Kwenye Utawala wa awamu ya 5 Bashiru Ally na wateule wengine wa Rais walijipa Utukufu kuliko hata Mitume wa Mungu

Kwenye Utawala wa awamu ya 5 Bashiru Ally na wateule wengine wa Rais walijipa Utukufu kuliko hata Mitume wa Mungu

Bado tungali tunaendelea na nyuzi za mwezi wa Mungu .

Dkt Bashiru Ally Kakurwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa ccm na wateule waliojiona wako karibu na Mamlaka ya Uteuzi , walijipa utukufu ambao hakuna kiongozi yoyote aliyewahi kujipa Tangu Nchi hii ipate uhuru wake .

View attachment 2937182

Yaani ilifikia Mkuu wa Wilaya anamvimbia mtu yeyote akiwemo hata Mkuu wa Mkoa wake , kwa vile tu yeye yuko karibu na Rais , haifahamiki kama walikuwa wanatumwa na aliyewateua au la

Kwa Mfano ukiacha Bashiru Ally ambaye kiburi chake na ukosefu wake wa Adabu kwa Wazee akina Makamba na Kinana hakuna aliyeusahau , DC Sabaya , Ally Happy , Alexander Mnyeti pamoja na Paulo Makonda walikuwa Jamhuri huru ndani ya Jamhuri ya Tanzania .

View attachment 2937183

Waliopiga U Turn na kurudi kwenye ubinadamu , japo nao walitaka kuingia kwenye Utukufu huo ni Amos Makalla , Chalamila na Mongela , hawa walianza kama wenzao lakini baadaye wakashikwa masikio .

Mara nyingi tumeonya na kufundisha sana hapa jf na kwingineko kuhusu hizi kazi za Kuteuliwa , kwamba hizi kazi ni Dhamana ya muda mfupi sana , ni vema tukazifanya kwa weledi maana hatujui kesho kutwa.

mwangalie Hapa Bashiru Ally baada ya kupigwa chini na kuteuliwa Mbunge wa viti maalum , Picha hii ikupe somo la kazi za kuteuliwa

View attachment 2937187

Kiburi na dharau za wateule wa awamu ya 5 hakijawahi kuwepo kwenye nchi hii tangu iumbwe na Mungu , kila mteule mwenye kiburi cha madaraka ajaribu kumchukulia Salmin Amour , kama Mfano , Salmin alifikia kuitwa Komando kwa kejeli , matusi na dharau kwa wakubwa zake na wadogo , lakini mnafahu kilichomkuta leo ? hana ukomando wowote tena , hawezi kufika hata Kisiwandui , Kibanda maiti wala Mchamba wima , Utukufu wa Mungu ni wa ajabu sana !

NITASEMA KWELI DAIMA FITNA KWANGU MWIKO
Mkuu heko sana, tena unavyokoleza na picha unafikisha ujumbe vizuri. Upatapo nafasi weka na video ili tuwe tunakumbushana vizuri na kuelimishana zaidi!
 
sasa hapo mimi wa shule za udongo nitaelewa kweli ?
tulisoma na chairman public administration kule uingereza, chairman ana confidence ila ana misamiati michache 🐒

huwa anatamani kumwaga ung'eng'e mwingi sana, wenye slang, phonology na syntax nyingi sana, lakini ngoma inagoma,
anaishia which which kibao 🐒

si unajua tena kugundua umuhimu wa shule utu uzimami 🐒
 
Screenshot_2024-03-19-13-08-24-1.png
 
Back
Top Bottom