Ebu taja kipengele kilichokuuliza kutaja warithi ni kipi. Hakuna kipengele kinachotaka kutaja warithi sema wewe na mwenzako mmeelewa vibaya maneno, najua ni pale kwenye next of kin, hiyo next of kin haimaanishi mrithi bali inamaanisha mtu wako wa karibu sana kwa mfano itokee tatizo kama kupotea, ugonjwa serious au kifo ndo wa kwanza kutafutwa ili washirikiane na mwajiri katika mambo yote. Masuala ya mirathi yako wazi kisheria,hakuna wa kurithi zaidi ya mwenza wa ndoa na watoto, so usiumize kichwa sana labda kama hamjafunga ndoa.