MBOWE NA MWANAE WASUSA CHADEMA WAGOMA KUMPA VIFAA VYA MKUTANO LISSU.
Mtoto wa Mbowe (James Mbowe) ambaye ana kesi ya Madai Mahakamani kwa kosa la kutowalipa Mishahara wafanyakazi wake zaidi ya miaka 3 leo ana muhujumu Lissu kwa kumnyima vifaaa vya Mziki na Jukwaa kwa ajili ya Mkutano wake wa mapokezi ya tarehe 15 Feb, 2025 Mkoani Singida.
#NoReformNoElection
Mtoto wa Mbowe (James Mbowe) ambaye ana kesi ya Madai Mahakamani kwa kosa la kutowalipa Mishahara wafanyakazi wake zaidi ya miaka 3 leo ana muhujumu Lissu kwa kumnyima vifaaa vya Mziki na Jukwaa kwa ajili ya Mkutano wake wa mapokezi ya tarehe 15 Feb, 2025 Mkoani Singida.
#NoReformNoElection
- Tunachokijua
- Godbless Lema ni mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA ambaye aliwahi kuwa mwenyekiti wa chama hicho kanda ya Kaskazini. Wakati wa uchaguzi mkuu ndani ya chama hicho uliofanyika January 2025 Lema alikuwa ni miongoni mwa makada ambao walikuwa wakimuunga mkono Tundu Lissu alipokuwa akigombea nafasi ya uenyekiti hadi kushinda dhidi ya Freeman Mbowe aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo kwa miaka 21.
Baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa CHADEMA uliomuweka maradakani Tundu Lissu kuwa Mwenyekiti wa chama hicho akimdondosha mtangulizi wake Freeman Mbowe aliyehudumu nafasi hiyo kwa miaka 21, kumekuwapo na taarifa nyingi zinazosambaa mtandaoni zikidaiwa kutoka pande zote mbili za miamba hii mikubwa kwa siasa za upinzani nchini.
Ikumbukwe kuwa, uchaguzi wa ndani wa CHADEMA ulijitanabaisha kwa kuvuta hisia za watu wengi kutokana na mvutano wa hoja, nguvu za wagombea kwa wapiga kura na mtazamo wa umma juu ya wagombea hao.
Hadi sasa, taarifa nyingi za kuzushwa zimeendelea kutengenezwa na watu, mojawapo ikiwa ni andiko lililodaiwa kuchapishwa na katibu Mkuu wa Chama hicho, John Mnyika kuwaonya team Lissu kuacha mpango wa kutaka kufanya fujo siku ya uchaguzi ambayo JamiiCheck ilikanusha uzushi huo.
Mnamo tarehe 15, Februari 2025 Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu anatarajiwa kupokelewa Ikungi, Mkoani Singida baada ya kuchaguliwa Januari 21, 2025.
Kumekuwapo na taarifa inayosambazwa katika mitandao ya kijamii ikimnukuu Godbless Lema kuwa amechapisha katika ukurasa wake wa mtandao wa X akisema "Mtoto wa Mbowe (James Mbowe) ambaye ana kesi ya Madai Mahakamani kwa kosa la kutowalipa Mishahara wafanyakazi wake zaidi ya miaka 3 leo ana muhujumu Lissu kwa kumnyima vifaaa vya Mziki na Jukwaa kwa ajili ya Mkutano wake wa mapokezi ya tarehe 15 Feb, 2025 Mkoani Singida"
Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck ulibaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli wala haikuchapishwa na Lema katika kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii.
Aidha chapisho hilo limebainika kuwa ni la kutengenezwa ili kupotosha kwa kusambaza taarifa zisizo za kweli.
Hata hivyo madai yanayomlenga James Mbowe kuwa ana kesi ya Madai Mahakamani kwa kosa la kutowalipa Mishahara wafanyakazi wake zaidi ya miaka mitatu si ya kweli na hahusiki na kesi hiyo.
Hata hivyo Lema pamoja na James wameikanusha taarifa hiyo kwa nyakati mbili tofauti kupitia kurasa zao rasmi za mitandao ya kijamii.
Kwa kutumia Key word Search iliyotumia maneno "James Mbowe" JamiiCheck ilibaini kuwa chapisho hilo lilisambazwa zaidi katika mtandao wa Facebook. Tazama hapa, hapa,hapa, hapa, na hapa.