!Kuhusu kuwa na madini kwenye makinikia ni swala ambalo halihitaji hata shule. Ndio maana yale makontena yalikuwa yanasafirishwa na Accacia kwa ulinzi mkali. Na sio kwamba kulikuwa na Copper concetrate pekee kama walivyosema. Kulikuwa na madini mengi tu.
Pia usichanganye kishika uchumba na kodi ambayo ndio ilikuwa ni trillions.
Kwa hiyo fuatilia kwa umakini ili utofautishe haya.
Bado nasiditiza Lissu ni msaliti maana alikuwa anasema serikali haiwezi kubadili mikataba ya uchimbaji madini hapa Tanzania. Na alienda mbali na kusema madini haya sio mali ya watanzania tena. Kwa hiyo Kawe Alumni na wenzake walikuwa sawa kumuita msaliti. Maana mikataba imebadilishwa kwa manufaa ya Tanzania.
Baada ya serikali kuzuia makinikia kusafirishwa Accacia walikuwa na mgogoro mkubwa na serikali juu ya kodi ambayo ilikwepwa kulipwa tokea 1998. Na kampuni mama ilingilia haya mazungumzo na ili kuweka mambo sawa ilisema itatoa kishika uchumba bil 700 ili majadiliano yaendelee, sababu Accacia na serikali hawakuwa kwenye good terms. Ndio maaana serikali ikawaambia Barrick wawaondoa Accacia kabisa ili majadialiano yaendelee.Kabla hatujaenda mbele zaidi, maana nataka nikujibu fresh tu, lakini kwanza naona kuna pahala tunatakiwa tuwekane sawa!
Kishika uchumba ilikuwa ni pesa ya nini? Unasema kodi ndo ilikuwa in trillions, hawakulipa hizo pesa, wakalipa kishika uchumba!
Wewe unaelewa kishika uchumba kuwa ni pesa ya nini? Si unajuwa ilitoka baada ya makubaliano? Sasa tulisema kishika uchumba ni pesa ya nini?
maeneo ya chato au?Smelter iko inajengwa geita
Kwahiyo kishika uchumba hakihusiani na makinikia? Huu mchakato hapo chini?Baada ya serikali kuzuia makinikia kusafirishwa Accacia walikuwa na mgogoro mkubwa na serikali juu ya kodi ambayo ilikwepwa kulipwa tokea 1998. Na kampuni mama ilingilia haya mazungumzo na ili kuweka mambo sawa ilisema itatoa kishika uchumba bil 700 ili majadiliano yaendelee, sababu Accacia na serikali hawakuwa kwenye good terms. Ndio maaana serikali ikawaambia Barrick wawaondoa Accacia kabisa ili majadialiano yaendelee.
Kishika uchumba hakihusiani kabisa. Na hata haya makinikia yakiuzwa sasa yanauzwa kama mali ya Twiga minerals ltd.Kwahiyo kishika uchumba hakihusiani na makinikia? Huu mchakato hapo chini?
1. Dhahabu Kamati imebaini kuwepo kwa viwango vingi vya juu vya dhahabu ndani ya makinikia yaliyofanyiwa uchunguzi. Viwango hivyo ni kati ya 671 g/t hadi 2375 g/t, sawa na wastani wa 1400 g/t. Wastani huu ni sawa na 28 kg za dhababu kwenye kontena moja lenye tani 20 za makinikia.
Hivyo, kwenye makontena 277 ya makinikia yaliyozuiliwa Bandari ya Dar es Salaam na Bandari Kavu yatakuwa na wastani wa tani 7.8 za dhahabu yenye thamani ya TZS bilioni 676 (USD 307,292,720).
Aidha, kwa kutumia kiwango cha juu kilichopimwa kwenye kontena moja lenye shehena ya tani 20 za makinikia (47.5 kg), kiasi cha dhahabu katika makontena 277 kitakuwa 13,157.5 kg ambazo thamani yake ni TZS 1,146,860,330,000 (USD 521,300,150).
Hivyo, thamani ya dhahabu katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 676 na bilioni 1,147.
Taarifa tulizopata kutoka kwa wazalishaji pamoja na Wakala wa Serikali wa Ukaguzi Madini (TMAA) zinaonesha kuwa makinikia yana wastani wa takriban 200 g/t. Kiwango hiki ni sawa na kilo 4 za dhababu kwenye kila kontena.
Hivyo, makontena 277 ya makinikia yaliyozuiliwa Bandari ya Dar es Salaam na Bandari Kavu yatakuwa na tani 1.1 za dhahabu. Kiasi hiki cha dhahabu kina thamami ya TZS bilioni 97.5 (USD 44,320,000).
Thamani hii ni ndogo sana ukilinganisha na thamani halisi iliyopatikana katika uchunguzi huu ya kati ya TZS bilioni 676 na bilioni 1,147. Kutokana na tofauti hii kubwa kati ya viwango vya dhahabu vilivyopo kwenye taarifa za usafirishaji na vile ambavyo Kamati imevibaini, ni dhahiri kuwa Taifa linaibiwa sana kupitia usafirishaji wa makinikia nje ya nchi.
2. Pamoja na viwango vikubwa vya dhahabu kwenye makinikia, Kamati ilipima na kupata viwango vikubwa vya madini ya copper (kiwango cha 15.09% hadi 33.78%, wastani wa 26%), silver (kiwango cha 202.7 g/t hadi 351 g/t, wastani wa 305 g/t), sulfur (kiwango cha 16.7% hadi 50.8%, wastani wa 39.0%) na iron (kiwango cha 13.6% hadi 30.6%, wastani wa 27%).
Copper Wastani wa kiwango cha copper kilichopatikana ni tani
5.2 na kiwango cha juu kilichopimwa ni tani 6.75 kwenye kila kontena lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, kiasi cha wastani wa copper kwenye makontena 277 ni tani 1,440.4 ambazo thamani yake ni TZS bilioni 17.9 (USD 8,138,260) na kiasi cha juu ni tani 1,871.4 ambazo zina thamani ya TZS bilioni 23.3 (USD 10,573,478). Hivyo, thamani ya copper katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 17.9 na bilioni 23.3.
Nyaraka za usafirishaji ambazo Kamati ilizipata kutoka bandarini zinaonesha kuwa makinikia yana wastani wa kiwango cha copper cha 20%. Kiwango hiki ni sawa na tani 4 za copper kwenye kila kontena; hivyo makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini yatakuwa na tani 1,108 za copper. Kiasi hiki cha copper kina thamami ya USD 6,204,800 sawa na TZS bilioni 13.6. Kwa takwimu hizi, kwa upande wa copper nako kuna upotevu mkubwa wa mapato ya taifa ukizingatia kuwa usafirishaji wa makinikia nje ya nchi umefanyika kwa muda mrefu.
Silver Wastani wa kiwango cha silver kilichopimwa ni 6.1 kg na kiwango cha juu ni 7 kg kwa kontena lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, kiasi cha wastani wa silver kwenye makontena 277 ni 1,689 kg (tani 1.7) ambazo thamani yake ni TZS bilioni 2.1 (USD 937,446); kiasi cha juu ni 1,939 kg (tani 1.9) ambazo thamani yake ni TZS bilioni 2.4 (USD 1,075,757). Hivyo, thamani ya silver katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 2.1 na bilioni 2.4.
Nyaraka za usafirishaji ambazo Kamati ilizipata kutoka bandarini zinaonesha kuwa makinikia yana silver kwa wastani wa takriban 150 g/t. Kiwango hiki kinamaanisha kuwa kuna 3 kg za silver kwenye kila kontena la tani 20 za makinikia. Kwenye makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini, kiasi cha silver kilichopo kwenye nyaraka za usafirishaji ni 831 kg. Kiasi hiki cha silver kina thamami ya USD 461,039 sawa na TZS bilioni 1.0. Kwa takwimu hizi, kwa upande wa silver nako kuna upotevu mkubwa wa mapato ya taifa.
Sulfur Wastani wa sulfur uliopimwa ni tani 7.8 wakati kiwango cha juu kilikuwa tani 10.2, kwa kontena lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini, yatakuwa na wastani wa tani 2,161 za sulfur, ambazo thamani yake ni TZS bilioni 1.4 (USD 648,130); na kiasi cha juu ni tani 2,825.4 ambazo zina thamani ya TZS bilioni 1.9 (USD 844,296).
Hivyo, thamani ya sulfur katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 1.4 na bilioni 4.9. Thamani hii ya sulfur ni kubwa ukizingatia kuwa haijawahi kutumika kukokotoa mrabaha katika mauzo ya makinikia.
Iron Wastani wa iron uliopimwa ni tani 5.4 wakati kiwango cha juu kilikuwa tani 6.1, kwa kontena lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini yatakuwa na wastani wa tani 1,496 za iron, ambazo thamani yake ni TZS bilioni 2.3 (USD 1,047,060); na kiasi cha juu ni tani 1,695 ambazo zina thamani ya TZS bilioni 2.6 (USD 1,186,668). Hivyo, thamani ya iron katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 2.3 na bilioni 2.6.
Kama ilivyo kwa sulfur, thamani hii ya iron ni kubwa ukizingatia kuwa haijawahi kutumika kukokotoa mrabaha katika mauzo ya makinikia. Hali hii inazidi kuonesha jinsi gani nchi yetu isivyofaidika na uuzwaji wa makinikia nje ya nchi.
3. Uchunguzi pia umeonesha kuwepo kwa madini mkakati (strategic metals) ambayo kwa sasa hivi yanahitajika sana duniani na yana thamani kubwa sambamba na thamani ya dhahabu. Madini hayo ni: iridium, rhodium, ytterbium, beryllium, tantalum na lithium.
Iridium Wastani wa iridium uliopimwa ni 6.4 kg wakati kiwango cha juu ni 13.75 kg kwa kontena lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini, yatakuwa na wastani wa 1,773 kg za iridium, ambazo thamani yake ni TZS bilioni 108 (USD 48,876,096); wakati kiasi cha juu ni 3,808.8 kg ambazo thamani yake ni TZS bilioni 231.0 (USD 105,007, 238). Hivyo, thamani ya iridium katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 108 na bilioni 231.
Rhodium Wastani wa rhodium uliopimwa ni 0.034 kg wakati kiwango cha juu ni 0.078 kg kwa kontena lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini yatakuwa na wastani wa 9.4 kg za rhodium, ambazo thamani yake ni TZS bilioni 0.7 (USD 300,731); wakati kiasi cha juu ni 21.6 kg ambazo thamani yake ni TZS bilioni 1.5 (USD 689,912). Hivyo, thamani ya rhodium katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 0.7 na bilioni 1.5.
Ytterbium Ytterbium ilipatikana kuwa na wastani wa 3.7 kg na kiwango cha juu kilikuwa 4.9 kg kwa kila kontena lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini yatakuwa na wastani wa 1024.9 kg za ytterbium, ambazo thamani yake ni TZS bilioni 12.4 (USD 5,636,950); wakati kiasi cha juu ni 1,357.3 kg ambazo thamani yake ni TZS bilioni 16.4 (USD 7,465,150). Hivyo, thamani ya ytterbium katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 12.4 na bilioni 16.4.
Beryllium Wastani wa kiasi cha beryllium kilichopimwa ni 19.4 kg na kiasi cha juu kilikuwa 26.9 kg kwa kila kontena lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, wastani wa beryllium kwenye makontena 277 ni tani 5.4 zenye thamani ya TZS bilioni 6.0 (USD 2,719,143); na kiwango cha juu kilichopimwa katika makontena 277 ni tani 7.5 ambazo thamani yake ni TZS bilioni 8.3 (USD 3,770,358). Hivyo, thamani ya beryllium katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 6.0 na bilioni 8.3.
Tantalum Tantalum ilipatikana kuwa na wastani wa 11.7 kg na kiwango cha juu kilikuwa 17.3 kg kwa kila kontena lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini yatakuwa na wastani wa 3240.9 kg za tantalum, ambazo thamani yake ni TZS bilioni 1.9 (USD 855,598); wakati kiasi cha juu ni 4,792 kg ambazo thamani yake ni TZS bilioni 2.8 (USD 1,265,114). Hivyo, thamani ya tantalum katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 1.9 na bilioni 2.8.
Lithium Wastani wa kiasi cha lithium kilichopimwa ni 21.5 kg na kiasi cha juu kilikuwa 29.8 kg kwa kila kontena lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, wastani wa lithium kwenye makontena 277 ni 5,955.5 kg zenye thamani ya TZS bilioni 1.0 (USD 468,698); na kiwango cha juu kilichopimwa katika makontena 277 ni 8,254.6 kg ambazo thamani yake ni TZS bilioni 1.4 (USD 649,637). Hivyo, thamani ya lithium katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 1.0 na bilioni 1.4.
Jumla ya thamani ya aina zote za Metali Mkakati katika makontena 277 yaliyoko bandarini ni kati ya TZS bilioni 129.5 na bilioni 261.5. Pamoja na kuwa na thamani kubwa, metali hizi hazikuwa zinajulikana kuwemo kwenye makinikia na hivyo hazijawahi kujumuishwa kwenye kukokotoa mrabaha na hivyo kuikosesha Serikali mapato makubwa kwa kipindi chote cha biashara ya makinikia.
“Newly calculated taxes and royalties, re-negotiations of large scale mineral development agreement”, siyo sawa na kubadili mkataba! Tatizo mnaifanya ni siri ndo maana. Mbona ripoti tunaichambua hapa bila tabu? Bungeni walitakiwa wafanye hiyo kazi. Shida yenu ni chama chenu na siasa zenu kupeleka kina Lusinde mule! Mkiweka ushabiki wa chama mbele za maslahi ya Taifa!Kishika uchumba hakihusiani kabisa. Na hata haya makinikia yakiuzwa sasa yanauzwa kama mali ya Twiga minerals ltd.
Unajadili mambo kwa hisia sana. Nafikiri ili uelewe huu mchakato ulivyo ungesoma sheria zote mpya za madini za mwaka 2017. Na kam sio kubadili mkataba kwa nini serikali ina hisa 16% na economic benefits 50% kwa 50% wakati awali kulikuwa na hakuna hisa? Haya mambo yanatakiwa utulie na ufuatilie kwa ukaribu. Sio kukaririshwa na kuanza kutoa mada bila facts. Mwaka 1998 Barrick walisaini mkataba na serikali mrahaba ulikuwa ni 4% na kulikuwa hakuna hisa hata 1. Leo serikali ina hisa 16% na mrahaba ni 6% unasema hakuna mabadiliko ya mkataba. Why?“Newly calculated taxes and royalties, re-negotiations of large scale mineral development agreement”, siyo sawa na kubadili mkataba! Tatizo mnaifanya ni siri ndo maana. Mbona ripoti tunaichambua hapa bila tabu? Bungeni walitakiwa wafanye hiyo kazi. Shida yenu ni chama chenu na siasa zenu kupeleka kina Lusinde mule! Mkiweka ushabiki wa chama mbele za maslahi ya Taifa!
Katiba inasema wazi kuwa inapokuja kwenye mikataba ya rasilimali zetu, basi wananchi lazima wajuzwe!
Kuuzwa kwa makinikia kuwa ni mali ya Twiga siyo kweli na ni uongo. Kwani kazi ya Twiga ni nini?Labda unazungumzia mambo ya kwenye mkataba ambao wewe umeuona.
Kishika uchumba kinahusiana na nini?
Uongo.chagu wa malunde , Kodi ni trillions 108, na wakati makinikia, ni trillions 188.
Hiyo link ina nini cha maana?Wewe ndiyo muongo. Mimi si nimekuwekea link hapo juu?
Kwa hiyo ndio nini? Kina husiana na kishika uchumba?Maelezo ya kiasi cha kodi toka 1998-2017, ni tzs 103 trillion, pamoja na makinikia tokea mwaka huo wa 1998- 2017, ambapo ni tzs 188 trillion. Hiyo ni kwa mujibu wa madai ya serikali.
Inawezekana yalikuwa kwenye mkataba tayari kama “clauses” pengine hamkujuwa? Ama pia pengine ni kutokana na shida ya upande wetu kuhusiana na mambo ya usajili wa Acacia, ndo maana wakakubali ku re-negotiate.Unajadili mambo kwa hisia sana. Nafikiri ili uelewe huu mchakato ulivyo ungesoma sheria zote mpya za madini za mwaka 2017. Na kam sio kubadili mkataba kwa nini serikali ina hisa 16% na economic benefits 50% kwa 50% wakati awali kulikuwa na hakuna hisa? Haya mambo yanatakiwa utulie na ufuatilie kwa ukaribu. Sio kukaririshwa na kuanza kutoa mada bila facts. Mwaka 1998 Barrick walisaini mkataba na serikali mrahaba ulikuwa ni 4% na kulikuwa hakuna hisa hata 1. Leo serikali ina hisa 16% na mrahaba ni 6% unasema hakuna mabadiliko ya mkataba. Why?
Nimeshakujibu. Labda hutaki kuelewa.Kwani wewe umeshanijibu swali langu?
Nimekuiliza mara ngapi kuwa kishika uchumba ni pesa ya nini? Haujajibu, badala yake unaniuliza tena!🤦🏾♂️
Vitu vingi una raise kwa hisia hauna facts. Jambo ambalo sio jema. Pitia sheria za madini za mwaka 2017. Pia fuatilia huu mgogoro toka unaanza mpaka Twiga minerals inaanzishwa ndio uibue mada. Sio kufanya mambo kwa hisia tu.Inawezekana yalikuwa kwenye mkataba tayari kama “clauses” pengine hamkujuwa? Ama pia pengine ni kutokana na shida ya upande wetu kuhusiana na mambo ya usajili wa Acacia, ndo maana wakakubali ku re-negotiate.
Tatizo mkataba mumeificha, mnatuambia vipande vile vinavyowapendeza nyie na kwasababu za kisiasa tu!
Kumbuka kutokana na ufisadi wa ccm, ndo maana kulikuwepo na shida kwenye kampuni ya Acacia, na ndipo Barrick wakainunuwa.
Wewe kwani umeweka facts gani hapa? Kuna ambacho nazungumzia na sijaweka facts zilizopo na ushahidi wa links kama unataka kujiridhisha?Vitu vingi una raise kwa hisia hauna facts. Jambo ambalo sio jema. Pitia sheria za madini za mwaka 2017. Pia fuatilia huu mgogoro toka unaanza mpaka Twiga minerals inaanzishwa ndio uibue mada. Sio kufanya mambo kwa hisia tu.