Kwenye Utawala wa awamu ya 5 Bashiru Ally na wateule wengine wa Rais walijipa Utukufu kuliko hata Mitume wa Mungu

Kwenye Utawala wa awamu ya 5 Bashiru Ally na wateule wengine wa Rais walijipa Utukufu kuliko hata Mitume wa Mungu

Hivi kuna kiongozi wa kisiasa mbinafsi kama mbowe? Lema , lisu na mbowe ndio wamejivika Uungu watu pale CDM. Ukitaka yakupate ya kukupata basi nenda ukagombee au uwe na nia na kiti cha Mbowe pale CDM
 
Ni kweli kabisa, Waraka ule ulikua ni Upumbavu wa wapumbavu


Habari njema ni kwamba, Mfumo upo unaishi.


Ipo Siku Dr Bashiru atainuliwa juuuuuu juuuuuu sana.
 
Dkt Bashiru Ally Kakubwa Wa Kemondo Bay Bunazi
 
Dkt Bashiru Ally Kakubwa Wa Kemondo Bay Bunazi
Huyu hapa enzi zile

Screenshot_2024-03-17-12-30-02-1.png


Hapa ndipo alipotangaza kwamba CCM ITASHINDA KWA KUTUMIA DOLA
 
Bado tungali tunaendelea na nyuzi za mwezi wa Mungu .

Dkt Bashiru Ally Kakurwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa ccm na wateule waliojiona wako karibu na Mamlaka ya Uteuzi , walijipa utukufu ambao hakuna kiongozi yoyote aliyewahi kujipa Tangu Nchi hii ipate uhuru wake .

View attachment 2937182

Yaani ilifikia Mkuu wa Wilaya anamvimbia mtu yeyote akiwemo hata Mkuu wa Mkoa wake , kwa vile tu yeye yuko karibu na Rais , haifahamiki kama walikuwa wanatumwa na aliyewateua au la

Kwa Mfano ukiacha Bashiru Ally ambaye kiburi chake na ukosefu wake wa Adabu kwa Wazee akina Makamba na Kinana hakuna aliyeusahau , DC Sabaya , Ally Happy , Alexander Mnyeti pamoja na Paulo Makonda walikuwa Jamhuri huru ndani ya Jamhuri ya Tanzania .

View attachment 2937183

Waliopiga U Turn na kurudi kwenye ubinadamu , japo nao walitaka kuingia kwenye Utukufu huo ni Amos Makalla , Chalamila na Mongela , hawa walianza kama wenzao lakini baadaye wakashikwa masikio .

Mara nyingi tumeonya na kufundisha sana hapa jf na kwingineko kuhusu hizi kazi za Kuteuliwa , kwamba hizi kazi ni Dhamana ya muda mfupi sana , ni vema tukazifanya kwa weledi maana hatujui kesho kutwa.

mwangalie Hapa Bashiru Ally baada ya kupigwa chini na kuteuliwa Mbunge wa viti maalum , Picha hii ikupe somo la kazi za kuteuliwa

View attachment 2937187

Kiburi na dharau za wateule wa awamu ya 5 hakijawahi kuwepo kwenye nchi hii tangu iumbwe na Mungu , kila mteule mwenye kiburi cha madaraka ajaribu kumchukulia Salmin Amour , kama Mfano , Salmin alifikia kuitwa Komando kwa kejeli , matusi na dharau kwa wakubwa zake na wadogo , lakini mnafahu kilichomkuta leo ? hana ukomando wowote tena , hawezi kufika hata Kisiwandui , Kibanda maiti wala Mchamba wima , Utukufu wa Mungu ni wa ajabu sana !

NITASEMA KWELI DAIMA FITNA KWANGU MWIKO
kuna yule mnyanganyi alie okoka, wa kule arachuga anajifanyanga yesu dah 🐒
 
kuna yule mnyanganyi alie okoka, wa kule arachuga anajifanyanga yesu dah 🐒
Jambo moja ambalo wengi hawajajua ni kwamba , Hizi mada hazitoki Chadema , naziandika mimi ambaye pia si Msemaji wa Chadema , kwahiyo mnapowahusisha akina Mbowe huwa nawashangaa sana
 
Watu wakipata vyeo hujisahau sana,kiburi,madharau vinakuwa juu mmno hasa hizi nchi zenye katiba mbovu ambamo viongozi huwa watawala badala ya kubaki viongozi!!
Ubabe wa kijinga,vitisho kujidai miungu watu Leo wamepatara wanaishi Kwa huruma ya walio madarakani.
Tujifunze uungwama tutafit kufanya kazi na aina tofautii za watu...
 
👇
Kwa Mfano ukiacha Bashiru Ally ambaye kiburi chake na ukosefu wake wa Adabu kwa Wazee akina Makamba na Kinana hakuna aliyeusahau.
Kama unajua kiswahili , hapo namuelezea Bashiru Ally alivyo , tena niliandika huku nikitabasamu , aliyechukizwa hawezi kutabasamu
 
Watu wakipata vyeo hujisahau sana,kiburi,madharau vinakuwa juu mmno hasa hizi nchi zenye katiba mbovu ambamo viongozi huwa watawala badala ya kubaki viongozi!!
Ubabe wa kijinga,vitisho kujidai miungu watu Leo wamepatara wanaishi Kwa huruma ya walio madarakani.
Tujifunze uungwama tutafit kufanya kazi na aina tofautii za watu...
Hasa wakidanganywa kwamba aliyewateua atatawala milele
 
Back
Top Bottom