Kwenye Uchaguzi Huu CHADEMA hatuna cha kujifunza kutoka CCM

Kwenye Uchaguzi Huu CHADEMA hatuna cha kujifunza kutoka CCM

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
Chadema inacheza katika kiwanja cha Demokrasia kiwanja ambacho CCM haiwezi kuingiza team uwanjani, Chadema imeshikilia kurasa zote za mbele za vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi juu ya uenyekiti wa chama.

CCM ni wageni wa mashindano haya ya Demokrasia ukiona wanashangilia usiwashangae ujue wamepata team ya kushangilia kwani wao ni ligi daraja la kwanza kwenye kombe la Demokrasia.

Wao mwenyekiti wanampata kwenye uchaguzi mkuu, yaani ukiona CCM wanaomba kura kwenye uchaguzi mkuu ujue wapo kwenye mchakato wa kumpata mwenyekiti wa chama pia.

Rais atakaye shinda ndio mwenyekiti wa chama Chao, mwenyekiti mwenye mamlaka ya urais, yaani wanavyoingia kwenye kikao cha chama wanakaguliwa mpaka sehemu za siri, mwanachama hana uhuru wa kumkumbatia mwenyekiti wake kama ambavyo sisi tuna jimwaya nao.

Na sio mwenyekiti tu hata makamu mwenyekiti hachaguliwi kama sisi chadema, wao wanateua tu, kwahiyo kwenye uchaguzi huu sisi hatufananishwi nao bali sisi ni walimu wao wa demokrasia.
Wakisema mwenyekiti wenu au makamu wenu amekaa muda mrefu waulizeni wao ni lini wamechagua mwenyekiti wao au makamu wao, wao hawana uhalali wa kutuuliza mambo ya uongozi wetu, simnakumbuka tulifiwa na rais magufuli basi wao hawakufiwa na rais tu bali walifiwa pia na mwenyekiti wao.

Msiwachukie CCM mkiwaona madirishani wakitazama mechi zetu za Demokrasia wao hawajawahi kuingiza team uwanjani, wanajifunza kupitia sisi karibuni wanafunzi wetu wa Demokrasia mjifunze bila kutoa Ada.
Mpaka sasa Team Lissu na Team Odero wapo uwanjani wanasubili mshindani mwingine, huku CCM wakiwa karibu na Runinga zao kufuatilia mtanange.

Walimuua Thedei Ole Mushi msitegemee majibu ya hoja zangu zaidi ya kuniombea nisitekwe.

May be an image of 2 people, newsroom, dais and text
 
Huyo odero amewekwa na Mbowe ili kuonekane kuna ushindani sio kama anataka kushinda 🐼
 
Back
Top Bottom