Kwenye siasa hata mpiga kura mmoja ana veto sana, puuzeni tu ya JF

Kwenye siasa hata mpiga kura mmoja ana veto sana, puuzeni tu ya JF

Tila-lila2

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2019
Posts
652
Reaction score
1,058
Nipo kwetu Idukilo, namalizia malizia mapalaghe ya Mwaka jana ili tuanze kumenya viazi vya Mwaka huu. Twala misosi ya asili ndiyo maana Wasukuma tupo rijali sana.

Nimekuwa nikifuatilia eti watu wanadharau comments za mitandaoni kwa kuwa wanaona eti watu ni wachache sana mitandaoni.

Pamoja na kuwa mimi sio Mwanasiasa lakini uzoefu wangu kura moja ya mpiga kura inaweza kubadili sana mwelekeo.

Kwa mfano mimi na baiashara yangu ya mahindi na mapalaghe hapa Idukilo nikisema tu kuwa nampigia kura fulani katika Uchaguzi kuna uwezekano mkubwa sana nikaungwa mkono na wateja wangu wote.

Yaani wale wananiletea viazi halafu ninavikatakata kuwa mapalaghe na wale amba nawauzia mahindi nikishayafuata kule Kahama na Ushirombo. Ninawajua sana wapiga kura wa huku.

Kwa maana hiyo basi najua tunadharau sana comments za humu JF tukiwa tumejawa na kiburi kuwa wapiga kura wengi hawajui kinachoendelea mtandaoni, lakini nawaambia mitamdao hadi Idukilo inafika.

Juzi nilikutana na rafiki yangu katokea Mipa akaniambia "aseee kwenye kasimu kangu nilifungua JF nikakuona ulivyotoa hoja huko" - nikashangaa lkn ndiyo uhalisia huo.

Tusifikirie utandawazi haujawafikia. Kuna mtu Mwaka huu atatembea na kompyuta Mpakato akawa anafanya kampeni huku akionyesha threads za JF na kuwabadili watu kwa jumla.

Hata hivyo sipingani labda ni mikakati ya kuharibu Uchaguzi km ilivyofanyika Serikali za Mitaa. Hilo likitokea Uchaguzi huu ujao tujue kuwa harufu ya majanga ya kifokifo nchini mwetu inatuvizia.
 
Upo Idukelo sehemu gani? Unamfahamu Ngwate, Ibapala na manju wengine maarufu wa ngoma ya beni? Vipi beni bado inatamba kipindi cha kiangazi?
 
Upo Idukelo sehemu gani? Unamfahamu Ngwate, Ibapala na manju wengine maarufu wa ngoma ya beni? Vipi beni bado inatamba kipindi cha kiangazi?
Beni inatamba ingawa ng'waka jana kulikuwa na ukata watu hawakushiliki sana!
 
Mkuu (nalewa) Tila Lila, hoja yako ni ya msingi sana.
Asante.
P
 
Back
Top Bottom