Msukuma Original
JF-Expert Member
- Oct 2, 2018
- 928
- 3,330
Napenda kuwajulisha wapinzani wa kweli kuwa nimefanya utafiti wangu usio rasmi. Nimejaribu kupita Facebook, tweeter, Instagram na humu JF na kwenye vyombo vya usafiri nakugundua kwamba wananchi wengi walio upande wa upinzani hawakubaliani na ujio wa Membe.
Hoja yao ya msingi ni kwamba Membe amekuja upinzani baada ya kufukuzwa, maana yake asingefukuzwa angekuwa bado mwana CCM. Kwa mantiki hiyo wananchi wanaona kwamba hana mapenzi na upinzani isipokuwa matatizo yake na chama chake cha awali ndio kimefanya aje upinzani.
Angekuwa anaupenda upinzani angeondoka kabla ya kufukuzwa kama ilivyokuwa kwa Lazaro Nyalandu. Ni sawa sawa na mtu na mpenzi wake wanakwaruzana ndio anaamua kumuacha na kwenda kwa bwana mwingine. Angekuwa anampenda huyo bwana mpya angemfuata kabla ya kugombana na mpenzi wake wa zamani.
Maana yake ni kwamba mpenzi mpya kapata mwenza baada ya mpenzi wake kukorofishana na bwana ake. Siku wakipigiana simu na kuweka tofauti zao pembeni mahaba yatarudi kama zamani na mpenzi mpya ataachwa kwenye mataa.
Napenda kuhitimisha kwa kusema kwamba upinzani wasimsimamishe Membe, wananchi wenye mapenzi ya dhati na upinzani hawamtaki Membe. Bora Nyalandu mara 100 kama Lissu atashindwa kurudi nchini au kama ataletewa mizengwe na mamlaka za Kiserikali.