Paulo wa Tarso ni Mtume WA kimataifa, aliyeinjilsha Maeneo ya ugiriki(korinto, Efeso, Galatia,) warumi, Uturuki n.k.
Akiwa nje ya uyahudi alikuwa akitumia zaidi maoni yake kuliko sheria ili awapate watu wa mataifa.
Paulo alikuwa Mtume wa watu wa Mataifa kwa neema ya Mungu. Kusema kwamba alikuwa akitumia maoni yake ni ama UPOTOSHAJI ama KUTOELEWA maandiko. Twende taratibu:
Mfano, Alipokuwa na Warumi wala-nguruwe aliwaambia mtu asiwahukumu Kwa vyakula vyenu, au kutokushika sabato kwenu(hao warumi) kwani walikuwa hawaabudu siku ya sabato
Paulo ni Kama hawa kina Masanja au Mwamposa sio ajabu wakimtumia zaidi katika Aya zao Kwa lengo la kuvuta watu wasiomjua Kristo.
Huu ni uzushi na upotoshaji mkubwa kumfananisha Paulo na akina masanja. Wewe naanza kuamini ni msabato ambao kimsingi ni wafuasi wa nabii mie INGAWA sheria haijampa ruhusa mwanamke kuongoza wanaume. Suala la vyakula halikuanzia kwa Paulo:
Mathayo 15 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁵ Basi Petro akajibu, akamwambia, Tueleze mfano huo.
¹⁶ Yesu akasema, Hata sasa ninyi nanyi mngali hamna akili?
¹⁷
Hamjafahamu bado ya kuwa kila kiingiacho kinywani hupita tumboni, kikatupwa chooni?
¹⁸ Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi.
¹⁹ Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano;
²⁰ hayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi; lakini kula kabla hajanawa mikono hakumtii mtu unajisi.
Embu tumsome hapa;
1 Wakorintho 9:20
Nalikuwa kama Myahudi kwa Wayahudi, ili niwapate Wayahudi; kwa wale walio chini ya sheria, nalikuwa kama chini ya sheria, (ingawa mimi mwenyewe si chini ya sheria), ili niwapate walio chini ya sheria.
Nini kilicho kuchanganya hapo? Ili niwapate... Paulo alitumia mbinu ya kawaida tu kuheshimu desturi zao ili wapate kumsikiliza, kisha akawahubiri kweli ya Mungu. Mfano kwako, ukitaka kwenda kuhubiri msikitini huwezi kuingia n aviatu, utavua viatu kwanza ndipo uingie halafu wakusikilize, hapo ndipo utawapata. Lugha ngumu kwako hii hata umshutumu Paulo kwa uongo?
1 Wakorintho 9:21
Kwa wale wasio na sheria nalikuwa kama sina sheria, (si kwamba sina sheria mbele za Mungu, bali mwenye sheria mbele za Kristo), ili niwapate hao wasio na sheria.
Kwao wasio na sheria ni wale ambao hawaijui ama hawaifuati sheria ya Mungu (ndio watu wa Mataifa) Paulo aliketi nao akawafundisha sheria ya Mungu kwa utaratibu, sio kama mwanasheria bali kama rafiki mwenzao lakini amesema wazi yeye aliishika sheria ya Kristo, hivyo hakuwa nao katika kutenda dhambi kama unavyopenda iwe. Acha uzushi.
1 Wakorintho 9:22
Kwa wanyonge nalikuwa mnyonge, ili niwapate wanyonge. Nimekuwa hali zote kwa watu wote, ili kwa njia zote nipate kuwaokoa watu.
1 Wakorintho 9:23
Nami nafanya mambo yote kwa ajili ya Injili ili kuishiriki pamoja na wengine.
Aya ya 9:23 inaeleza kusudio la Paulo ni kupata wafuasi WA Injili na sio Wafuasi WA Mungu.
Wafuasi wa Injili ni nini? Mbona unaanzisha uzushi na upotoshaji wa namna hii? Mungu akurehemu. Haya tuonyeshe aina ya wafuasi wa Injili aliowapata Paulo ambao si wafuasi wa Mungu. Lete ushahidi wa wazi nami nitakuonyesha wafuasi mahususi wa Mungu ambao walitokana na kazi ya Injili kupitia Paulo. Acha uzushi utaishi.
Alichofanya Paulo ni Kama mhubiri ambaye ameenda Kwa Mtu Malaya au mlevi alafu akamuambia mtu huyo asijali kuhusu umalaya wake, wala mtu asimhukumu Kwa umalaya wake, sio kwamba kahalalisha umalaya Ila anajaribu kumfanya Malaya ajione kuwa amekosea Ila ana -second option ya kutibu.
Kuna Mtume yupi aliyekemea kwa ukali dhambi kama Paulo? Kwa nini umeamua kuwa ajenti wa ibilisi aliye baba wa uongo. Sioni msingi wa maandiko kwenye hoja zako bali ni mtu anayetetea imani ya genge fulani. Napata taabu hata kukujibu kwani maneno yako ni uongo wa wazi kabisa.
Lakini kwenye ishu ya Talaka Paulo anakiuka amri ya Mungu inayompa mwanaume ruhusa ya kutoa Talaka Kwa mkewe.
Soma malaki 2 na mathayo 19 kwa kuanzia. Uongo wako utakuwa dhahiri
Pia Paulo kwenye amri ya ndoa anatoa maoni yake kuwataka watu Kama wataweza wasioe Jambo ambalo linakiuka sheria kuu ya mungu ya Mwanaume kuoa na kuzaa ili kutekeleza amri ya kuijaza dunia
Wewe ndugu, Acha kabisa kumezeshwa uongo wa shetani, emekuwa mwongo mpaka unamkana Kristo?
Mathayo 19 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹¹ Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa.
¹² Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao; tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi;
tena wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee.
Je, wewe umeshindwa kulipokea neno hili la Kristo ambalo Paulo alijengea msingi wa mafundisho yake? Mtu kukushauri kutokuoa ili upate UFALME WA MUNGU ni kosa? Kwani amesema usioe ili uwe huru kufanya ukahaba? Hivi mnayasomaje maandiko ninyi lakini? Omba sana kuongozwa na Roho wa MUNGU nawe utaijua kweli.
Amina