Kwenye msitu wangu kuna black mamba/ koboko natafuta njia za kumwangamiza bila kuleta madhara kwenye jamii

Wengi msilolijua kuhusu nyoka na porini ni kwamba tunakutana na nyoka wengi sana porini na barabarani hasa vijijini ila nyoka wanatuepuka bila sisi kuwaona.
Nyoka anahisi hatari ya binadamu kwa kishndo chake tuu akiwa mbali na anakuepuka. Na ndio maana ni rahisi kumuona nyoka akiwa kwenye windo, au sehemu ya wazi au kumbabatiza " encounter" yani papo kwa papo mmekutana, hakutarajia wala hukutarajia.
 
Hapo achana na kufuga nyuki. Fuga hao Koboko. Wanalipa sana. Unaweza ukawa unawakamua sumu yao unaweka kwenye vikopo unauza. Au unachinja unakuja uza kwa wachina. Wachina wanapenda sana nyama ya koboko. Na hiyo sumu ya koboko ni very expensive.

Hata ngozi yake inatumika kutengenezea viatu, pochi, mikanda na ni very expensive. Achana na nyuki endeleza kufuga koboko. Yaani umenifanya mpaka mwili usisimke. Nikasema kweli upele unamwotea asiye na kucha.

Hapa ilitakiwa uje kuuliza soko la sumu ya koboko, nyama na ngozi yake. Chakula si issue sana. Fuga panya walishe koboko wako wanenepe wazaane. Utatajirika sana.

Usione kama ni tatizo hiyo ni fursa ndugu. Ni fursa ya utajiri.
 
[emoji3590][emoji3590][emoji3590]
 
Tafuta Nyegere(Honey badger) dume na jike.. Ni vigumu kuwapata ila ukiwasiliana na wenyeji na ukatangaza pesa utaletwa .. Hao Koboko wako wataliwa ndani ya wiki moja.. Na wasipoliwa basi watahama eneo hilo na kutokomea mbali kabisa.. Koboko ni chakula cha Nyegere.. Nimesema ulete dume na jike ili wakae kwenye hilo pori.. Ukileta mmoja tu lazima atahama kutafuta mwenza.. Ila wawili wataweka makazi yao hapo..
 
Daaah...hawa motivation sprakers watakuja kuua watu
 
Huyo nyoka ni hatari sana mkuu, ana upeo mkubwa, kuwa makini usikute ashaona hata huu uzi

Hapo anakusubiri urudi msituni, umueleze comments zilikuwaje?
🤣🤣🤣
 
Nilifikiri kuna Inland Taipan 🤷🏾‍♂️🤷🏾‍♂️🤷🏾‍♂️
 
paka anaua nyoka yeyote yule isipokuwa chatu .......paka anauwezo mkubwa wakuona kasi ya nyoka yoyote yule (kasi ya kurusha mate au ya kung'ata) anaiona in slow motion ndo maana anaweza epuka mate au mdungo wa nyoka na kumchapa makofi meng tu mpaka akaded ..........hakuna cha koboko au king kobra wote n wachumba tu kwa paka.
 

ni mkoa ngani mkuu?? Hawa viumbe wanapatikana zaidi mikoa ya Tabora, Shinyanga, kigoma , Geita. Tafta wale wataalam wa nyoka ( waganga wa kienyeji ) atawatoa wote
 
King Cobra NI mkazi wa Asia,hasa India na Pakistan,sasa atamfikishaje kigoma?? MbonA unakuwa Kama mwehu hivi
 
Mrejesho. Kwa Sasa nikiangazi yule nyoka haonekan Tena sio kelele anazo Lia usiku ama Kuonekana Kwa macho.

Wenyeji wanasema huenda kaliwa na bundi maana bundi Kwa Sasa Wakati huu wakiangazi ni wengi sana.

USHAHIDI:- mifupa iliyosadikika kuwa ya nyoka ilionekana na baadhi ya wamama wanao senya Kuni mle na kumpa taarifa mzee wangu.

Mzee alienda kuitambua yeye Kwa uzoefu wake alikiri kuwa ni kweli ni mabaki ya nyoka

Lakini huenda ni ya nyoka aina ya swila ( wale weusi) maana Kuna baadhi ya mabaki ya ngozi ni nyeusi.

USHAHIDI:- wachungaji wa mifugo.

Wao wanasema katika kati ya mwezi wa sita mbwa wao aling'atwa na nyoka na kufa ndani ya muda mfupi.japo hawakumuona huyo nyoka dalili zote za mbwa kung'atwa na nyoka zilionekana.

Baada ya siku chache mbele nao walikuta mabaki ya mifupa ya nyoka sehemu tofauti Hawa walikiri yatakuwa ya koboko Moja Kwa Moja.

Bado Sina jibu la Moja Kwa Moja kama nikweli huyu nyoka kashakufa au kahama Kwa muda kupisha shughuli za kibinadamu kama kusenya Kuni na walina asali usiku japo Kwa uchache sana.

Wiki ijayo nitaanza mapumziko mafupi nitaenda mwenyew na kuwaletea mrejesho kamili.

Ahsanteen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…