Kwenye mkataba nimemwandika kama mrithi Ila yeye kamwandika baba yake

Kiukweli nimegundua wanawake wengi hawaandiki waume zao sababu ya maisha ya sasa ww ukiandika andika acha kuwaza jambo ilo ingawa linaumiza
Wanaogopa wanaume kuoa tena mke mwangine pale wao watapo fariki, wanaona bora wamuandika mzazi kuliko mume.
 
KAA CHINI UMUULIZE SABABU YA YEYE KUFANYA HIVYO, UTAPATA MAWILI MATATU
Sababu ni umasikini wa familia yao, naamini huyo mke we kwao wangekuwa wana mzuri wazazi wake wana jiweza'' naamin ange waandika watoto na mumewe, lakini haiwezekani mwanamke kwao choka mbaya wazazi hawana vipato na wapo vijijini na wanamtegea mtoto wao.
 
Hizo taarifa hazina impact ikitokea mmoja ametangulia ni formalities za kiutumishi, hata akifa leo urithi hauendi kwa aliowaandika hadi taratibu za MIRATHI zifuatwe ambazo kwa sehemu kubwa husimamiwa na Msimamizi wa mirathi.

NEXT OF KIN sio warithi bali ni ndugu wa karibu wa mtumishi ikiwa jambo lolote likitokea awe wa kwanza kutafutwa
 
Yuko sawa 100% japo mie sijafanya hivyo. Mwanamke akifa mara nyingi ndugu wa mume na wengine hawagawanyi mirathi baba anabaki anaisimamia na watoto wake na hata akioa ni sawa. Ila mume akifa mali zinasambaratishwa na kugawanywa na hata akiolewa watataka aache kila kitu. Bado sheria za mirathi zimempendelea mwanaume.
 
aisee kumbe, haya mambo yana namna yake
 
Unaandika mme ana nyumba ndongo ishirini kidogo. Mimi nimeandika wanangu na baba na mama yangu.
Sasa bahati mbaya umefariki una uwakiwa watoto wako watanufaika na mali zako? Kuna jambo nimejifunza kuna rafiki yangu kaka yake alfarikia kaacha mke na watoto wa3 na Nyumba na viwanja kwenye urithi aliandika baba yake, sasa cha kushangaza huyo baba yake ana chukua pesa za kodi ya nyumba ana wagaiya watoto wake t, huyo rafiki yangu akipewa mgao hana kataa, na huyo Baba hawapi mgao mke wa marehemu na wajukuu zake, viwanja vyote mzee ana uza pesa ana wagaiya watoto wake wa kuwa zaa tu.
 
Yani urithi wa mali zake kamuandika baba yake na wanae??? huyo mwanamke wako ana mali zake na wewe una zako wakati nyie mmeoana ??? duuh bhasi nyie mnaishi pamoja anyway na wewe kabadilishe muandike mama yako ila mwisho wa siku jua wanao ndio watakaoteseka
 
Mmmh unauwakika
 
Unaweza kutoa japo mfano wa sheria mojawapo ya mirathi iliyompendelea mwanaume?
 
Amekufanyia makusudi mkeo sio ndugu yako na wewe ungejiweka mwenyewe au mngejaza wote
 
She doesn't trust you and even you don't trust her. Kwa nini ulitafuta kujua kama yeye amejaza nini,???
Hv nyie wanawake[emoji51][emoji51][emoji51][emoji51]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…