Kwenye offside huwa inaangaliwa nini?

Kwenye offside huwa inaangaliwa nini?

Viol

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Posts
25,420
Reaction score
18,298
Nataka nifahamu offside huwa inakuwaje?
Mchezaji anayeshambulia akiwa peke yake kule mbele?
Je asipogusa mpira?
Kuna wengine wanasema ukipigiwa mpira na upo juu ukaunganisha shuti hata ukiwa mbele siyo offside
Usahihi wa offside ni upi?
 
Last edited by a moderator:
hahahah wamekudanganya hao waliokwambia hivyo, we huoni watu wanafunga magoli ya vichwa lakini yanakua offside??
 
kibendera huwa anatembea na beki wa mwisho,, kwa hiyo ukimzidi beki wa mwisho ni offside, na offside inaanza kuesabiwa katikat ya uwanja....
 
Nataka nifahamu offside huwa inakuwaje?

Mchezaji anakuwa 'offiside' pale tu anapopokea pasi ilihali yupo mbele zaidi ya mchezaji wa mwisho wa timu pinzani kuelekea lango la timu pinzani.

Na eneo ambalo sheria ya 'offiside hutumika ni eneo lote la nusu ya timu pinzani.

Kuna wengine wanasema ukipigiwa mpira na upo juu ukaunganisha shuti hata ukiwa mbele siyo offside

Endapo mpira umerushwa basi hapo hakuna offiside, kinyume na hapo mpira wowote utaoguswa na mchezaji aliyeotea utahesabiwa ni faulo ya offside...
 
Ushawahi kuona video clip YouTube,kipa kadaka mpira akasahau kuna mshambuliaji nyuma yake,ile anauweka chini aupige mshambuliaji akatoka nyuma akamwahi na kufunga goli,hiyo siyo offside?
 
Mabeki huwa wanatengenezaje offside?
 
Nataka nifahamu offside huwa inakuwaje?
Mchezaji anayeshambulia akiwa peke yake kule mbele?
Je asipogusa mpira?
Kuna wengine wanasema ukipigiwa mpira na upo juu ukaunganisha shuti hata ukiwa mbele siyo offside
Usahihi wa offside ni upi?

Mchezaji anakuwa offside ikiwa sehemu aliyokuwepo atakuwa amewazidi walinzi wa timu pinzani zaidi ya nchi moja pindi mpira unapotoka mguuni mwa anayempigia pasi hata awe ni golikipa.
 
Je inaruhusiwa mpira ukiwa juu ila upo nje ya mstari ukawahiwa kabla haujatua chini ukarudishwa uwanjani?yaani zile pande mpira ukitoka unarushwa
 
Hiyo ni kazi ya mshika kibendera huo mpira utakuwa umetoka nje ya uwanja hata kama haukutua chini.
 
Ushawahi kuona video clip YouTube,kipa kadaka mpira akasahau kuna mshambuliaji nyuma yake,ile anauweka chini aupige mshambuliaji akatoka nyuma akamwahi na kufunga goli,hiyo siyo offside?

Si offside...
 
Je inaruhusiwa mpira ukiwa juu ila upo nje ya mstari ukawahiwa kabla haujatua chini ukarudishwa uwanjani?yaani zile pande mpira ukitoka unarushwa

Mpira ukishavuka mstari hata kama upo hewani bado unahesabiwa umevuka mstari...

Sasa itategemea ni mstari upi; kama ni mstari wa goli basi litakuwa ni goli na kama ni mstari wa pembeni utakuwa mpira wa kurusha, kona au golikiki
 
Hebu nami niulize swali,
Kama mchezaji amepiga mpira mbele ila kule mbele kuna mchezaji mwenzake ambae yupo offside lakin yule mchezaji alie offside hajagusa ule mpira na yule mchezaji aliepiga mpira amekimbia na kuukuta ule mpira, Je inakuwa offside au anaweza kufunga tu kama amepata nafasi ya kufunga?!!!
 
Mchezaji anakua off side tu pale anapowazidi mabeki Wa timu pinzani pindi pasi inapotoka mguuni mwa anaeipiga,

Lakini anakua off side tu pale anapoonekana kutaka kujihusisha na pasi ile ikiwa hatoonesha kujihusisha na mpigaji akaifuta mwenyewe na kufunga ni goli halali.

Mnaweza mkawa wachezaji wengi mnaooneka mmezidi lakini kama hamkuujihusisha na play hiyo haiwi off side
 
Mchezaji anakuwa 'offiside' pale tu anapopokea pasi ilihali yupo mbele zaidi ya mchezaji wa mwisho wa timu pinzani kuelekea lango la timu pinzani.

Na eneo ambalo sheria ya 'offiside hutumika ni eneo lote la nusu ya timu pinzani.

Endapo mpira umerushwa basi hapo hakuna offiside, kinyume na hapo mpira wowote utaoguswa na mchezaji aliyeotea utahesabiwa ni faulo ya offside...

Ahsante Mkuu, umeeleza kama kile ambacho mimi nimetaka kueleza hususani ktk sentensi zako za mwanzo.
Hii dhana ya kuzuia Offside ndio inawaumiza sana wapinzani wanaocheza dhidi ya Barcelona.
 
Mchezaji anakua off side tu pale anapowazidi mabeki Wa timu pinzani pindi pasi inapotoka mguuni mwa anaeipiga,

Lakini anakua off side tu pale anapoonekana kutaka kujihusisha na pasi ile ikiwa hatoonesha kujihusisha na mpigaji akaifuta mwenyewe na kufunga ni goli halali.

Mnaweza mkawa wachezaji wengi mnaooneka mmezidi lakini kama hamkuujihusisha na play hiyo haiwi off side

Absolutely, mfano ni Goli la Messi msimu uliopita dhido ya PSG. Alves alipiga pasi na beki za PSG wakajua kuwa mpira unaenda kwa Neymar au Alba, basi wao wakawakaba Neymar na Alba.
Kumbe Alves alikusudia mpira uende kwa Messi na kweli bhana Messi nae akajua ule mpira unaenda kwake. Beki za PSG hata hazikulalamika.
 
Hebu nami niulize swali,
Kama mchezaji amepiga mpira mbele ila kule mbele kuna mchezaji mwenzake ambae yupo offside lakin yule mchezaji alie offside hajagusa ule mpira na yule mchezaji aliepiga mpira amekimbia na kuukuta ule mpira, Je inakuwa offside au anaweza kufunga tu kama amepata nafasi ya kufunga?!!!
Inategemea... kama huo mpira uliopigwa ulielekezwa kwa huyo mchezaji aliyekuwa mbele na hakuhugusa na alikuwa offside (akihusika nao vyovyote vile aidha body movement )basi hiyo itahesabika kama offside
Lakini kama huyo mchezaji aliyekuwa mbele hakuhusika na mpira huyo kinamna vyovyote vile na ikatoke yule jamaa aliyeupiga mpira akaukuta na kufunga basi hilo goli litakuwa halali kabisa
 
Ahsante kwa ufafanuzi wako mkuu.
 
Mchezaji anakua off side tu pale anapowazidi mabeki Wa timu pinzani pindi pasi inapotoka mguuni mwa anaeipiga,

Lakini anakua off side tu pale anapoonekana kutaka kujihusisha na pasi ile ikiwa hatoonesha kujihusisha na mpigaji akaifuta mwenyewe na kufunga ni goli halali.

Mnaweza mkawa wachezaji wengi mnaooneka mmezidi lakini kama hamkuujihusisha na play hiyo haiwi off side
Ahsante kwa ufafanuzi.
 
Tusijikite zaidi kwenye kikundi nomino 'mabeki wa timu pinzani' inaweza kupotosha ukweli.

Mchezaji atakuwa offside endapo kipindi mpira unapigwa kwake huku akiwa amemzidi mchezaji wa pili wa mwisho (second last player) kuelekea lango la timu pinzani basi atahesabika kuwa ameotea.

Sheria hiyo namba 11 ya mchezo wa soka inataka angalau wachezaji wawili wa timu pinzani wawepo kipindi mfungaji anapigiwa pande kuelekea langoni kutafuta bao. Golikipa ni mmoja wa wachezaji hao wawili. Endapo golikipa atakuwa ameingia ndani ya uwanja basi angalau wawepo wachezaji wengine wawili. Endapo atabaki mchezaji mmoja tu mfano beki Tshabalala wa Simba wakati Kipa Mapunda ameingia uwanjani kusaka bao, Msuva wa Yanga akipigiwa pande huku Tshabalala pekee kabaki mbele yake basi hiyo nayo ni clear offside.

Sheria za mchezo wa soka zinapatikana katika website ya FIFA. Aidha unaweza kuzipata kwa ku-google: 'Football Laws of the Game filetype😛df' utazipata na kujisomea mwenyewe, huenda ukashawishika kuelewa zaidi ukajiunga na mafunzo ya waamuzi na hatimaye ukaja kuchezesha Simba na Yanga kwa haki kuliko waamuzi wa sasa akina Sanya, Nkongo na wengine wa namna hiyo.
 
Makoye Matale;

uko sawa kabisa kuhusu atlest wawepo watu wawili umenikumbusha tukio la game ya ufunguzi worldcup 2010 south na mexco
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom