Uchaguzi 2020 Kwenye mitandao ya kijamii na mtaani, Membe hakubaliki

Uchaguzi 2020 Kwenye mitandao ya kijamii na mtaani, Membe hakubaliki

Ulichokiandika kinafurahisha na kuwapa amani ya matarijio mema na furaha ya muda wafuasi wa upinzani, hasa ujio wake Membe.

Niko mikoani kwa shughuli zangu, tena vijijini, na hata kwao Membe nimepita, wimbo ni Magufuli tu, kuanzia watoto hadi wazee. Hakuna asiyemjua Magufuli kwa sababu ndiye anahusishwa na elimu bure, madawati, barabara zinazopitika majira yote, zahanati, wakulima kutokusumbuliwa wakati wa kusafirisha na kuuza mazao yao, machinga kufanya biashara zao kwa amani bila buguhuza, na kadhalika.

Kuishi kwa matumsini huongeza siku za maisha, bila shaka

Upo kijiji gani wewe? , vijiji ninavyovijua mimi wanalia kuhusu korosho, kahawa, ufuta, mbaazi, alizeti kote huko wanalaumu serikali ya Magufuli kwa kuwasababishia njaa

Wamachinga wanalaani kutozwa shilingi 20000 pesa ambazo siyo kodi za TRA wala za Manispaa bali ni amri ya Magufuli tu.

Wamachinga wanalia biashara zao nibovu, wateja wenye kunua bidhaa zao wamepungua sana kwa sababu Magufuli kawatia umasikini wananchi wengi, purchasing power yao imeshuka mno.

Kwenye Elimu bure tena huko. ndo usiseme maana michango kibao inaendelea huko, kuna maeneo watu wanaambiwa waende na madawati ya watoto wao, hiyo ni elimu bure ipi wakati michango ipo kwa mlango wa nyuma.

Zahanati nyingi dawa za msingi na vifaa kama vile gloveszi raia wanaandikiwa wakanunue mitaani na huko ni bei ghali.

Unazungumzia madawati wakati tunaona watoto katika sehemu mbalimbali za nchi bado wanakaa chini, na wanafanyia mitihani chini

Ukichanganya na hasira za watumishi wa umma na wafanyabiashara ambao TRA imevuruga biashara zao sioni ni kitu gani Magufuli ataenda kuwaambia wananchi.

Ana wakati mgumu sana kushinda uchaguzi!
 
Ulichokiandika kinafurahisha na kuwapa amani ya matarijio mema na furaha ya muda wafuasi wa upinzani, hasa ujio wake Membe.

Niko mikoani kwa shughuli zangu, tena vijijini, na hata kwao Membe nimepita, wimbo ni Magufuli tu, kuanzia watoto hadi wazee. Hakuna asiyemjua Magufuli kwa sababu ndiye anahusishwa na elimu bure, madawati, barabara zinazopitika majira yote, zahanati, wakulima kutokusumbuliwa wakati wa kusafirisha na kuuza mazao yao, machinga kufanya biashara zao kwa amani bila buguhuza, na kadhalika.

Kuishi kwa matumsini huongeza siku za maisha, bila shaka
Kwani kwenu ni wapi? au ndio huku huku kwetu?
1595064957894.png
 
Kama hakubaliki, mbona umeacha kazi zako zote unamjadili.
 
Hahaha mpaka sasa kampeni hazijaruhusiwa, uchaguzi October, Magufuli, ccm na serikali macho yao yote yako CHADEMA kwa Tanzania bara, kule visiwani macho yao yako ACT.

Wao ccm wanafahamu hawategemei kura kushinda bali tume na vyombo vya ulinzi vyote.

Nyie mnajadili ushindi wa kura wao huko hawajali, wanaogopa mtu anayejua kuzungumza, na huyu mtu ni LISU.

Lakini angaluzo kuhusu Tundu Lisu hawezi kuruhusiwa kuingia nchini hadi awe mgombea, anazo kesi za uchochezi hazijaisha, anatafutwa kwa kosa la kujipiga risasi wasemavyo ccm na serikali yao, wanamtafuta kwa kesi za usaliti kwa taifa, yani yule akifika tu anadakwa moja kwa moja segerea, mtakaa kimya kama waislamu wa uamsho na sasa sheikh Ponda, mtasahau Lisu ni nani na hatoki ng'o kwa dhamana maana wanasababu eti ame ruka au kuvunja misingi ya dhamana kwa kesi zingine nazo watamuweka mahabusu mpaka kesi ziishe.

Hivyo Lisu hata msimjadili hapa mnapoteza muda kwa serikali hii, ccm hii na Magufuli huyu watamuweka ndani tu,na wanajua hamna cha kuwafanya.

Keep my word, mtakuja kubadilisha mjadala humu.
 
Hivi yule Chief Lutayosa Yemba hagombei 2020? Maana namkumbuja Jaji Mark Bomani 2015 alivyokuwa anamtamka jina kwa mikogo
 
Siasa ni mchezo, na mwenye kucheza vizuri ndiyo mshindi, na nchi haikabidhiwi kwa watu wa aina ya Lissu. nchi inakabidhiwa kwa watu waliopitia kwenye tanuri la system na kuaminiwa kwamba wanaweza kulinda maslahi ya nchi.

Kwenye uchaguzi wowote lazima nchi iwe na alternative. 2015 alternative president alikuwa Lowassa, this time alternative President ni Membe incase ikatokea Magu ambaye ndiye first choice akashindwa. Hiyo ndiyo michezo ya siasa kwa wasiojua.

Mwambieni tu Lissu huko aliko, hawezi kukabidhiwa nchi. wenye mapovu ruksa kutoa povu
 
Mnanichekesha sana mnaposema leo hii Lowasa aliwaingiza kingi!

Kwahiyo mlipokuwa mnaambiwa mlifikiri mnaonewa wivu au?
Mzee

Tulivuna vya kutosha...

Infact tulipata zaidi na zaidi

Tunachokichukia ni yeye kuondoka jinsi alivyoondoka na kukutolea maneno machafu

Ila hesabu za namba and etc,tuli-win big time...

With Membe coming,kwa numbers hakuna kitu maana hajafikia 1/4 ya Lowassa's population..Kaja na numbers ndogo sana,and still,atakuja kuondoka kijinga kama alivyoondoka Lowassa...

Lowassa alikuja inevitably,na his oust ilikua sponteneous,na alikuja na mafuriko..sio huyu anakuja kama yeye

Kwa kifupi Membe hana faida kama ile faida ya Lowassa back in that time.

Ndio maana amekaushiwa kama alivyo....ACT haina cha kupoteza to begin with!

Na the big boy CDM wont buy that Membe shit maana ni liability!
 
Utafiti wako ulitumia methodolijia gani?

Membe anakubalika sana, nimefanya utafiti binafsi juu ya hilo!

Wewe umeuliza wakulima wangapi, wafanyakazi wangapi, wanawake wangapi, wanaume wangapi, umeuliza vijana wangapi, wazee wangapi, umeuliza watu mikoa ipi.

Yote haya lazima uzingatie ili kupata sampuli inayowakilisha picha ya umma.

Umma utazidi kumpenda na kumkubali Membe kwa sababu maono yake ni yaleyale ambayo wananchi majority wamekuwa wakilia na kusaga meno katika utawala huu mfano maslahi ya wafanyakazi, maslahi ya watumishi wa vyombo vya usalama, Ajira kwa vijana, Maslahi ya wakulima, Katiba mpya iliyo bora, etc

Mimi utafiti wangu binafsi unaonyesha Membe anakubalika kuliko Magufuli na kukubalika huku kutaendelea kila siku baada ya kampeni kuanza.

Kama kukiwa na uchaguzi huru na haki Magufuli ajiandae kukabidhi Ikulu kwa Membe au Lissu
Na mimi utafiti nilioufanya inaonesha kuna mkakati wa makusudi wa kumuanda Membe ili ashindane na JPM kwa kumwagia sifa tele tele ili ashindwe na waompigia debe wengi wa ni ccm wanaamini Membe ni mwepesi kuliko Lissu na wanajua iwapo Lissu atasimama shughuli itakuwa ngumu zaidi historia inaonyesha kila alietoka ccm kwa ajili ya kutaka urais mwisho wa siku hakini Nyalandu kwakuwa alipotoka ccm urais haukuwa dhamira yake mpaka leo bado yupo na hajaonesha kungangania urais
 
Na mimi utafiti nilioufanya inaonesha kuna mkakati wa makusudi wa kumuanda Membe ili ashindane na JPM kwa kumwagia sifa tele tele ili ashindwe na waompigia debe wengi wa ni ccm wanaamini Membe ni mwepesi kuliko Lissu na wanajua iwapo Lissu atasimama shughuli itakuwa ngumu zaidi historia inaonyesha kila alietoka ccm kwa ajili ya kutaka urais mwisho wa siku hakini Nyalandu kwakuwa alipotoka ccm urais haukuwa dhamira yake mpaka leo bado yupo na hajaonesha kungangania urais
JPM, akiwa hana nguvu kisiasa, aliwashinda waliokuwa na nguvu kisiasa, ikiwemo huyo Membe. Ni ndoto leo atokee wa kumshinda wakati tayari amekonga mioyo ya wapiga kura (hasa vijijini - 70% ya wapiga kura) kwa utendaji wake wa kazi usio na mfano Tanzania, Afrika Mashariki na dunia nzima. Asilimia 30% iliyobaki ni ya wakosoaji wake na wafuasi wao, kama ifuatavyo:-

Wanaomkosoa ni wanasiasa uchwara, mabingwa wa siasa za majukwaani, ambao baada ya kuzuiwa kufanya hivyo wamehamia kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii wakimpachika sifa ya dikteta uchwara. Hawa wanadai Tume Huru ya Uchaguzi kwa sababu hawana hoja ya maendeleo ya kushawishi wapiga kura, ili waitumie kama sababu ya kushindwa vibaya kwenye Uchaguzi Mkuu ujao.

Wengine wanaomkosoa ni kundi la mafisadi, wafanyabiashara wakwepa kodi, na waliogeuza nchi tajiri kuwa shamba la bibi. Pasipo kumung'unya maneno, kundi hili limeathirika kiasi kwamba nguvu yao ya kiuchumi/kifedha kwa sasa haina madhara makubwa kama kwenye chaguzi zilizopita.

Kundi lingine ni la vijana wa "mishemishe au misheni town" ambao ni bendera fuata upepo. Wakipewa chochote wako tayari kumfanyia lolote atakalotaka au kuagiza huyo mtu wao kama ilivyotokea Uchaguzi Mkuu 2015, walizungusha mikono ati ndiyo mabadiliko, wengine walipiga deki barabara, na wengine walibadilishiwa gia angani na bahati mbaya chombo kikaanguka ardhini, pu!

WAPIGA KURA WAMESIKIA NA WAMEONA TANZANIA INAVYOBADILIKA KUTOKANA NA JUHUDI BINAFSI ZA JPM
 
Ni ndoto leo atokee wa kumshinda wakati tayari amekonga mioyo ya wapiga kura (hasa vijijini - 70% ya wapiga kura) kwa utendaji wake wa kazi usio na mfano Tanzania, Afrika Mashariki na dunia nzima
Nakala ya utafiti ulioufanya please
 
Show ya Zuchu ilikuwa Kali hatari,yaaani Jana nimemuona membe act Ila hii ya mwaka huu lissu anabeba magufuli yeye na simba tu.
 
Back
Top Bottom