Kwenye Suala la Engagement fans,Yanga wametuzidi kwasababu ya ujinga wetu

TUKANA UONE

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2018
Posts
2,345
Reaction score
6,970
Salamu ni Utumwa


Hapa ndugu zangu inapaswa tutofautishe kati ya Fans Engagements na Followers au Subscribers!.

Haiwezekani kila siku mashabiki wa Simba wenzangu tuendelee kuizungumzia Yanga tukidhani tunaipondea kumbe ndo tunaipaisha,mwanzo kabla ya kufahamu na mimi nilikuwa mpondaji Sugu wa UTOPOLIANS lakini baada ya kugundua nawapa Mileage nikaamua kukaa kando.Yanga imefanikiwa huko mitandaoni kwasababu yetu sisi mashabiki wa Simba iwe ni kujua au kutokujua,jamaa wanapata Engagements kubwa kuliko tunavyodhani.

Hebu niwasii wanasimba wenzangu tuigeukie club yetu sasa,hapo miaka 2 iliyopita Utopolians walikuwa wanatafutana lakini cha kushangaza leo sisi ndo tunatafutana,hii ni aibu kubwa sana nikiwa kama mwana lunyasi.

Tusipobadirika naona kabisa hawa Utopolians wanaenda kutake over huko mitandaoni,hebu tuachane na habari za utopolo na kuwapa umaarufu,turudi tusapoti mambo yetu
 
Yanga ni kama maji tu bwashee..

Usipoga basi utakunywa au utanawa..
 
Nyinyi Kila siku kutukandia tu. Sisi muda wa kuwafungulia thread za kuwakandia humu hatuna. Na uzuri wa yanga fans waliokosa ajira wachache so muda huu hatuna. Simba Ina jobless wengi sana ndo mana tukishindaga tunawasaidia hela za kula
 
Mbona Simba wana number kubwa kwenye Social media platforms zao tofauti na Yanga?
Rejelea Facebook, Instagram, Twitter na YouTube channel.
Imekaaje hii kitaalam?
 
Huwezi kukuta Diamond platinum anamuongelea Baba levo, Bali baba levo analazimika kumuongelea Diamond.

Kikubwa husemwa na kuimbwa sana lakini kidogo huungana na vidogo vyenzake kukisema kikubwa.

Simba
Azam
Namungo
Singida watake wasitake lazima waiseme yanga πŸ˜…
 
Hapa ndo nimeelewa hoja ya mleta mada

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Unasema mrudi msapoti mambo yenu yapi sasa. Vunjabei kuleta jezi mwezi mzima baada ya msimu? Kumleta manzoki kwenye uchaguzi na si kumsajili? Kukosa makombe yote? Kuendelea kuwasajili kina bocco na onyango?
 
Simba angeenda Hadi fainali ya champions league usingesema hivi...
Huwezi lazimisha engagement kama hata mechi huchezi
 
Wasiwasi wako tu wa kutojiamini.
 
Sasa msipoiongelea Yanga huku mitandaoni mtakuwa mmefuata nini? Si bora mjitoe tu?
Rais amewaagiza Yanga walimalize swala la Feisal, msitafute namna ya kukwepa kulifuatilia na kuliongelea hili. Yanga wanasubiri Simba waliongelee hili likiwemo la kupewa ndege na rais kwenda kucheza Mbeya.
Msipoyaongelea haya mnataka nani ayaongelee wakati mnajua fika kuwa mashabiki wa Yanga wana mambo mengi ya kufanya na wanawategemeeni sana nyie ndiyo muwe mnaongelea mambo ya club yao?
Acheni ujinga wa kutaka kuyakimbia majukumu yenu.
 
Umeuwa aisee ndiyo kazi iliyobaki kwao sasa wanataka kukwepa kutimiza majukumu yao, walahi nimecheka sana
 
Daah,we jamaa πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Simba ya try again imekuwa paka.

We simba mnatangaza jersey saa 6 usiku kama mnafanya zindiko.

Simba wamrudishe Gonzales yule dada alikua kichwa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…