Ad majorem
JF-Expert Member
- Aug 11, 2018
- 939
- 1,460
Napenda kuwajulisha wapinzani wa kweli kuwa nimefanya utafiti wangu usio rasmi. Nimejaribu kupita Facebook, tweeter, Instagram na humu JF na kwenye vyombo vya usafiri nakugundua kwamba wananchi wengi walio upande wa upinzani hawakubaliani na ujio wa Membe.
Hoja yao ya msingi ni kwamba Membe amekuja upinzani baada ya kufukuzwa, maana yake asingefukuzwa angekuwa bado mwana CCM. Kwa mantiki hiyo wananchi wanaona kwamba hana mapenzi na upinzani isipokuwa matatizo yake na chama chake cha awali ndio kimefanya aje upinzani.
Angekuwa anaupenda upinzani angeondoka kabla ya kufukuzwa kama ilivyokuwa kwa Lazaro Nyalandu. Ni sawa sawa na mtu na mpenzi wake wanakwaruzana ndio anaamua kumuacha na kwenda kwa bwana mwingine. Angekuwa anampenda huyo bwana mpya angemfuata kabla ya kugombana na mpenzi wake wa zamani.
Maana yake ni kwamba mpenzi mpya kapata mwenza baada ya mpenzi wake kukorofishana na bwana ake. Siku wakipigiana simu na kuweka tofauti zao pembeni mahaba yatarudi kama zamani na mpenzi mpya ataachwa kwenye mataa.
Napenda kuhitimisha kwa kusema kwamba upinzani wasimsimamishe Membe, wananchi wenye mapenzi ya dhati na upinzani hawamtaki Membe. Bora Nyalandu mara 100 kama Lissu atashindwa kurudi nchini au kama ataletewa mizengwe na mamlaka za Kiserikali.
Pamoja na vyama vya upinzani kusimamisha makada wa CCM tutarajie watakaotewa CCM kuhama na kujiunga na vyama visivyo na wagombea wenye sifa. Ikiwa hivyo, hakuna ubishi kuwa CCM ni chama dumeKwa hali ilivyo Sasa, huenda CCM wakasimamisha Wagombea watatu wa ngazi ya Urais kupitia vyam vitatu tofauti, katika uchaguzi mkuu mwaka huu. Wagombea hao watakuwa Comrade JPM, Comrade ambae wengine mnamuita Kamanda Nyalanduna na Comrade Mzalendo Membe. Ukizingatia kuwa, TLP na UDP wameshatangaza kumuunga mkono Mh. Jpm, huenda CHAUMA NA NLD wakamuunga mkono Nyarandu, na kufikisha vyama sita ambavyo vitakuwa vikifanya kampeni kwa niaba ya CCM. Kwa hesabu hiyo ya Std 4, wacha CCM waendelee kutusomesha namba za kirumi maana viongoz wa tunavyoviita vyama vyetu vya upinzani ama hawajielewi au hawana nia ya dhati ya kumkomboa Mtanzania.
Lissu anakubalika sana hilo sina ubishi,
Isipokuwa kama Membe akisimama na Magufuli, Magufuli anapigwa asubuhi na mapema.
Watu wana hasira na utawala wa Magufuli zaidi kuliko kutomjua Membe.
Nyalandu huyo anashika mkia kwenye kukubalika!
Upo kijiji gani wewe? , vijiji ninavyovijua mimi wanalia kuhusu korosho, kahawa, ufuta, mbaazi, alizeti kote huko wanalaumu serikali ya Magufuli kwa kuwasababishia njaa
Wamachinga wanalaani kutozwa shilingi 20000 pesa ambazo siyo kodi za TRA wala za Manispaa bali ni amri ya Magufuli tu.
Wamachinga wanalia biashara zao nibovu, wateja wenye kunua bidhaa zao wamepungua sana kwa sababu Magufuli kawatia umasikini wananchi wengi, purchasing power yao imeshuka mno.
Kwenye Elimu bure tena huko. ndo usiseme maana michango kibao inaendelea huko, kuna maeneo watu wanaambiwa waende na madawati ya watoto wao, hiyo ni elimu bure ipi wakati michango ipo kwa mlango wa nyuma.
Zahanati nyingi dawa za msingi na vifaa kama vile gloveszi raia wanaandikiwa wakanunue mitaani na huko ni bei ghali.
Unazungumzia madawati wakati tunaona watoto katika sehemu mbalimbali za nchi bado wanakaa chini, na wanafanyia mitihani chini
Ukichanganya na hasira za watumishi wa umma na wafanyabiashara ambao TRA imevuruga biashara zao sioni ni kitu gani Magufuli ataenda kuwaambia wananchi.
Ana wakati mgumu sana kushinda uchaguzi!
watu wanajitekenya tu. wapiga kura wa ccm wako huko vijijini, mitandaoni wameingia lini?Kwenye Poll moja huko twitter, Lissu kapata asilimia 55.6 ya kura zote, Magu 23.9 na Membe asilimia 20.5, na wapiga kura walikuwa ni zaidi ya watu 9,243.
Sawa kabisa mkuu lakini hakuna aliyepewa upako akaicha biblia kando na kubeba ilaniNashangaa watu walopewa upako wa kuhubir injili wanaweka biblia kando na kubeba ilani. Wanajua kabisa siasa haina kitu maalumu bali huchanganya vyote, haki na dhulma, upendo na chuki, ukweli na uwongo, utu na udhalimu, wema na ubaya
Kazi ya viongozi wa dini kuhusu wanasiasa na siasa ni kukemea mabaya na kuhimiza mazuri katika siasa ili watu waishi vizuri zaidi duniani.
Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
Nione kama unafikia vigezo vya kuitwa utafitiUnataka nakala ya utafiti ili wewe kama wewe ikusaidieje?
Sasa hilo kundi lilizuiwa kufanya siasa na wanatumia mitandao kwani kudai tume huru ni dhambi? Isitosho kama maendeleo anaonekana hofu ya tume huru ni nini? Lakini hao wafanyabiashara wakwepa kodi unadhni ni wengi kushinda wanao ona maendeleo? Hata hao vijana uliosema ni fuata upepo ni wengi sana kiasi wanaweza kuathiri matokeo ya ccm?JPM, akiwa hana nguvu kisiasa, aliwashinda waliokuwa na nguvu kisiasa, ikiwemo huyo Membe. Ni ndoto leo atokee wa kumshinda wakati tayari amekonga mioyo ya wapiga kura (hasa vijijini - 70% ya wapiga kura) kwa utendaji wake wa kazi usio na mfano Tanzania, Afrika Mashariki na dunia nzima. Asilimia 30% iliyobaki ni ya wakosoaji wake na wafuasi wao, kama ifuatavyo:-
Wanaomkosoa ni wanasiasa uchwara, mabingwa wa siasa za majukwaani, ambao baada ya kuzuiwa kufanya hivyo wamehamia kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii wakimpachika sifa ya dikteta uchwara. Hawa wanadai Tume Huru ya Uchaguzi kwa sababu hawana hoja ya maendeleo ya kushawishi wapiga kura, ili waitumie kama sababu ya kushindwa vibaya kwenye Uchaguzi Mkuu ujao.
Wengine wanaomkosoa ni kundi la mafisadi, wafanyabiashara wakwepa kodi, na waliogeuza nchi tajiri kuwa shamba la bibi. Pasipo kumung'unya maneno, kundi hili limeathirika kiasi kwamba nguvu yao ya kiuchumi/kifedha kwa sasa haina madhara makubwa kama kwenye chaguzi zilizopita.
Kundi lingine ni la vijana wa "mishemishe au misheni town" ambao ni bendera fuata upepo. Wakipewa chochote wako tayari kumfanyia lolote atakalotaka au kuagiza huyo mtu wao kama ilivyotokea Uchaguzi Mkuu 2015, walizungusha mikono ati ndiyo mabadiliko, wengine walipiga deki barabara, na wengine walibadilishiwa gia angani na bahati mbaya chombo kikaanguka ardhini, pu!
WAPIGA KURA WAMESIKIA NA WAMEONA TANZANIA INAVYOBADILIKA KUTOKANA NA JUHUDI BINAFSI ZA JPM
Mkuu, kuweka biblia kando ni matendo kinyume na neno hata kama umeshika biblia mkononi. Wakoloni walifanya haya na hata sasa watawala wa Afrika mh!Sawa kabisa mkuu lakini hakuna aliyepewa upako akaicha biblia kando na kubeba ilani
SANDUKU LA KURA LINALORATIBIWA NA NEC NDIO MSEMAKWELI WA MWISHO. Huko twitter nadhani hata mkenya anaweza kupiga kura. πππKwenye Poll moja huko twitter, Lissu kapata asilimia 55.6 ya kura zote, Magu 23.9 na Membe asilimia 20.5, na wapiga kura walikuwa ni zaidi ya watu 9,243.
Sauli hakubatizwa na kuitwa Petro. Labda umekosea! Aliitwa Paul.Msukuma Original,
Lakini sauli aliyebatizwa kuitwa Petro alikuwa farisayo aliyewaua na kuwatesa wakristu, lakini ni huyu sauli ndo kaeneza injili duniania kuliko petro swahiba yake Yesu.
Dogo usikariri
Watu kweli hawamjui kabisa
Watu wanashindwa kuelewa kitu kidogo sana... ukiapply technique flan katika jambo ikafanikiwa ikajualikana... mtu mwingine akiiaply kwa lengo la kumuonesha aliyeanzisha kwamba naye anajua, mara nyingi huwa haifanikiwi kwa kuwa watu hudharau....Napenda kuwajulisha wapinzani wa kweli kuwa nimefanya utafiti wangu usio rasmi. Nimejaribu kupita Facebook, tweeter, Instagram na humu JF na kwenye vyombo vya usafiri nakugundua kwamba wananchi wengi walio upande wa upinzani hawakubaliani na ujio wa Membe.
Hoja yao ya msingi ni kwamba Membe amekuja upinzani baada ya kufukuzwa, maana yake asingefukuzwa angekuwa bado mwana CCM. Kwa mantiki hiyo wananchi wanaona kwamba hana mapenzi na upinzani isipokuwa matatizo yake na chama chake cha awali ndio kimefanya aje upinzani.
Angekuwa anaupenda upinzani angeondoka kabla ya kufukuzwa kama ilivyokuwa kwa Lazaro Nyalandu. Ni sawa sawa na mtu na mpenzi wake wanakwaruzana ndio anaamua kumuacha na kwenda kwa bwana mwingine. Angekuwa anampenda huyo bwana mpya angemfuata kabla ya kugombana na mpenzi wake wa zamani.
Maana yake ni kwamba mpenzi mpya kapata mwenza baada ya mpenzi wake kukorofishana na bwana ake. Siku wakipigiana simu na kuweka tofauti zao pembeni mahaba yatarudi kama zamani na mpenzi mpya ataachwa kwenye mataa.
Napenda kuhitimisha kwa kusema kwamba upinzani wasimsimamishe Membe, wananchi wenye mapenzi ya dhati na upinzani hawamtaki Membe. Bora Nyalandu mara 100 kama Lissu atashindwa kurudi nchini au kama ataletewa mizengwe na mamlaka za Kiserikali.
Umenena kweli mkuu. CHADEMA wasifanye kosa. Lissu ndio habari ya mjini kwa sasa.Watu wanashindwa kuelewa kitu kidogo sana... ukiapply technique flan katika jambo ikafanikiwa ikajualikana... mtu mwingine akiiaply kwa lengo la kumuonesha aliyeanzisha kwamba naye anajua, mara nyingi huwa haifanikiwi kwa kuwa watu hudharau....
Cdm waliipatia... na km unafatilia siasa mbowe alitamka wazi wazi kwamba ile ilikuwa na lengo gani na kwa sasa wamejifunza nn baada ya technique ile....
Act wamezingua kwa 7bu wananchi wameshajua/elewa lengo la wahamiaji toka ccm... kwa hiyo Act ni waz wanataka wagawe kura za upinzani kwa tamaa zao(ama kujionesha nao wanaweza) ss hii inaweza kuwacost coz wapiga kura wengi wako dilema kwa ss...
Kama cdm watatumia hii scenario vzur wanaweza rudi kwa nguvu..
1. Kupitia lisu wanaweza kuamsha ari ya wafuasi wao(na wale walokata tamaa) kwa maana kwamba waandae tour ya jamaa kuwatembelea wafuasi kushukuru(wafanye kwa zone km walivyozoea)
2. Ikibidi waichape na act(kama watakataa muungano wa kusimamisha mgombea wa cdm)- hapa tunaongelea propaganda za akili zinazoelekea na ukweli kuiunganisha act na ccm. Na pia udini uko wazi act lkn cdm lazma waingie gharama ya kutoa mafas nying kwa waislam ili kudemonstrate nankujustify propaganda yao.
Membe hakubaliki POPOTE, siyo huko ulikotaja hata kwa wananchi wa kawaida; hii ni kwa sababu HAWAMJUI utendaji wake na uzalendo wake. Wanao mkubali Membe ni mabeberu wa nje aliwatumikia na kuutana nao huko angani alikokuwa akiruka na kuwafanyia kazi zao kwa miaka yote. Hata hao wa kwao wanamjua kupitia nyumba za kuabudia alizowajengea kwa pesa za kifisadi za CHENJI YA RADAR NA ZA GADDAFI. Vinginevyo hana chochote cha kuifanyia nchi hii Zaidi ya kuiuza kwa mabeberu kwa faida na maslahi yake ndio maana anaomba na kulilia grand coalition ya wapinzani which is NEVER COMING. Apambane na tamaa zake mwenyewe na apambane na HALI YAKE.Napenda kuwajulisha wapinzani wa kweli kuwa nimefanya utafiti wangu usio rasmi. Nimejaribu kupita Facebook, tweeter, Instagram na humu JF na kwenye vyombo vya usafiri nakugundua kwamba wananchi wengi walio upande wa upinzani hawakubaliani na ujio wa Membe.