Kwenye mkutano wa ACT-Wazalendo Lindi hakukuwa na Mwananchi mwenye Elfu 10 mfukoni. Halafu tunaambiwa tuna Uchumi wa Kati

..Bernard Membe aliuliza wananchi waliohudhuria mkutano wake kuhusu fedha walizonazo mfukoni.

..Katika wananchi waliohudhuria mkutano ule wa kampeni hakuna aliyekuwa na shilingi elfu 10 mfukoni mwake.

..Wakati huohuo serikali inajigamba kwamba tumepanda daraja na kufikia uchumi wa kati.

..Kwa kweli CCM, Dkt. Magufuli, na Serikali, wako out of touch na hali halisi ya maisha ya Watanzania.

..Propaganda walizokuwa wakieneza zimeanza kuwaathiri hata wao wenyewe.
Elfu 10 wapi angeuliza elfu 2 tu kama wanazo
 
Kwa hiyo kipimo cha uchumi wa kati ni watu kutembea na "maburungutu" kwenye mikutano ya kisiasa?

1.What if watu wameona uchuro tu kujitokeza mbele ya kadamnasi ila wanazo?

2.What if wameamua tu kumfurahisha baada ya kujua lengo la swali lake?

3.What if wamehamia kwenye mobile banking zaidi kuliko kutembea na cash?

HITIMISHO:Hoja ina makengeza!
 
Jokakuu,

Swala la nchi yetu kuingia uchumi wa kati sio tamko la Serikali yetu wala CCM ila ni tamko la World Bank

Hvyo kama una pingamizi, manung'uniko, sikitiko, kisununu, miwasho miwasho, kiraruraru basi wapigie World Bank kwa hii namba +1 202-473-1000
Na ndo maana wenye akili kama JK walisema wazi kwamba "sisi kama sisi, target yetu ni $3000 ndipo tutajua tumefika uchumi wa kati" kwa kufahamu, tukishafika hizo $3000, at least uchumi utaanza kuwa reflected kwa wananchi!

Ajabu, ma-CCM yanatamba kwamba tumefika uchumi wa kati kabla ya wakati wakati Vision 2025 inasema wazi kwamba target yetu ni $3000.

That being said, kama ni tamko la WB basi wasingetuambia kwamba tumefika uchumi wa kati kabla ya 2025 kwa sababu hiyo 2025 ni target yetu sisi kwa kiwango cha $3000!
 
Waza.

Vipi kama tungeweza kufanya hakuna mwenye noti ya elfu kumi ila kwa sh 500 unaweza kununua sahani ya wali nyama.

So ingekua tuna uchumi ambao kitathmini chake kisiwe nani ana noti ya elfu 10 ila iwe kwamba kati ya watu 100 watu 89 wanaweza kumudu sahani ya wali nyama.

Ingekua sawa zaidi nafikiri.
 
Hizo "what if" ZOTE ni assumption but deep inside your heart unafahamu majority hawana huo ubavu wa kutembea na 10K sio kwa sababu wameziacha nyumbani bali kwa sababu HAWANA!
 
Ingekuwa sawa kwa sababu, kimsingi ina maana pesa yetu ingekuwa na thamani kubwa... si ajabu, hata $1 tungekuwa tunabadilisha kwa hiyo 500! Na huenda hata hiyo 10K isingekuwepo kwenye mzunguko!
 
Ila Membe ni kichwa kizuri yule jamaa, hotuba kaitoa kichwani yote hskuna cha karatasi wala teleprompter.

Na anajua kujenga hoja na pia kumbe anajua kuiteka hadhira

Kwa sasa namuunga mkono kwa kiwango sawa na ninavyomuunga mkono Lissu. Ngoja tuendelee kusikia sera zao, nabadirika kulingana na hoja!
 
Na ndo maana wenye akili kama JK walisema wazi kwamba "sisi kama sisi, target yetu ni $3000 ndipo tutajua tumefika uchumi wa kati" kwa kufahamu, tukishafika hizo $3000, at least uchumi utaanza kuwa reflected kwa wananchi!

Ajabu, ma-CCM yanatamba kwamba tumefika uchumi wa kati kabla ya wakati wakati Vision 2025 inasema wazi kwamba target yetu ni $3000.

That being said, kama ni tamko la WB basi wasingetuambia kwamba tumefika uchumi wa kati kabla ya 2025 kwa sababu hiyo 2025 ni target yetu sisi kwa kiwango cha $3000!
CCM walisema Tanzania itafika huko 2025 LAKINI BENKI YA DUNIA IKATUFIKISHA HUKO 2020.Tatizo liko wapi?
Ila Membe ni kichwa kizuri yule jamaa, hotuba kaitoa kichwani yote hskuna cha karatasi wala teleprompter.

Na anajua kujenga hoja na pia kumbe anajua kuiteka hadhira
Nadhani hiyo ni kutokana na mafunzo aliyopata kama Security au Intelligence Officer.
 
..Bernard Membe aliuliza wananchi waliohudhuria mkutano wake kuhusu fedha walizonazo mfukoni.

..Katika wananchi waliohudhuria mkutano ule wa kampeni hakuna aliyekuwa na shilingi elfu 10 mfukoni mwake.

..Wakati huohuo serikali inajigamba kwamba tumepanda daraja na kufikia uchumi wa kati.

..Kwa kweli CCM, Dkt. Magufuli, na Serikali, wako out of touch na hali halisi ya maisha ya Watanzania.

..Propaganda walizokuwa wakieneza zimeanza kuwaathiri hata wao wenyewe.
Hata mtunzi mahiri hufika kipindi huishiwa vina. CCM haina jipya, itashinda uchaguzi, si kwa sera na weledi wa utawala, bali uchaguzi usio huru na haki. Moja ya tambo zinazotawala vinywa vya wagombea wa CCM ni huduma za afya na ongezeko la budget ya madawa, huku hospitali za mikoa na vituo vya afya zikiwa na upungufu mkubwa wa madawa. Majengo mazuri yaliojengwa au kukarabatiwa ya vituo vya afya na zahanati hayana tofauti na makaburi yaliopakwa chokaa ndani kukiwa na mifupa ya wafu. Majukwaani maneno ni matamu masikioni, lakini ni kwa wasio jua propaganda za wanasiasa.
 
CCM walisema Tanzania itafika huko 2025 LAKINI BENKI YA DUNIA IKATUFIKISHA HUKO 2020.Tatizo liko wapi?

Nadhani hiyo ni kutokana na mafunzo aliyopata kama Security au Intelligence Officer.
Hawakuishia kusema "tutafika 2025" bali by 2025 tutafika middle income with at least $3000. Na walisema hivyo kwa kuangalia mazingira halisi ya mahitaji yetu!

Sasa WB waliotufikisha huko kwani wamesema hivi sasa tupo kwenye $3000?!

Tuchukue tu hesabu za kawaida! $1080 ni takribani TZS 2,380,000 (at exchange ya Sh 2,200), ambayo ni almost 200K za Kibongo kwa mwezi!

Je, mwenye kipato halisi cha 200K kwa mwezi Bongo hata katika maisha yetu anaweza kuwa considered ni wa kima cha kati?!

Lakini ile $3000, ina maana kwa mwezi ni Sh, 550K. At least Kibongo bongo 550K unaweza kujitutumua!
 
Hawakuishia kusema "tutafika 2025" bali by 2025 tutafika middle income with at least $3000. Sasa WB waliotufikisha huko kwani wamesema hivi sasa tupo kwenye $3000?!
Tuko kwenye kundi la "low middle income countries" hii ina range ya kipato na hiyo $3000 unayong'ang'ania wewe imo kwenye hiyo low middle income.
 
Hizo "what if" ZOTE ni assumption but deep inside your heart unafahamu majority hawana huo ubavu wa kutembea na 10K sio kwa sababu wameziacha nyumbani bali kwa sababu HAWANA!
Hiyo Deep inside yako ni assumption.

Na hata hitimisho lako pia ni assumption vilevile.

10K mwaka 2020 nayo pesa sasa?

Posho ya kibarua site useme majority hawana hata nyumbani!

Labda alikuwa anahutubia umati wa ombaomba na walemavu.
 
Jokakuu,

Swala la nchi yetu kuingia uchumi wa kati sio tamko la Serikali yetu wala CCM ila ni tamko la World Bank

Hvyo kama una pingamizi, manung'uniko, sikitiko, kisununu, miwasho miwasho, kiraruraru basi wapigie World Bank kwa hii namba +1 202-473-1000
Mbona ngoma ilisharudishshwa ilipotoka
 
Hiyo Deep inside yako ni assumption.

Na hata hitimisho lako pia ni assumption vilevile.

10K mwaka 2020 nayo pesa sasa?

Posho ya kibarua site useme majority hawana hata nyumbani!

Labda alikuwa anahutubia umati wa ombaomba na walemavu.
Sasa mbona unajikanganya!!!

Unahoji ikiwa 10K na yenyewe ni pesa huku ukiona hoja ya Membe ni Makengeza kwa vile tu amesema wakati tunadai nchi imefika uchumi wa kati, lakini watu wanashindwa kuwa hata na 10K mfukoni!

Halafu acha kujifanya wewe ndo unazo sana kiasi cha kuwaona wale ambao hawana 10K eti watakuwa ni ombaomba na walemavu!! Unataka kujifanya mtoto wa kishua uliekulia ughaibuni kiasi kwamba hujui maisha halisi ya Watanzania, au?!
 
Tuko kwenye kundi la "low middle income countries" hii ina range ya kipato na hiyo $3000 unayong'ang'ania wewe imo kwenye hiyo low middle income.
Ninayong'ang'ania mimi kwani mimi ndie niliandaa Vision 2025?!!
 
Sasa mbona unajikanganya!!!

Unahoji ikiwa 10K na yenyewe ni pesa huku ukiona hoja ya Membe ni Makengeza kwa vile tu amesema wakati tunadai nchi imefika uchumi wa kati, lakini watu wanashindwa kuwa hata na 10K mfukoni!

Halafu acha kujifanya wewe ndo unazo sana kiasi cha kuwaona wale ambao hawana 10K eti watakuwa ni ombaomba na walemavu!! Unataka kujifanya mtoto wa kishua uliekulia ughaibuni kiasi kwamba hujui maisha halisi ya Watanzania, au?!
Rubbish.
 
Back
Top Bottom