Kwenye ndoa watu wanaviziana

Kwenye ndoa watu wanaviziana

Mume alioa mpumbavu na pia mume hakuwa akijitambua,huu ujinga wa 50/50 unabomoa sana ndoa za vijana wa siku hizi

Mwanaume ndiye unaeoa ukitegemea unaemuoa atazaa watoto sasa kwanini uanze kutegeana na mkeo namna ya kuiletea mafanikio familia yako?mwanaume unatakiwa kila kitu ukifanye wewe kiwanja nyumba ada za watoto etc vyote ni juu yako.
Una kaujinga fulani

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hoja ya kuandika jina la Nani kwa Mali za wanandoa Haina mashiko!

Jina lolote liandikwe Ila Mali inabaki kuwa ya wote as long as imepatikana ndani ya ndoa
Na hata ikitokea kuachana mgao utapigwa bila kujali Mali ina jina la mume au mke

Labda iandikwe jina la mtoto au individual yoyote nje ya ndoa, hio ni kesi tofauti

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Wewe Masai Ndito, wacha hayo mambo, ndani ya boma ya ng'ombe, ng'ombe ni wa baba na maziwa ya ng'ombe ni ya mama. Ile upendo ilienda na muzee SOKOINE, sasa wewe tafuta pesa mingi, amani itakuwa na wewe. Hata huko kanisani, zamani ilikuwa inafundishwa upendo, lakini sasa inafundishwa kutoa sadaka mingi ya mbesa na inaambiwa kanyaka mafuta ili ipate mbesa mingi, siyo kanyaga mafuta ipate upendo mingi. Wee, chah erru, angalia sana hii kitu! Ile mutu kule Kenya, morani moja imeiba " mbessa sabuni ya roho" haijaimba" upendo sabuni ya roho". Mimi iko nasema hivi, meti hela, meti upendo!
Ahsante sana ni mimi Ole Supu Supu , kama haitaki ite Ole Mukuki.
 
Ki uhalisia hapo ilitakiwa iweje????

Haya mambo mkiwa wote hizo mali na bla bla wala sio ishu.....ishu inakujaga pale mmoja akitangulia tena especially mwanaume. Na una watoto.....kiukweli hili hata tukijifanya hatuongelei ila huwa linaclick kichwani.

Ndugu wanakujaga kudai hadi miswaki. Baba angu alitangulia mapicha picha niliyaona kwa mama angu.
Sahihi sana
 
Lile dhumuni halisi la upendo, kuaminiana na kuwa na dhati ya mpaka kuzikana ni wachache sana wenye hiyo mutual intention, ni either mmoja awe anamvizia mwenzie au wote kwa pamoja.

Akili na uwezo wote anapeleka kwenye kulinda mali zake such as kuandika majina yake kwenye vitu vyake kuogopa huko baadaye huyu anaweza nigeuka.

Kufanya project za siri, kutokumshirikisha mwenzako kiwango cha pesa zako, yaani ilimradi kuviziana tu.

Lile lengo la kuwa pamoja hata halipo kabisa.

Wewe ukiwa kwenye side ya kuviziwa unaweza umizwa sana tena ukararuliwa kila mahali, maana watu wengi wenye mioyo safi ni wachache kiasi kwamba anaye kuvizia muda mwingine sio lengo lake lakini ashakutana/ashashuhudia mbwa mwitu wengi wenye ngozi ya kondoo.

Kama upo kwenye ndoa/upo na mwenza na moyo wako upo safi kabisa lakini unahisi uliyenae maybe anakuvizia ujae kwenye mfumo....endelea kuwa mwema tu, ipo siku atauona wema wako na ataacha hizo habari za kuishi na wewe kimachale machale na kutenda dhumuni la ndoa.

Ila watu wanatakiwa wajue haya mambo yanaumiza sana kuingia kwenye ndoa na wasiwasi wa namna hiyo. Hilo sio lengo la ndoa.

Wakati fulani tulishasuluhisha jambo fulani lakini katika huo ugomvi wa wanandoa.

Mke alitoa 50% ya hela ya kiwanja na mume nae alitoa.

Ila mke akawa anataka kuandika jina lake na mwanaume nae anataka jina lake liandikwe. It was real sad kwa sababu wote walikua wanaviziana. WALIKUJA KUACHANA.
Pia kinga ni bora kuliko tiba
 
Back
Top Bottom